TFF YATUMA SALAMU ZA RAMBIRAMBI MREFA

Katika salamu zake, Malinzi amewapa pole familia ya marehemu Kavenga, ndugu, jamaa, marafiki na MREFA na kusema kwa niaba ya familia ya mpira wa miguu nchin, TFF ipo pamoja nao katika kipindi hichi kigumu cha maombolezo
Mipango ya mazishi inafanywa nyumbani kwa marehemu Block T, Mbeya na kwamba mwili wa marehemu Kavenga unatarajiwa kusafirishwa kesho Jumatatu Mei 9, 2016 kwenda Dodoma, ambapo mazishi yanatarajiwa kufanyika Jumatano, Mei 11, 2016 katika mji wa Mpwapwa mkoani humo.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni