Ijumaa, 28 Oktoba 2016

RAIS DK. SHEIN AKUTANA NA MFALME WA MOROCCO MOHAMMED VI


vi1
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein (kulia)akipokea mmoja wa Miongoni mwa Misahafu elfu kumi iliyotolewa na Mfalme wa Morocco, Mohammed VI,mara baada ya Swala ya Ijumaa iliyoswaliwa leo katika Msikiti wa Mwembeshauri Mjini Unguja,Mfalme Mohammed VI akiwa katika ziara ya kibinafsi na ujumbe wake, ambapo amefikia katika Park Hyatt Hotel- Shangani Mjimkongwe wa Zanzibar,[Picha na Ikulu.]28/10/2016.
vi2
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein na Mfalme wa Morocco, Mohammed VI, (katikati) pamoja na Viongozi mbali mbali na Ujumbe wa Mfalme wakijumuika na Waislamu wengine wakiswali swala ya Ijumaa iliyoswalishwa na Sheikh Fadhil Soraga katika  Msikiti wa Mwembeshauri Mjini Unguja,Mfalme Mohammed VI yupo Nchini kwa  ziara ya kibinafsi, [Picha na Ikulu.] 28/10/2016.
vi3
Mfalme wa Morocco, Mohammed VI(kulia) akisalimiana na  Katibu wa Mufti wa Zanzibar Sheikh Fadhil Soraga mara baada ya kuswalisha Swala ya Ijumaa katika  Msikiti wa Mwembeshauri Mjini Unguja,Mfalme Mohammed VI yupo Nchini kwa  ziara ya kibinafsi, [Picha na Ikulu.] 28/10/2016.
vi4
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein (kushoto) akifuatana na Mfalme wa Morocco, Mohammed VI, pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Mhe,Ayoub Mohamed Mahmoud (kulia) wakitoka nje ya Msikiti wa Mwembeshauri Mjini Unguja baada ya swala ya Ijumaa leo,[Picha na Ikulu.] 28/10/2016.
vi5
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein (kushoto) akiagana na Mfalme wa Morocco, Mohammed VI, mara baada ya kumalizika kwa swala ya Ijumaa leo katika  Msikiti wa Mwembeshauri Mjini Unguja,Mfalme wa Morocco, Mohammed VI yupo nchini na ujumbe wake kwa ziara ya kibinafsi,[Picha na Ikulu.] 28/10/2016

Jumapili, 23 Oktoba 2016

‘NILIAHIDI, NIMETIMIZA, NITAENDELEA KUTIMIZA’ – RAIS JOHN POMBE MAGUFULI


MSHAMA AWAPA MWEZI MMOJA WAKAZI WA KAZAMOYO ZAIDI YA 600 HUKO SOGA KULIACHIA ENEO


unnamed-4
Mkurugenzi halmashauri ya wilaya ya Kibaha, Tatu Selemani akielezea jambo kwa wananchi wa Soga, walioshiriki kwenye mkutano wa mkuu wa wilaya ya Kibaha Assumpter Mshama wakati alipokwenda kuzungumza hatima ya wana Kazamoyo . 
 (Picha na Mwamvua Mwinyi)
…………………………………………………………………………………………………………………
Na Mwamvua Mwinyi,Soga
WAKAZI zaidi ya 600 waliovamia shamba kwenye Kijiji cha Soga kata ya Soga wilayani Kibaha mkoani Pwani(KAZAMOYO)wamepewa mwezi mmoja kuhama kwenye shamba hilo ambalo limerudishwa mikononi mwa serikali.
Agizo hilo limekuja  baada ya aliyekuwa mmiliki wa shamba hilo Jangil Kasamal kunyanganywa kwa kushindwa kuliendeleza.
Mkuu wa wilaya ya Kibaha ,Assumpter Mshama ,alisema agizo hilo ni kuanzia mwezi huu hadi Novemba 18 
baada ya kutoa miezi miwili tangu agosti hadi oktoba mwaka huu kuwataka waondoke lakini hawakufanya hivyo.
Alitoa kauli hiyo akiwa ameambatana na kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya hiyo kwenye kijiji hicho.
Mshama alielezea kuwa watu hao hawako kisheria hivyo wanapaswa kuondoka ili shamba hilo lenye ukubwa wa hekari 900 litumike kwa shughuli nyingine za kijamii.
“Kamishna wa ardhi ameshatoa maelekezo juu ya shamba hilo kuwa baada ya hati ya umiliki kutenguliwa limerudishwa kwa halmashauri ambayo itaweka huduma za kijamii na si watu kujigawia kama wana Kazamoyo walivyofanya,” alisema Mshama.
Alisema wananchi hao ambao wengi wao wanatokea Jijini Dar es Salaam na kulipa jina eneo hilo kuwa Kazamoyo na kujiwekea uongozi wao ambao hauko kisheria kwa madai ya kushindwa kupatiwa huduma na uongozi wa kijiji cha Soga.
“Kutokana na hali halisi iliyopo na tangu mwanzo tulitoa maagizo muondoke kwani tayari wizara na vyombo husika vimeona kuwa taratibu za kukaa hapo zimekiukwa.
,” alisema Mshama.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Kibaha Tatu Seleman alisema kuwa wamepata barua toka kwa waziri wa ardhi ,nyumba na maendeleo ya makazi ,Wiliamu Lukuvi ikisema kuwa watu hao wako hapo kinyume cha sheria.
Seleman alisema kuwa barua ya Waziri ilikuja baada ya wananchi hao kumwandikia barua wakitaka wamilikishwe eneo hilo ili wkae hapo kihalali.
Mmoja wa wakazi walioko kwenye eneo hilo alifafanua aliingia hapo baada ya kusikia eneo hilo linagawiwa ambalo lilikuwa shamba pori .
Awali Mery Kaijage alisema waliamua kuvamia shamba hilo na kugawana na kuanza kulima na kujenga kutokana na viongozi wa kijiji kuliuza eneo hilo kinyume cha sheria.

SERIKALI MKOANI PWANI YAONGEZA MIEZI MITATU KUWABOMOLEA WALIO NDANI YA HIFADHI YA BARABARA NDANI YA MITA 60


unnamed
 Mkuu wa mkoa wa Pwani mhandisi Evarist Ndikilo akizungumza na baadhi ya wafanyabiashara  na wananchi kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika viwanja vya Bwawani Kibaha.
unnamed-1
Mkuu wa mkoa wa Pwani mhandisi Evarist Ndikilo akiingia kwenye uwanja wa Bwawani Mailmoja Kibaha kuzungumza na wananchi kuhusiana na zoezi la bomoa bomoa lililosogezwa mbele hadi January 23 mwakani.
unnamed-2
Baadhi ya wananchi Mail moja Kibaha wakionekana kusikiliza mkuu wa mkoa wa Pwani mhandisi Evarist Ndikilo. 

(Picha zote na Mwamvua Mwinyi) 
………………………………………………………………………………………………….
Na Mwamvua Mwinyi,Pwani
SERIKALI mkoani Pwani ,imewaongezea muda wafanyabiashara na wananchi waliojenga kwenye eneo la hifadhi ya barabara kuu ya Dar es salaam –Morogoro waliotakiwa kubomolewa novemba 23 mwaka huu badala yake itakuwa January  2017.
Zoezi hilo lilikuwa likihusisha walioingia ndani ya barabara hiyo kuanzia eneo la Kiluvya-Tamco na soko la Mailmoja ambapo wameongezewa miezi mitatu kutokana na soko jipya kuchelewa kujengwa chini ya halmashauri ya Kibaha Mji.
Mkuu wa mkoa wa Pwani ,mhandisi Evarist Ndikilo,aliyasema hayo wakati alipokuwa akizungumza na baadhi ya wafanyabiashara hao na wananchi kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika viwanja vya Bwawani Kibaha.
Aliwataka wahusika hao kuanza kubomoa na kuhama kwa hiari ,ndani ya kipindi hicho kilichoongezwa kabla ya january 23 mwakani .
Hata hivyo mhandisi Ndikilo,alieleza kuwa wafanyabiashara hao hawataondolewa hadi halmashauri ya Mji wa Kibaha itakapojenga soko jingine.
“Maandalizi ya kuhamia kwenye soko jipya hayajakamilika na hakuna chochote kilichojengwa ambapo ni miezi miwili imepita toka TANROADS walipotoa notisi kwa waliojenga kwenye hifadhi hiyo kuondoka likiwemo na soko hilo”
“Maelekezo yametolewa na waziri wa ujenzi ,uchukuzi na mawasiliano kwamba zoezi la bomoabomoa ni mita 60 na siyo mita 120 kama ilivyoonyesha na kutangazwa na wakala wa barabara Tanzania (TANROADS)mkoa wa Pwani,”alisema mhandisi Ndikilo.
Mhandisi Ndikilo alisema  mkurugenzi Jeniffer Omolo kasema mkandarasi kapatikana hivyo namtaka ajenge soko ndani ya siku 30 ili ibakie kujenga vizimba na ujenzi uanze kuanzia wiki ijayo ili wafanyabiashara wapate eneo lao la kufanyia biashara zao.
Alisema ujenzi wa soko utafanyika kwenye eneo la Mnarani maarufu kama Sagulasagula ama Loliondo na wanatarajia kutakuwa na huduma muhimu ikiwemo maji na huduma nyingine zitapatikana.
Alifafanua muda uliopangwa wa miezi mitatu sawa na siku 90 vitu vyote viwe vimekamilika kwani hakutoongezwa muda mwingine hivyo wale waliojenga kwenye eneo ambalo ni hifadhi ya barabara ndani ya mita 60 waanze kuvunja wenyewe bila kusubiri kushurutishwa.
Mhandisi Ndikilo anasema  walionunua kwenye eneo la kitovu cha Mji wanapaswa kujenga haraka.Huu ni wakati wa jamii kukubali mabadiliko hayo ambayo yapo ndani ya sheria ili mji wa Kibaha uweze kuwa katika mpangilio mzuri.
“Lengo letu ni halmashauri ya Mji kuwa manispaa hivyo moja ya vigezo ni kupanga Mji huu ,wananchi watuelewe na wote tunahitaji kupanga Mji wetu alisisitiza .
Nae mwenyekiti wa jumuiya ya wafanyabiashara Tanzania (JWT) mkoa wa Pwani ,Abdallah Ndauka alimshukuru mkuu wa mkoa kwa kutoa muda huo ili kutekelezwa agizo hilo na halmashauri.
Ndauka alisema kuwa utekelezaji wa ujenzi wa soko hilo umechukua muda mrefu kutokana na baadhi ya watendaji kutowajibika ipasavyo na kusababisha mipango mingi kushindwa kukamilika.
Awali mkurugenzi wa mji wa Kibaha Jeniffer Omolo , alikuwa na wakati mgumu baada ya wafanyabiashara kuinua mabango wakitaka mkurugenzi huyo atumbuliwe ama mkuu wa mkoa wa Pwani aondoke nae wakidai ameshindwa kuwajibika .
Kufuatia hali hiyo mhandisi Ndikilo ,alisema anatoa muda wa miezi mitatu kuitisha mkutano mbele ya wananchi ambao watapiga kura endapo kutakuwa na mtendaji ambae ni kero na ataondoka nae.
Alisema serikali ya sasa si ya kubembelezana kwani inahitaji watumishi wa umma  wanaowatumikia wananchi badala ya kufanya kazi kwa mazoea.
Mkurugenzi wa halmashauri ya mji wa Kibaha Jennifer alieleza  kwamba mchoro wa soko ulizinduliwa tangu mwaka 2014 .
Alisema tatizo kubwa ni uhaba wa fedha licha ya mpango uliopo ni kumaliza ujenzi  mapema iwezekanavyo.
Jennifer alisema  soko kwa sasa litahamia eneo la Sagulasagula na fedha zipo na tangazo la kumpata mkandarasi limeshatoka.
Alisema endapo zoezi la bomoa bomoa litafanyika itawasaidia halmashauri kupanga Mji na kuwa na kujenga mabanda ya kupumzikia abiria eneo la stend ya sasa.
Kwa mujibu wa Tanroads mkoani Pwani,awali zoezi hilo lilikuwa lifanyike mwezi agost lakini muda uliongezwa hadi mwezi novemba na kudai wapo watu wengine walishawekewa alama ya X tangu mwaka 2004 .
“Sheria ya barabara ya mwaka 1932 na kufanyiwa marekebisho 1958 kifunga na 52 na marekebisho ya sheria ya barabara na 13 ya mwaka 2007 “
Taratibu za sheria za usimamizi wa barabara kifunga na 30 (b) eneo la hifadhi ya barabara,mita 120 sawa na futi 400 kwenda kila upande kutoka katikati ya barabara ni marufuku kufanya maendelezo yoyote katika eneo hilo.

TBL Group yaadhimisha mwezi wa Saratani ya matiti kwa vitendo


–Yaendesha zoezi la kupima afya za wafanyakazi na familia zao
Wafanyakazi wa kampuni ya  TBL Group katika viwanda vyake vyote nchini vilivyopo katika mikoa ya Dar Es Salaam,Mwanza,Mbeya,Arusha na Kilimanjaro mwishoni mwa wiki walipimwa Saratani ya matiti ikiwemo kupatiwa elimu juu ya ugonjwa huu ambao umekuwa ukiongezeka kwa kasi nchini ikiwa ni maadhimisho ya Mwezi wa Saratani ya Matiti kupitia mpango wa kampuni wa Afya Kwanza.sara1
Maofisa wa TBL Arusha wakifuatilia maelezo ya semina ya afya
sara2
Baadhi ya wafanyakazi wa TBL wakifuatilia mafunzo ya Afya kuhusiana na saratani
sara3
Baadhi ya wafanyakazi wa TBL Dar es Salaam wakifuatilia mafunzo wakati wa semina ya masuala ya saratani ya matiti
sara4
Baadhi ya wafanyakazi wa Konyagi wakiwa katika picha ya pamoja wakati wa semina ya afya kuhusiana na Saratani ya Matiti
sara5
Baadhi ya wafanyakazi wa TBL Mbeya katika picha ya pamoja kabla yakuanza semina ya Saratani ya matiti
sara6
Baadhi ya wafanyakazi wa TBL Mwanza wakati wa mafunzo kuhusiana na saratani ya matiti

MANGULA AFURAHISHWA 100 KUFUKUZWA UANACHAMA WA CCM MWANZA, ASEMA ANAYEFAA KUWA KIONGOZI NI MWENYE UZALENDO WA KUJITOLEA SIYO UHODARI WA HOTUBA


Mzee Philip Mangula
Na Bashir Nkoromo, Mkuranga
MAKAMU Mwenyekiti wa CCM-Bara, Philip Mangula ameelezea kufurahishwa kwake kufukuzwa kwa wanachama 100 mkoani Mwanza kwa kubainika kukisaliti chama wakati wa uchaguzi mkuu uliopita.

“Haiwezekani, unajiita mwanachama, halafu badala ya kujitolea kwa nguvu zako zote chama kishinde vita ya kushika dola, wewe unakisaliti,  hapo unakuwa si mwanachama bali jeshi la kukodiwa”,  Mangula alisema, hayo jana, wakati akizungumza na Vijana wanaosoma na waliohitimu vyuo vikuu 20, ambao wameweka kambi ya kufyatua matofali kwa ajli ya ujenzi wa mabweni na nyumba za walimu katika shule ya Sekondari Nasabagani, Mkuranga mkoa wa Pwani.


 “Taarifa ya Chama kuwafukuza uanachama wale 100 kule Mwanza imenifurahisha sana, ni matumaini yangu kwamba hatua kama hizi zitaendelea kuchukuliwa  kila mahala nchini kote kwa waliokisaliti chama. hivi ni mchezaji gani anayempiga ngwara mchezaji wa timu yake wakati wa mechi ya kutafuta ubingwa halafu akaachwa kuendelea kuwa katika timu?” Mangula alisema na kuhoji kwa mshangao.


Mangua alisema, wakati mikoa itaendelea kuchukua hatua, lakini pia kwa ngazi ya taifa hatua dhidi ya waliokisaliti chama zitaendelea kuchukuliwa, ikiwa ni pamoja na kuwatupilia mbali watakaojaribu kuomba nafasi za uongozi wakati wa uchaguzi wa Chama mwakani, huku wakiwa wameshabainika kuwa walikisaliti chama wakati wa uchaguzi mkuu ulipita.


Mangula aliwataka vijana nchini kote hasa wasomi, kuepuka kutumiwa vibaya na wanachama watakaokuwa wanasaka uongozi wakati wa uchaguzi mkuu wa CCM unaotarajiwa kufanyika mwakani, kwa kuwa kijana yeyote atakayekubali kutumiwa vibaya atakuwa amekisaliti na kuchangia kunyong’onyesha nguvu na uhai wa Chama.


“Hili la kutumiwa vibaya hasa ninyi vijana, nawaasa sana kuepuka nalo, jambo hili ni baya sana, na si kwa Chama tu lakini hata kwa wewe uliyekubali kutumika, maana utatumiwa kama ngazi, halafu akishapita hatakuwa na manufaa kwako na hata kwa taifa maana atakuwa mvurugaji tu, badala ya kushiriki kuleta maendeleo ya chama na taifa”, Alisisitiza mangula.


Alisema, vijana hao 53 waliojitolewa kufyatua matofali kwa ajili ya ujenzi huo wa mabweni na nyumba za walimu, wameonyesha moyo mkubwa wa uzalendo kwa nchi yao, na kwamba huo ndiyo uzalendo wa kweli unaopaswa kuonyeshwa na kila mwananchi hasa viongozi katika ngazi mbalimbali.


Mangula alisema, vijana hao wameoyesha mwamko ule uliokuwa umejengwa na kuwepo wakati wa Baba wa taifa Mwalimu Nyerere, ambao katika miaka ya hivi karibuni hasa baada ya kuanza kwa mfumo wa vyama vingi umetoweka kwa watu kuanza kujinasibu kwa majina ya vyama vyao vya siasa badala ya kuonyesha uzalendo kwa kuisaidia jamii kwa za kujitoea.


Alisema, umefikia wakati sasa kipimo cha kwanza kwa yeyote kupata uongozi iwe ni kutazamwa kama kweli ni mzalendo ambaye yupo mstari wa mbele kufanya kazi za kujitolea katika jamii, na siyo kutazama uwezo wake wa kuzungumza na kumwaga hotuba nzuri majukwaani.


“Sifa za mtu kupewa uongozi isiwe ukasuku wa kutoa talalila za hotuba nzuri za kisiasa majukwaani, kwanza atazwamwe kama amekuwa akitoa mchango gani kwa jamii kwa kufanya kazi za kujitolea katika kusukuma maendeleo ya taifa mbele kama ilivyokuwa wakati wa Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere, hongereni sana vijana kwa kuonyesha moyo wa kfufua uzalendo.”, alisema  Mangula.


Mapema, Katibu wa Kambi ya vijana hao, Daniel Sarungi, alisema, tangu walipoanza kambi hiyo, na kuanza kufyatua matofali Septemba 29, 2016, wameshafywatua matofali zaidi ya 30,000, kati ya lengo lao la matofali 45,000, ambalo watahakikisha wamelifikia kesho Oktoba 24, 2016.


Alisema, vijana hao wamejikusanya kutoka vyuo vikuu 20, vutatu vikiwa ni vya nchi za nje, na wamekuwa wakishirikiana vizuri, tangu kusomba mchanga na kufyatua matofali, kujipikia chakula, kufundisha wanafunzi wa kidato cha tano na sita katika shule hiyo, kutoa huduma ya afya, kushiriki michezo mbalimbali na kufanya semina na mijadala ya kukuza uwezo wa kuleta maendeleo katika jamii.


Sarungi alisema, vijana hao ambao baadhi wameshahitimu masomo na wengine bado wanasoma katika taaluma mbalimbali wameamua kujitolea kusaidia ujenzi wa mabweni na nyumba za walimu, baada ya kuguswa na adha ya kulala chini wanafunzi wa kidato cha tano na cha sita katika shule hiyo huku walimu na wakiwa hawana nyumba za kutosha kuishi.


Wakati wanafunzi waliopo sasa wanalala chini katika chumba cha maabara, nyumba moja yeneye nyumba vitatu inatumiwa na walimu saba kuishi katika nyumba hiyo, haliambayo hairidhishi.


Mapema, Mangula alishiriki kufyatua matofali na baadaye kusema kwamba aliamua kwenda kuwaunga mkono vijana hao baada ya kusikia taarifa zao kwenye vyombo vya habari hatua yao ya kuamua kujitolea kusaidia shule hiyo baada ya kuhamasishwa na Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga, Filberto Sanga ambaye siyo tu amekuwa akiratibu bali amekuwa pia ashiriki katika ufyatuaji huo wa matofali.

Ijumaa, 21 Oktoba 2016

NHC LAFANYA UHAKIKI WA VIKUNDI VYA VIJANA KATIKA MIKOA YA MWANZA, GEITA NA MARA

Jengo la ofisi linalojengwa na vijana wa kikundi cha Sarorya ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa mradi wa vijana wa kutengeneza matofali ya kufungamana kupitia mashine zilizotolewa na NHC kama msaada kwa vijana. Wa Pili Kulia ni Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Huduma kwa Jamii, Susan Omari ambaye aliongoza ujumbe wa NHC  katika uhakiki wa shughuli zinazofanywa na vijana hao baada ya kupewa msaada wa mashine.
nc2
Kanisa lililojengwa na vijana  wa kikundi cha Hope Revival – Manispaa ya Musoma ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa mradi wa vijana wa kutengeneza matofali ya kufungamana kupitia mashine zilizotolewa na NHC kama msaada kwa vijana.
nc3
 Kanisa lililojengwa na vijana  wa kikundi cha Hope Revival – Manispaa ya Musoma ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa mradi wa vijana wa kutengeneza matofali ya kufungamana kupitia mashine zilizotolewa na NHC kama msaada kwa vijana.
nc4
Meneja wa Mkoa wa Mwanza Mhandisi Benedict Kilimba ya utekelezaji wa mradi wa vijana wa kufyatua matofali yanayofungamana kupitia ufadhili wa na NHC wa msaada wa mashine ya kufyatua matofali kwa vijana wa Manispaa ya Ilemela – Mwanza.
nc5
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Huduma kwa Jamii, Susan Omari akiwa katika mahojiano na vyombo vya habari baada ya kuhakiki vikundi vya vijana wa Ukombozi Vijana Magu kwenye eneo lao la kazi wanalotegemea kujenga nyumba.
nc6
Moja ya kazi za vijana wa kikundi cha Sarorya – Halmashauri ya Rorya ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa mradi wa vijana wa kutengeneza matofali ya kufungamana kupitia mashine zilizotolewa na NHC kama msaada kwa vijana.
nc7
Moja ya Nyumba iliyojengwa na vijana wa kikundi cha Ukombozi Vijana – Halmashauri ya Magu.
nc8
 Moja ya Nyumba iliyojengwa na vijana wa kikundi cha Ukombozi Vijana – Halmashauri ya Magu.
nc9
 Nyumba iliyojengwa na kikundi cha Ukombozi Vijana Magu.
nc10
Nyumba iliyogengwa na vijana Ukombozi Vijana Halmashauri ya Magu.
nc11
 Nyumba iliyojengwa na vijana wa kikundi cha JOMUGI Maswa.
nc12
 Nyumba iliyojengwa na vijana wa Misungwi.
nc13
 Nyumba ya mwananchi iliyojengwa na vijana Rorya.
nc14
 Picha ya pamoja na vijana wa kikundi cha Ukombozi Vijana Magu mble ya mojawapo ya nyumba ziliyojengwa na vijana hao
nc15
 Eneo jingine la kazi ya vikundi cha Ukombozi Vijana Magu.
nc16
Eneo la kazi la kufyatua matofali ya vijana wa Misungwi.
nc17
Eneo la kazi la kufyatua matofali ya vijana wa Misungwi.
nc18
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Huduma kwa Jamii, Susan Omari na timu yake ya NHC akikagua matundu kumi  vya choo vilivyojengwa na vijana wa kikundi Jiendeleze – Halmashauri ya Musoma Vijijini.
nc19
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Huduma kwa Jamii, Susan Omari na Ujumbe wa NHC wakipata maelekezo kutoka kwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya wa ya Magu Bw. Lutengano Mwalwiba.
nc20
 Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Huduma kwa Jamii, Susan Omari na Ujumbe wa NHC wakipata maelekezo kutoka kwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti  Bw. Juma Hamsini.
nc21
  Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Huduma kwa Jamii, Susan Omari na Ujumbe wa NHC wakipata maelekezo kutoka kutoka kwa Mkuu wa wilaya ya  Biutiama Bi. Anna Nyamubi.
nc22
 Ujumbe kutoka NHC ukizungumza na Mkurugenzi  Halmashauri ya Mji wa Tarime Bw. Fidelica Myovella.
nc23
Ujumbe wa NHC ukipata maelekeo kutoka kwa Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Rorya Bw. Gasper Mago.