NAIBU KATIBU MKUU WA WIZARA YA NISHATI NA MADINI FROF. JAMES MDOE AFUNGA MKUTANO WA JOTOARDHI JIJINI DAR ES SALAAM
Naibu
Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini anayeshughulikia madini,
Prof. James Mdoe ( wa nne kutoka kulia) akisoma hotuba ya ufungaji wa
mkutano wa siku tatu uliokutanisha wataalam wa masuala ya jotoardhi
kutoka katika nchi za Tanzania, Kenya, Uganda, Rwanda, Ethiopia,
Eritrea, Marekani, New Zealand na Djibouti kwa ajili ya kujadili
taarifa ya mtaalam mwelekezi kuhusu utafiti uliofanywa katika Ziwa
Ngozi lililopo mkoani Mbeya ambapo kuna viashiria vya jotoardhi
pamoja na eneo la Kibiro nchini Uganda.
Naibu
Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini anayeshughulikia madini,
Prof. James Mdoe (kushoto) akisisitiza jambo wakati alipokuwa akifunga
mkutano huo. Kulia ni Mjiolojia Mkuu kutoka Idara ya Nishati, Wizara ya
Nishati na Madini, Jacob Mayalla.
Sehemu
ya washiriki wa mkutano huo wakifuatilia kwa makini hotuba ya ufungaji
iliyokuwa inatolewa na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini
anayeshughulikia madini, Prof. James Mdoe (hayupo pichani)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni