WANANCHI WA KITONGOJI CHA PERA CHALINZE WAANZA KAMPENI YA KUPAMBANA NA MLIPUKO WA KIPINDUPINDU
By Newsroom on May 9, 2016
Baadhi
ya wafanyabishara katika kitongoji cha pera Chalinze wakiwa katika
Mkutano huo wa kujadili masuala ya usafi pamoja na kupambana na
kipindupindu.
………………………………………………………………………………………………
NA VICTOR MASANGU, CHALINZE
KATIKA kuunga mkono juhudi za
serikali katika kupambana na magonjwa ya mlipuko ikiwemo kipindupindu
wafanyabiashara mbali mbali katika kitongoji cha Pera halmashauri ya
Chalinze Mkoa wa Pwani wameungana na kuanzisha kampeni maalumu kwa
ajili ya kutokomeza taka zote zinakuwa zikitupwa ovyo.
Wakizungumza kwa nyakati
tofauti katika kikao kilichoandaliwa kwa ajili ya kuweza kujadili
mambo mbali mbali kuhusiana na suala la usafi pamoja na kupanga
mikakati ya kuweza kuhakikisha wanapambana vilivyo na mlipuko wa
ugonjwa wa kipindu pindu.
Wafanyabishara hao akiwemo
Rashid Kirumbi,William Mshauri Pamoja na Mwanaidi Tambiligogo walisema
kwamba kwa sasa wanafanya kazi zao katika wakati mgumu sana kutokana na
kitongoji hicho cha pera hakina eneo la kutupia taka hivyo kusababisha
kuzagaa kwa uchafu mwingi ambao unaweza kuleta madhara makubwa kwa
wananchi wa eneo hilo.
Aidha walisema kwamba kwa sasa
katika eneo hilo la pera hakuna eneo maalumu kwa ajili ya kutupia taka
ukizingatia na wafanyabiashara hao wanazalisha taka nyingi kwa siku
hivyo hivyo kuwapa wakati mgumu pindi wanapotaka kutupa taka.
“Hapa kitu kikubwa kikao hiki
kimeandaliwa kwa lengo a kuweka mikakati ya kupambana na mlipuko wa
magonjwa hususan ugonjwa wa kipindupindu ambao kwa sasa umeongia katika
eneo hili kwa hiyo sisis kama wafanyabiashara inatubidi tuhakikishe
kwamba tunafanya usafi katika maeneo yetu ambayo tunafanyia biashara na
hili suala inabidi wote kwa pamoja tushirikiane na serikai
yetu,”walisema wafanyabiashara hao.
Pia walibainisha kuwa kwa sasa
wanajipanga kwa ajili ya kuhakikisha kuwa wanatafuta eneo maalumu la
kutupia taka hizo, pamoja na kuwa na gari ambalo litakuwa likipita
katika maeneo mabali mbali kwa ajili ya kuweza kuzikusanya taka hizo la
kwenda kuzipeleka dampo.
Nao wajumbe wa serikali ya
kitongoji hicho cha pera akiwemo Simon Mbena pamoja na Nadhil Abdallah
walisema kwamba kwa sasa hali ya ugonjwa wa kipindu pindu katika eneo
hilo ni mbaya hivyo kunahitajika juhudi za makusudi katika kufanya usafi
katika sehemu za biashara na majumbani ikiwemo sambamba na kutenga eneo
kwa ajili ya dampo maalumu la kutupitia taka hizo.
Awali akifungua kikao hicho
Mwenyekiti wa mamlaka ya mji mdogo wa Chalinze Hussein Mramba amekiri
kutokuwepo kwa eneo la serikali lililotengwa katika kitongoji hicho kwa
ajili ya matumizi ya kutupa taka,na kubainisha kwamba tayari kuna
wagonjwa watano wa kipindu pindu ambao tayari wamesharipotiwa hivi
karibuni katika eneo la Chalinze.
Mramba alisema kwamba nia ya
serikali ni kuweza kuhakikisha kwamba wanapambana na ugonjwa huo wa
kipindu pindu hivyo atashirikiana bega kwa began a wananchi wa kitongoji
hicho cha pera ili kuweza kulitafutia ufumbuzi suala hilo na kuongeza
kuwa kwa sasa wapo katika hatua za awali za kutafuta eneo maalumu kwa
ajili ya kutupia taka.
KITONGOJI hicho cha Pera
kilichopo katika mamlaka ya mji mdogo Chalinze Wilaya ya Bagamoyo Mkoa
wa Pwani hakina dampo la kutupia taka, na kupelekea wafanyabiashara na
wananchi kuamua kuzitupa sehemu yoyote hali ambayo inachangia kwa kiasi
kikubwa kuzagaa kwa uchafu huo ambao umedai unasababisha kutokea kwa
magonjwa ya mlipuko hasa katika kipindi hiki cha masika.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni