NA MWANDISHI WETU, DAR
KAMPUNI ya Hope Light Film inayojishughulisha
na uandaaji wa filamu,Documenti na shughuli mbalimbali ambazo zinawiana na
uchukuaji wa picha za mnato na video imeunda group ambalo litaweka ukaribu
baina ya wadau na mashabiki wa filamu za
Bongo Movie katika kujadiliana mambo mbalimbali katika uendelezaji wa kazi za
sanaa nchini.
Akitoa taarifa hiyo kupitia
mtandao wa kijamii wa Facebook,Mkurugenzi wa kampuni hiyo,Ally Njenje,alisema
kuwa ameunda kundi la ALLY NJENJE FANS kupitia Whatsap na Facebook ili kuwaleta
pamoja wadau na mashabiki wa kazi za filamu za bongo movie za hapa nchini
pamoja na kuunganisha katika mzunguko wa biashara kwa wao kama hope Light Film
kutangaza kazi zao na kwa watu wengine pia kutangaza biashara zao ambapo
linakuwa kundi la kubadilishana mawazo ya kujiinua kiuchumi lakini pia
kusapotiana katika suala zima la biashara.
Ally Njenje
“Ndugu zangu wadau wa Kampuni ya
Hope Light Film napenda kuwajuza kuwa nimeunda group la ALLY NJENJE FANS ambalo
linaweka karibu mashabiki wa kazi zetu na kwa sababu wewe ni shabiki wangu nami
pia ni shabiki wako ambapo katika kundi hili ni vyema kila mtu ajitambulishe
kwa kazi anayofanya ili tupeane fursa wenyewe kwa wenyewe kwa mfano nikijua
wewe unafanya biashara aina fulani basi humu kaa ukijua kuna wateja wako mmoja
wapo ni mimi Ally Njenje lakini isiwe biashara hatarishi”Alisema Njenje
Aidha amesema kuwa watu wote
watakaojiunga na kundi hilo watapata fursa ya kuwa wa kwanza kuangalia kazi za
Hope Light Film na kwa wale wote watakaokuwa tayari kuisambaza kwenye libraly
zao au zilizokuwa karibu yao au kwa wateja wowote wale na kwa mwanakundi yeyote
atakayekuwa tayari kuchukua copy kadhaa ambazo ataenda kuziuza kwa kila copy
atakayouza kutakuwa na pesa yake ni mwanakikundi na uwezo wake wa uchakarikaji
katika uuzaji wa kazi hizo.
“Ndio maana nasema kuwa ukiwa
ndani ya kundi hili utakuwa wa kwanza kuona kazi zangu na kazi za Hope Light
Film ili uangalie uzuri wake na kuangalia wapi utapeleka kuuza kazi hizo suala
hili ni la hiyari sio shuruti kwa mwenye kuiona fursa hii ya biashara ambayo
itakusaidia wewe na mimi kupata faida katika kundi hili anakaribishwa sana”Alisema
Njenje
Aliongeza kwa kutoa nafasi kwa mtu
yeyote mwenye kuona ana kipaji na ana nia ya kushiriki katika kampuni yake kama
muigizaji na akaongeza kusema kuna nafasi nyingi sana ambazo zinahitaji watu
kama uandishi wa stori za filamu,upigaji wa picha za mnato na jongefu,kuongoza
filamu,kuwafanyia make up waigizaji pamoja na kuwa mshauri katika uboreshaji wa
utengezaji wa filamu za Hope Light Film ili kutoa kazi bora.
“Kama unahisi ndozto zako ni
kuigiza na hayo niliyoainisha hapo juu ukiwa kama kijana au mtu wa rika lolote
nakukaribisha kwenye group hili ili tufahamiane na kusaidiana katika kujikwamua
kiuchumi na kimaisha pia nataraji siku za karibuni kuanzisha academy ya kulea
watoto na watu wakubwa katika kuwajenga kisanaa kwa kuwa naamini mimi ni msaada
mkubwa kwao nitajitolea kutoa elimu ya uigizaji na kuwapa nafasi wewe,kijana
wako au ndugu yako aliyeunganishwa au kupata taarifa hii kupitia mtu
aliyejiunga katika group langu la Ally Njenje Fans kwa sababu umenipa thamani
kubwa name napaswa kukurudishia thamani hiyo”Alisema Njenje
Alimaliza kwa kutoa wito kwa watu
wote wenye kuona wanaweza kuchangamkia fursa hiyo wajitokeze mapema kumtafuta
kupitia mtandao wa facebook kwa jina la Ally Njenje au kwa Whatsap namba yake 0713103521
na kutoa angalizo kuwa katika kundi hilo heshima na maadili ya mtanzania
yazingatiwe kwa kuwa ni katika kundi hilo kutakuwa na watu wa rika mbalimbali
na kushauri watu kuacha tabia ya kufuatana inbox kuelezana mambo ya kijinga
wengi wao katika kundi hilo wana ndoa zao
mtu anapokuchekea haimaanishi anakutaka au anastahili kusumbuliwa mtu
anapokuheshimu na yeye mheshimu.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni