TAARIFA YA MKUU WA WILAYA :MAANDAMANO YA WALIMU BUKOMBE NI BATILI

Aidha Mkuu wa Wilaya amekitaka
chama cha Walimu kama hakikuridhishwa na majibu ya hoja zao, bado kina
nafasi ya kukutana tena na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya na
Kuzungumzia masuala hayo badala ya kufanya maandamano ambayo yataathiri
shughuli za mitihani ya “Mock” kwa kidato cha nne iliyoanza tarehe 10
hadi 20/05/2015 na ile ya “STEP” chini ya BRN kwa shule za sekondari
iliyoanza tarehe 16 hadi 20/05/2016.
Kamati kuu ya Ulinzi na usalama
ipo imara kudhibiti maandamano hayo na vitendo vyovyote vinavyoashiria
uvunjifu wa Amani katika Wilaya ya Bukombe.
Imetolewa na
Ofisi ya Mkuu wa Wilaya Bukombe
Geita
17 Mei, 2016
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni