MCHOKOZE FELLAIN UPATE PEPSI YAKO YA BURE KAMA HAYA YALIYOMKUTA HUTH WA LEICESTER...
Mechi
kati ya Manchester United dhidi ya Leicester City haikuwa mchezo, maana
wengine wanataka ubingwa na wengine wanataka kucheza Ligi ya Mabingwa
Ulaya.
Ndani
ya Old Trafford, mechi hiyo imeisha kwa sare ya bao 1-1, lakini mtiti
kati ya kiungo wa Man United, Marouane Fellaini dhidi ya beki wa kati wa
Leicester City, Robert Huth umebaki kuwa gumzo.
Huth alitaka kumchanganya Fellaini na mara nyingi alikuwa akimvuta nywele.
Juhudi
za Fellaini kuzuia shambulizi hilo la Huth kwa amani hazikuzaa matunda
hadi alipoamua kufanya ile kazi yake anayosifika nayo.
Kupiga kiwiko, maarufu kama Pepsi. Huth akakaa chini kusikilizia maumivu.
Wachambuzi
wanaeleza kwamba inawezekana Fellaini akaingia matatizoni na kufungiwa
mechi tatu kama ile ishu ya Delle Alli wa Spurs. Lakini Huth
aliyeanzisha vita kwa kuvuta nywele za mwenzake je?
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni