MKUTANO WA LOWASSA NA WANAFUNZI MUHIMBILI WAZUILIWA
Na Dotto Mwaibale
……………………..
UONGOZI
wa Chuo Kikuu cha Sayansi ya Tiba Shirikishi Muhimbili (MUHAS) umezuia
mkutano uliokuwa ufanywe na baadhi ya wanafunzi wa chuo hicho na Waziri
Mkuu wa zamani Edward Lowaasa.
Mkutano
huo ambao ulikuwa ufanyike na baadhi ya vijana wa kikristo ambao ni
wanafunzi wa chuo hicho ulikuwa pangwa kufanyika juzi chuoni hapo
kuanzia saa za mchana.
Akizungumza mtandao wa www. habari za jamii.com
mmoja wa wanafunzi hao ambaye hakupenda kutaja jina lake alisema
maandalizi yote ya mkutano huo ambao ulikuwa baada ya ibada yalikuwa
yamekamilika.
“Tulifanya
taratibu zote ikiwa ni pamoja na kutoa taarifa kwa uongozi wa chuo
ambao ulitukubalia na kumualika ndugu Lowassa lakini tumeshangazwa na
zuio lililotolewa na uongozi wa chuo” alisema mwanafunzi huyo.
Mwanafunzi
huyo alisema kuwa saa sita mchana wakati wakimsubiri mgeni rasmi Edward
Lowassa awasili mkuu wa chuo hicho na viongozi wengine waliwaita na
kuwaeleza kwamba mkutano huo umewekewa zuio kutoka juu hivyo
hautafanyika bila ya kutoa sababu .
Msemaji
wa Lowassa Abubakar Lihongo alisema wanafunzi hao baada ya kuzuiliwa
kufanya mkutano huo walimuomba radhi Lowassa na kumueleza watamualika
tena kipindi kingine wakiwa tayari.
“Mimi
naona zuio hilo linatokana na masuala ya kisiasa lakini kuna barua ya
wanafunzi hao ipo katika mitandao ya kijamii mkiipata mnaweza kupata
picha halisi” alisema Liongo.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni