JPM amaliza mgogoro wa makazi Magomeni Kota
Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imemaliza mgogoro wa makazi wa Magomeni Kota uliodumu kwa kipindi kirefu.
Hayo yamesbainishwa leo jijini
Dar es Salaam na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe.
William Lukuvi wakati akiongea na Kamati ya Mgogoro wa Makazi ya
Magomeni Kota mbele ya waandishi wa habari.
“Mhe. Rais Dkt. John Pombe
Magufuli amefuta hati na mikataba yote inayohusiana na ardhi ya
yaliyokuwa makazi ya Magomeni Kota, Dar es Salaam”,alisema Lukuvi.
Kwa mujibu wa Lukuvi Rais
ameondoa umiliki wa eneo hilo toka Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
(TAMISEMI) na kumilikisha Serikali Kuu ambayo ndiyo itakayosimamia
ujenzi wa nyumba 644 ambazo zitauzwa kwa bei nafuu kwa waliokuwa wakazi
wa Magomeni Kota.
“Tutajenga nyumba 644 na kuwauzia
kwa bei ya jengo na siyo ya ardhi ili kuwapeni unafuu katika
kununua,”alisema Lukuvi huku akishangiliwa na baadhi ya wakazi wa
Magomeni.
Aidha, Lukuvi amesema kuwa
anampongeza Mhe. Rais Magufuli kwa kumaliza mgogoro huu ambao umedumu
kwa muda mrefu na kuongeza kuwa ameagiza timu ya wataalamu wa Wizara
kupima na kuchora michoro kwa ajili ya ujenzi.
Lukuvi amesema katika eneo hilo
zitajengwa nyumba za heshima ambazo kila moja itakuwa na vyumba vitatu
ili kukidhi mahitaji ya kifamilia kwani watu hawa wamekaa kwa miaka
takribani 50 hadi wameshapata wajukuu. Ameongeza kuwa kila mmiliki wa
nyumba hiyo atapewa hati yake hata kama nyumba hiyo itakuwa kwenye
ghorofa.
Lukuvi amesema kuwa Rais ameagiza
maeneo kama ya Magomeni Kota katika mikoa ishirini ya Tanzania Bara
nayo yatakuwa katika mfumo huo wa Magomeni. Kwa mujibu wa Lukuvi wazee
ambao wanakaa kwenye nyumba kama hizo sehemu nyingine wasiondolewe kwani
hao walikuwa watumishi wa umma hivyo Rais amesema wasibughudhiwe.
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa
Kamati ya Mgogoro wa Makazi Magomeni Kota, George Abel ameshukur Mhe
Rais Magufuli na Wazir Lukuvi kwa kutatua mgogoro huo ambao anadai
umewasumbua sana.
Ameahidi kutoa ushirikiana kwa Serikali pindi suala la ujenzi litakapokuwa linaendelea ili kuhakikishaujenzi unaenda haraka.
Naye Wakili ambaye alikuwa
akiendesha kesi hiyo kabla ya Mhe. Rais kuingilia kati, Mhe. Twaha
Tasilima ameonyesha kuridhishwa na utendaji wa Rais Magufuli.
“Rais Dkt Magufuli na Mhe. Waziri
Lukuvi ni watu wa vitendo na si maneno na kweli wanawajali wanyonge,
nawashukuru sana,”alisema Tasilima.
Uamuzi wa kurudisha eneo hilo kwenye Serikali Kuu umetolewa na Rais Magufuli tarehe 10/7/ 2016.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni