NHIF yazindua huduma Toto Afya Kadi
Meneja
Huduma za Dawa Michael Kishiwa kutoka Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (
NHIF) akiwaeleza waandishi wa habari kuhusu huduma mpya ya mfuko huo
iitwayo “Toto Afya Kadi” inayohusisha watoto wenye umri chini ya miaka
kumi na nane ambao sio wanachama wa kundi la mwajiriwa, Kushoto ni Afisa
Masoko wa Mfuko huo Bi. Sabina Komba.
Baadhi ya waandishiwa Habari wakifuatilia mkutano wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF)
Picha na Hassan Silayo-MAELEZO
……………………………………………………………………………………………………..
Na: Lilian Lundo – MAELEZO
Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) umepanua huduma za mfuko wake kwa k uanzisha huduma mpya iitwayo “Toto Afya Kadi”.
Hayo yameelezwa na Meneja Huduma
za Dawa NHIF Michael Kishiwa leo jijini Dar es Salaam alipokuwa akiongea
na waandishi wa habari.
“Huduma ya Toto Afya Kadi ni
huduma ambayo inahusisha watoto chini wenye umri chini ya miaka kumi na
nane ambao sio wanachama wa kundi la mwajiriwa kwa mwajiri hasa wale
ambao wanalelewa katika vituo vya watoto yatima au wanaolelewa na ndugu
waliokosa fursa ya kujiunga na huduma ya Bima ya Afya,” alisema Kishiwa.
Kishiwa alisema kuwa, mwanachama
ambaye ni mtoto mwenye umri chini ya miaka 18 atatakiwa kujaza fomu
zinazopatikana nchi nzima chini ya uangalizi wa mdhamini ambaye ni mlezi
wake aidha kwenye kituo anacholelewa au mahali anapoishi.
Aidha, Kawishe alisema kuwa
mwanachama wa Toto Afya Kadi atapata huduma zote ambazo mwanachama wa
huduma ya Bima ya Afya ya NHIF anapata na ambazo zimeorodheshwa katika
huduma ambazo zinatolewa na Bima hiyo kwa gharama ya shilingi 50,400 kwa
mwaka.
Pia alisema kwa kijana ambaye
amepita miaka 18 ili kuweza kuendelea kuwa mwanachama wa Bima ya Afya na
hajaajiriwa atatakiwa kujiunga katika vikundi vilivyosajiliwa ili aweze
kusajiliwa katika mfumo wa kikoi kwa kuchangia kiasi cha shilingi
76,800 kwa mwaka.
NHIF ina wanachama asilimia 12 ya
watanzania huku ikiwa na jumla ya vituo 6700 nchi nzima, na mpaka sasa
jumla ya wanachama 2,000 wa Toto Afya kadi wamesajiliwa nchi nzima tangu
ianze Machi, 2016.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni