SADC kudumisha usalama katika usafiri wa Anga.

Waziri wa Kazi, Usafiri na Mawasiliano Mh. Makame Mbarawa akiongea na wadau mbali mbali wa Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi zilizopo kusini mwa Afrika (SADC) hawap[o pichani katika ufunguzi wa mkutano wa 19 wa kamati ya SADC usafiri wa anga uliofanyika jijini Dar es salaam.
……………………………………………………………………………………….
Na Ally Daud-Maelezo
Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi
zilizopo kusini mwa Afrika (SADC) imeadhimia kuimarisha usafiri wa anga
ili luleta huduma bora na kuwapa amani wananchi wanaotumia usafari wa
anga katika Jumuiya hiyo.
Hayo yamesemwa leo na Waziri wa
Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mheshimiwa Makame Mbarawa alipokuwa
akifungua Mkutano wa 19 wa Kamati ya SADC ya usafiri wa Anga
uliofanyika jijini Dar es salaam.
“Mkutano huu unalenga kuadhimia
kuimarisha usalama wa anga katika nchi za Jumuiya ya SADC, kwa kuwa
unahitajika sana kwa wananchi ili kuongeza shughuli za kiuchumi na
kijamii na kuleta maendeleo ya nchi wanachama” alisema Mbarawa
Ameongeza kuwa “ni lazima
tuadhimie mambo yatayoleta maendeleo na huduma bora katika usafiri wa
anga kwa jumuiya ya SADC ili kujenga uhusiano na malengo yaliyo bora kwa
maendeleo ya nchi zetu.”
Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkuu
wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga nchini Bwana Hamza Johari amesema kuwa
mkutano huo unalenga kuhakikisha wanafikia na kutekeleza malengo
Jumuiya ya usafiri wa anga wa kimataifa (ICAO) katika kuboresha huduma
za usafiri huo.
“Ni lazima tuyafanyiekazi
maadhimio ya mkutano huu ili kuboresha huduma kwa kiwango cha
kimataifa pamoja na kuleta unafuu kwa watumiaji wa usafiri wa anga”
alisisitiza Bw. Johari.
Naye, Mwenyekiti wa SADC Bw.
Geoffrey Moshabesha amesema kuwa kamati hiyo inajipanga kuunda taasisi
ya kiusalama ili kusimamia mifumo yote kwa nchi nzima ili kuweka
mazingira mazuri kwa watumiaji wa usafiri wa anga.
Jumuiya ya SADC imeweka mikakati
ya kutekeleza maadhimio hayo katika kuleta usalama wa anga pamoja na
kutunza mazingira ili kuboresha huduma kwa watumiaji wa usafiri wa anga
kwa nchi wanachama.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni