Jumanne, 10 Mei 2016

MFUKO YA MAENDELEO YA VIJIJINI WATANGAZA WASHINDI WA SHINDANO LA ONGEZA KIPATO



NA RAYMOND URIO, Dar


KATIKA kuhakikisha sekta kilimo na wafanyabishara na watu waliochini ki maisha hapa nchini Shirika lisilo lakiserikali la Mastercard Fundation For Rural prosperity, limeanzisha miradi ya mikopo katika kuwasaidia wakulima wadogo na wafanyabiashara, watu walio katika hali ya chini ili kuwawezesha kiuchumi na kuondokana na hali ya umasikini.

Mikopo yenye thamani ya dola za kimarekani milioni 35 fedha hizo zitagawiwa katika vikundi vya akiba,bima na mikopo kwa manufaa ya karibu takribani milioni 8, katika maeneo ya vijijini kwa Afrika vinavyojishughulisha na kilimo, wafanyabiashara na walipo katika kaya masikini zilizopo vijijini katika nchi za bara la Afrika.


Mtaalam Mshauri wa Kiufundi wa Shirika lisilo la la Kiserikali linalojihusisha na maendeleo vijijini lijulikanalo kama Mastercard Foundation for Rural Prosperity, Gabriel Kivuti (Pichani) akionesha jinsi Shirika hilo la Mastercard Linavyowasaidia watu hao wa vijijini. Picha na Raymond Urio

Baadhi ya Wadau wakimsikiliza Mtaalam, Mshauri wa Kiufundi wa Shirika hilo kwenye mkutano huo leo Maelezo jijini Dar es Salaam. Picha na Raymond Urio

 Akizungumza na waandishi wa habari Mshauri wa taasisi hiyo Gabriel Kivuti amesema kuwa kwakushirikiana na taasisi zakifedha zilizopo hapa nchini taasisi hiyo imeamua kutoa fedha ambazo sio za mkopo ilikuweza kumsaidia kiuchumi wakulima na wafanya biashara wadogodogo.
 
‘’Katika kipindi cha mwaka jana taasisi yetu imetoa zaidi ya dola zakimarekani milioni 35 ikiwa nalengo lakuwasaidia wakulima wadogo wawadogo mradi huu wa mfuko kwa ajili yamaendeleo vijijini unasimamiwa na Taasisi ya KPMG international Development advisor services Afrika ‘’Alisema Mshauri Gabriel KIVUTI .
Mshauri Kivuti alisema kuwa kumekuwepo na changamoto nyingi katika kaya nyingi zilizopo vijijini barani afrika kutoshirikishwa katika masuala yakifedha ambapo zaidi ya asilimia 70 kaya  masikini zilizokusini mwajangwa la sahara zimekuwa zikitegemea kilimo kama uti wa mgongo wauchumi .

 Mtaalama Mshauri wa Kiufundi wa Shirika lisilo la kiserikali linalojihusisha na maendeleo ya vijijini lijulikanalo kama MasterCard Foundation, for Rular Prosperity, Gabriel Kivuti akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo, kuhusiana na kuwatangaza washindi wa tuzo kwa makampuni matano yenye thamani ya Dola za Kimarekani 10 kwaajili ya kukuza uchumi wao. Picha na Raymond urio

Alisema wakulima wadogo wadogo wamekuwa wakikabiliwa nachangamoto ya baadhi ya taasisi za kifedha kuweza kuwafikia katika maeneo yao hali inayozorotesha jitihada za kukwamua sekta ya kilimo na wakulima wenyewe.
‘’Gharama kubwa zakufanya biashara ,ukosefu wa wafanyakazi wenye ujuzi namiundo mbinu yabiashara isiyo badilika inazorotesha jitihada za kupanua bidhaa sahihi ambazo zingeweza kuwasaidia kaya masikini’’Aliongeza KIVUTI.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni