watumishi wizara ya mambo ya ndani watakiwa kufanya kazi kwa kufuata taratibu, kanuni na sheria za utumishi

Mtumishi
wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi Bw. Berious Nyasebwa akieleza
changamoto kadhaa zinazoikabili Idara ya Huduma za Sheria kwa
Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali (Hayupo pichani) katika mkutano
uliofanyika leo wizarani hapo leo ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya Wiki
ya Utumishi wa Umma ambayo kilele chake ni leo.
Mtumishi
wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi Bw. Shomari akieleza changamoto
kadhaa zinazoikabili Idara ya Huduma za Sheria kwa Mkurugenzi wa
Utawala na Rasilimali (Hayupo pichani) katika mkutano uliofanyika leo
wizarani hapo ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma
ambayo kilele chake ni leo.
Baadhi
ya Wakurugenzi wa Idara na watumishi mbalimbali wa Wizara ya Mambo ya
Ndani ya Nchi wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kumaliza Mkutano
wao uliofanyika wizarani hapo katika kuadhimisha kilele cha Wiki ya
Utumishi wa Umma.
———————————————————————
Mkurugenzi
wa Utawala na Usimamizi wa Rasilimali watu Wizara ya Mambo ya Ndani ya
Nchi Bi. Lilian Mapfa amewataka watumishi wote wa wizara hiyo kufanya
kazi kwa kufuata taratibu, kanuni na sheria za utumishi wa umma ili
kuleta ufanisi wa kiutendaji katika kuhudumia wananchi.
Mkurugenzi
Mapfa ameyasema hayo leo wakati akipokea changamoto mbalimbali za
kiutumishi kutoka kwa watumishi wa ngazi tofauti wanaofanya kazi katika
wizara hiyo ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma
ambayo kilele chake ni leo.
Bi.
Mapfa amesema kuwa ni muhimu watumishi wakafanya kazi kwa ushirikiano
kwa kuwa ndio nguzo kubwa inayoleta ufanisi wa kiutendaji mahali pa kazi
na hivyo kufanikisha majukumu ya wizara.
Katika
kikao hicho ambacho ni sehemu ya Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa
Umma, Wakurugenzi wa Idara na Wakuu wa Vitengo vya wizara hiyo pia
walishiriki na kupokea kero na changamoto mbalimbali zinazowakabili
watumishi wao.
Miongoni mwa changamoto hizo ni pamoja na malipo ya fedha za likizo, malipo ya kazi kwa muda wa ziada pamoja na vitendea kazi.
Akijibu
hoja mbalimbali zilizotolewa na watumishi hao Bibi. Mapfa amesema kuwa
ofisi yake imepokea changamoto na kero mbalimbali zilizotolewa na hivyo
zitafanyiwa kazi kwa mujibu wa sheria, kanuni na miongozo ya Utumishi wa
Umma.
Aidha
Bibi Mafpa amewataka watumishi wote kuimarisha upendo na amani miongoni
mwao kwani ndio nguzo pekee inayochangia kuleta maendeleo ya kweli ya
wizara na ya mtumishi mmoja mmoja.
Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali
Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni