UTUMISHI YAWAAGA WATAALAMU 7 WA KUJITOLEA KUTOKA JAPANI WALIOMALIZA MUDA WA KUTOA HUDUMA NCHINI

Kaimu
Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais-Utumishi, Bw. Mick Kiliba (kushoto)
akikabidhi zawadi kwa Mtaalam wa Kujitolea kutoka nchini Japani Bw.
Kosuke MATSUDA aliyemaliza muda wake wa kutoa huduma nchini katika
hafla fupi ya kuwaaga wataalam hao iliyofanyika ukumbi wa Ofisi ya
Rais-Utumishi mapema leo.
Kaimu
Katibu Mkuu Ofisi ya Rais- Utumishi, Bw.Mick Kiliba ( wa tatu kutoka
kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na Wataalam wa Kujitolea kutoka
nchini Japan waliomaliza muda wao wa kutoa huduma nchini baada ya hafla
fupi ya kuwaaga iliyofanyika ofisini kwake leo. Wengine ni watumishi wa
Ofisi ya Rais-Utumishi na wawakilishi kutoka JICA.
Kaimu
Katibu Mkuu Ofisi ya Rais- Utumishi, Bw.Mick Kiliba (kulia) akifuatilia
maelezo ya Bi. Yuka ITO ya namna alivyofanya kazi katika Hospitali ya
Mkoa wa Mtwara (Ligula) wakati wa hafla fupi ya kuwaaga wataalam wa
kujitolea kutoka nchini Japan waliomaliza muda wao iliyofanyika ukumbi
wa Ofisi ya Rais-Utumishi mapema leo.
Kaimu
Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais-Utumishi, Bw. Mick Kiliba (kushoto)
akikabidhi zawadi kwa Mtaalam wa Kujitolea kutoka nchini Japani Bi. Yuka
ITO aliyemaliza muda wake wa kutoa huduma nchini katika hafla fupi ya
kuwaaga wataalam hao iliyofanyika ukumbi wa Ofisi ya Rais-Utumishi
mapema leo.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni