BENKI YA DIAMOND TRUST YAANZISHA KAMPENI MAALUMU KATIKA MITANDAO YA KIJAMII
BENKI ya Diamond Trust Tanzania
(DTBT) imeanzisha kampeni maalum kupitia mitandao ya kijamii ambayo
inalenga kutoa uelewa juu ya huduma wanazotoa kwa wateja na wadau
mbalimbali. Mbali na hayo kampeni hiyo iliyopewa jina la ‘miaka 70
jiunge nasi ushinde’ imedhamiria kuwapa wadau wake zawadi mbalimbali
hususani wanaowafuatilia kupitia mitandao ya kijamii ukiwemo Facebook.
Picha: MKUU wa
Kitengo cha ICT kutoka Benki ya Diamond Trust Tanzania,Stella Mosha
(kushoto) akitoa zawadi kwa mmoja wa washindi wa kampeni yao ya ‘miaka
70 jiunge nasi ushinde’,Said Mpanju kutoka KIBAHA mkoani Pwani,mwishoni
mwa wiki.Picha na DTBT 9( Na Mpiga Picha Wetu)
Hayo yalibainishwa Jana kupitia
taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa na benki hiyo huku ikisisitiza
zawadi nyingi zitaenda kwa watakaokuwa wanajibu vema maswali kupitia
mitandao hiyo. Kwa mujibu wa taarifa hiyo maswali mengi yatakuwa katika
ukurasa wa benki wa,www.Facebook.com/DTB Tanzania.
“Miongoni mwa zawadi hizo in jezi
za michezo,tiketi za sinema,vocha za manunuzi,Samsung Galaxy J7,simu za
kisasa na kompyuta mpakato,”ilifafanua sehemu ya taarifa hiyo. Kwa
mujibu wa taarifa hiyo kampeni hiyo ni muendelezo wa shamrashamra za
maadhimisho ya miaka 70 ya DTBT kutoa huduma nchini ambayo imekuwa na
mafanikio makubwa.
“DTB Tanzania imejizatiti
kikamilifu kuwafikishia wateja wetu wa thamani huduma bora ikiwemo
kupitia majukwaa haya ya kidigitali,” alibainisha MKUU wa Kitengo cha
Huduma na Masoko DTBT,Sylivester Bahati. Aliongeza kuwa,mitandao ya
kijamii itawasaidia kuwasiliana moja kwa moja na wadau wao wakiwemo
wateja ili kupeana tasrifa juu ya Yale yanayojiri katika jamii na ndani
ya banki. “Pia tumejipanga kuongeza ukaribu zaidi na wadau wetu.Kwani
tumejipanga kuwapa huduma bora zaidi,” alisema.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni