Wabunge kushiriki harambee ya Media Car Wash
Mjumbe
wa Kamati ya Okoa Maisha ya Waandishi wa habari Bw. Peter Nyanje
akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani)leo jijini Dar es
Salaam kuhusu harambee ya kuosha magari itakayofanyika siku ya Jumamosi
tarehe 25 Juni mjini Dodoma. Kushoto ni Mratibu wa Mratibu wa Media Car
Wash Grace Nacksso
Msanii
wa Bongo Fleva Inspekta Harun akizungumza na waandishi wa habari
(hawapo pichani)leo jijini Dar es Salaam kuhusu harambee ya kuosha
magari itakayofanyika siku ya Jumamosi tarehe 25 Juni mjini
Dodoma.Katikati ni Mjumbe wa Kamati ya Okoa Maisha ya Waandishi wa
habari Bw. Peter Nyanje. Kushoto ni Mratibu wa Mratibu wa Media Car Wash
Grace Nacksso.
Waandishi wa habari wakiwa katika mkutano na Wajumbe wa Kamati ya Okoa Maisha ya Waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam.
Picha na: Frank Shija, Maelezo
————————————————————————–
Na: Frank Shija, MAELEZO
Zaidi
ya waandishi wa Habari 1000 kutoka vyombo mbalimbali kunufaika na Mfuko
wa Bima ya Afya kupitia msaada kutoka kwa Kamati ya Okoa Maisha ya
Waandishi wa habari.
Hayo
yamebainishwa leo jijini Dar es Salaam na mjumbe wa kamati hiyo Peter
Nyanje wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu harambe ya
maalum ya kuosha magari Media Car Wash for health itakayofanyika tarehe
25 Juni mjini Dodoma.
“Lengo
la harambee hiyo ni kukusanya zaidi ya fedha takribani shilingi milioni
200 ambazo zitatumika kuwakatia Bima ya Afya waandishi zaidi ya 1000
hapa nchini.”Alisema Nyanje.
Nyanje
amesema kuwa harambe hiyo itakuwa ni yapili ikitanguliwa na ile
iliyofanyika katika viwanja vya Leaders jijni Dar es Salaam na
kufanikiwa kukusanya zaidi ya shilingi milioni 30 ambazo zilisaidai
kugharamia matibabu kwa waandishi watatu waliokuwa taabani.
Aliongeza
kuwa na harambee hiyo imekusudia kuhakikisha waandishi wengi zaidi
wanakatiwa Bima ya Afya, ili kujikinga na kadhia ya kuchangiwa fedha
pale wanapofikwa na maradhi.
Kwa upande wake Mratibu wa Media Car Wash Grace
Nacksso ametoa rai kwa Wabunge, viongozi mbalimbali na wakazi wa mji wa
Dodoma kujitokeza kwa wingi katika katika viwanja vya Jamhuri ili
kushiriki katika zoezi hilo ambapo watu wataoshewa magari yao na watu
maarufu wakiwemo wasanii wa Bongo fleva ,Bongo Movie na Miss Tanzania
Lilian Kamazima.
Grace
amesema kuwa wao kama waratibu wa harambee hiyo wamejidhatiti
kuhakikisha harambee hiyo inafanyikiwa ili kutimiza azma ya kusaidiana
miongoni mwa wanataaluma ya habari nchini.
Harambe
ya Media Car Wash itakayofanyika mjini Dodoma inatahudhuriwa na watu
mashuhuri wakiwemo wasanii Joh Makini, Inspekta Haroun, Nikki Wa Pili,
G. Nako, Aunt Ezekiel,Kajala Masanja, Ray Kigosi, Jacob Steven (JB)
pamoja na Miss Tanzania Lilian Kamazima
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni