SERIKALI MKOANI MBEYA YAFUTA HATI YA KIWANJA CHA MAKAZI KILICHOTOLEWA NA HALMASHAURI YA JIJI LA MBEYA
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Amosi Makala (Picha Maktaba
……………………………………………………………………………………………..
Na EmanuelMadafa,Mbeya(Jamiimojablogu
SERIKALI Mkoani Mbeya imeagiza kufutwa kwa hati ya kiwanja
kilichotolewa na halmashauri ya Jiji la Mbeya kwenye chanzo kikuu cha maji
kilichopo eneo la Nyibuko kata ya Mwakibete kwa matumizi ya makazi.
kilichotolewa na halmashauri ya Jiji la Mbeya kwenye chanzo kikuu cha maji
kilichopo eneo la Nyibuko kata ya Mwakibete kwa matumizi ya makazi.
Agizo hilo, limetolwa na Mkuu wa
Mkoa wa Mbeya Amos Makala mara baada ya kutembelea na kukagua chanzo
kikuu cha maji cha Nzovwe, chenye uwezo wa kuzalisha mita 12 za ujazo
kwa siku na
kusambaza maji kwa asilimia 41 kwa wakazi wa jiji la Mbeya wapatao zaidi
ya 200,000. Kiwanja hicho ambacho kipo karibu na eneo la chanzo cha maji cha Nzovwe, kilitolewa na maafisa ardhi, idara ya mipango miji kwa ajili ya matumizi ya makazi na kumilikiwa na mtu binafsi aliyetajwa kwa jina moja la Mwakasala.

Makala amesema, chanzo hicho cha
maji ndio tegemezi kwa kusambaza huduma ya maji kwa wananchi wa Jiji la
Mbeya, hivyo kama kitaachwa na kuharibiwa, wananchi zaidi ya 200,000
wapo hatarini kuikosa huduma
hiyo ambayo ni haki yao ya msingi.
hiyo ambayo ni haki yao ya msingi.
Mkuu huyo wa Mkoa amesema
Serikali iliwaondoa wananchi wote waliokuwa wanaishi au kuendesha
shughuli zao za kiuchumi ndani ya mita 60 na kuwalipa fidia zao hivyo
hatua ya wananchi hao kuendelea kuishia
mahali hapo ni kukaidi agizo la serikali.
mahali hapo ni kukaidi agizo la serikali.
Amebainisha kuwa kiwango kikubwa
cha upotevu wa maji kwa asilimia 31 inatokana na baadhi ya vyanzo vya
maji kuharibiwa kwa kufanyika kwa shughuli za kibinadamu, kulisha mifugo
au kujenga
nyumba za makazi pamoja na mabadiliko ya kihaidrolojia.
nyumba za makazi pamoja na mabadiliko ya kihaidrolojia.
Hata hivyo, Mkuu huyo aliutaka uongozi wa mamlaka ya maji kwa kushirikiana na Mkurugenzi wa halmashauri ya
Jiji la Mbeya, kuhakikisha wanalisiamamia zoezi hilo la kumondoa mvamizi huyo
ndani ya siku tatu.
Jiji la Mbeya, kuhakikisha wanalisiamamia zoezi hilo la kumondoa mvamizi huyo
ndani ya siku tatu.
“Wananchi wengine wameondoka tena
kwa hiari yao wenyewe, sasa kwa nini huyu atuchezee mchezo mchafu?.. kwa
hili sikubaliani nalo, huku akiwataka wananchi ambao ni vijana
kulilinda eneo hilo
na kuwaonya wale ambao watakubali kutumiwa na mtu au watu kufanya
fujo,”alisema.
na kuwaonya wale ambao watakubali kutumiwa na mtu au watu kufanya
fujo,”alisema.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni