Jumapili, 1 Mei 2016

YALIYOJIRI SIKU YA MEI MOSI UWANJA WA JAMUHURI MJINI DODOMA JANA

F 
Rais John Pombe Magufuli , Makamu wa Rais, Samia Suluhu, Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu,Sera,Bunge, Ajira, Kazi, Vijana na Watu Wenye Ulemavu, Jenista Mhagama  (wapili kushoto) wakishiriki kuimba wimbo maalum wa mshikamano wa wafanyakazi katika sherehe za Mei Mosi zilizofanyika kitaifa kwenye uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma na kuhutubiwa na Rais, Mei 1, 2016.  Wapili kulia ni Rais wa Shirikisho la Wafanyakazi  Tanzania (TUCTA), Gratian Mukoba.
D 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na wazee wa Dodoma baada ya Rais John Magufuli kuhutubia katika sherehe za Mei Mosi kwenye uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma Mei1, 2016.
(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

1Rais Dkt. John Magufuli,  akimkabidhi cheti cha mfanyakazi bora wa mwaka 2015 Enock Kalege, na zawadi ya Sh. milioni 5 iliyotolewa na Mfuko wa Pensheni wa PPF kwa mfanyakazi huyo bora wa mwaka, wakati wa Kilele cha sherehe za Mei Mosi zilizofanyika Kitaifa mkoani Dodoma leo,Mei 1,2016.
2Kutoka kushoto, ni Kaimu Murugenzi wa Bernard Konga,Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni PPF, William Erio na Mkurugenzi Mkuu wa LAPF Eliud Sanga, wakiwa katika sherehe za Mei Mosi Mkoani Dodoma leo,
Picha na Mpiga Picha Wetu

GU1 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwahutubia mamia ya Wafanyakazi katika kilele cha Maadhimisho ya Sherehe za Siku ya Wafanyakazi Duniani zulizofanyika Kitaifa katika Uwanja wa Jamhuri mkoani Dodoma.
GU2 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa ameshikana mikono na viongozi wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi TUCTA wakati wakiimba wimbo wa Mshikamano Daima katika kilele cha Maadhimisho ya Sherehe za Siku ya Wafanyakazi Duniani zilizofanyika Kitaifa katika Uwanja wa Jamhuri mkoani Dodoma .
GU3 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimkabidhi kombe la ushindi wa jumla kwa Rais wa TUCTA Gratian Mukoba katika kilele cha Maadhimisho ya Sherehe za Siku ya Wafanyakazi Duniani zilizofanyika Kitaifa katika Uwanja wa Jamhuri mkoani Dodoma.
GU4 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimkabidhi Cheti cha Mfanyakazi bora kutoka Ofisi ya Rais Ikulu Ndugu Peter Chisunga katika kilele cha Maadhimisho ya Sherehe za Siku ya Wafanyakazi  Duniani zilizofanyika  Kitaifa katika Uwanja wa Jamhuri mkoani Dodoma.
GU5 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiangalia namna ya uokozi katika majanga mabalimbali yanayotokea Migodini nje ya uwanja wa Jamhuri mkoani Dodoma.
GU7 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiifurahi picha yake ya kuchora alipokabidhiwa wakati anakagua mabanda ya Maonesho katika katika kilele cha Maadhimisho ya Sherehe za Siku ya Wafanyakazi Duniania zilizofanyika    Kitaifa katika Uwanja wa Jamhuri Mkoani Dodoma.
GU8 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisikiliza maelezo kutoka kwenye banda la mamlaka ya udhibiti wa mifuko ya hifadhi ya jamii SSRA mjini Dodoma .
GU9 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisikiliza maelezo kutoka kwenye banda la Wakala wa Afya na Usalama mahala pa kazi OSHA mkoani Dodoma
GU10 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Katibu Mkuu wa Shirikisho la Wafanyakazi wa Tanzania TUCTA Ndugu Nicholas Mgaya mara baada ya kuwasili katika viwanja vya Jamhuri Mkoani Dodoma
GU11 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Rais wa TUCTA Gratian Mukoba wakati alipowasili katika katika viwanja vya Jamhuri Mkoani Dodoma.
GU12 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na wazee wa mkoa wa Dodoma mara baada ya kuhutubia katika kilele cha Maadhimisho hayo ya siku ya Wafanyakazi Duniani zilizofanyika Kitaifa Mkoani Dodoma.
GU13 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipunga mkono kuagana na mamia ya wafanyakazi katika uwanja wa Jamhuri mkoani Dodoma.
GU14 
Sehemu ndogo ikionesha wafanyakazi waliojitokeza katika Uwanja wa Jamhuri mkoani Dodoma katika kilele cha sherehe za Siku ya Wafanyakazi Duniani zilizofanyika Kitaifa Mkoani Dodoma. 
PICHA NA IKULU

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni