MAJALIWA:WANAVYUO WAFUATE TARATIBU NA SHERIA ZILIZOPO VYUONI KWAO

Hata hivyo imesema itaendelea
kuwahudumia Watanzania wote ikiwemo kutoa elimu kuanzia ngazi awali hadi
elimu ya juu bila kujali ya itikadi za dini wala vyama vyao vya siasa.
Waziri Mkuu,Kassm Majaliwa
ameyasema hayo leo (Alhamisi, Mei 5, 2016) wakati akijibu swali la papo
kwa papo la Mheshimiwa Ester Matiko (Viti maalum Chadema) aliyetaka
kujua kama Serikali imetoa maelekezo kwa uongozi wa vyuo vikuu
kunyanyasa wanafunzi wanaojihusisha na masuala ya siasa.
“Nakanusha si kweli kwamba kuna
maelekezo kwenye vyuo vyote vya elimu ya juu na pia hakuna unyanyasaji
wowote wa vyuo na Watanzania wote wanao uhuru wa kujiunga na vyama vyote
wanavyovitaka, lakini kila eneo limeweka utaratibu wake hivyo wafuate
taratibu na sheria katika sehemu husika,” alisema.
Katika hatua nyingine, Waziri
Mkuu amesema Serikali imeondoa tozo ya asilimia 15 ya eneo la manunuzi
ya vifungashio katika zao la korosho ili kumfanya mkulima kupata tija
zaidi.
Akijibu swali la papo kwa papo la
Mheshimiwa Katani Katani (Tandahimba-CUF) aliyetaka kujua ni lini tozo
hiyo itaondolewa, Waziri Mkuu Majaliwa amesema tayari tozo hiyo
imeshaondolewa na gharama hizo kwa sasa zipo katika mfuko wa wakfu
ulioundwa na wadau wa zao hilo na unachangiwa na asilimia 65 ya tozo za
korosho zinazouzwa nje.
Amesema mfuko huo wa wakfu
unatakiwa kusimamia upatikanaji wa masoko ya zao la korosho, kununua
pembejeo, kusimamia uboreshaji na upanuzi wa mashamba na kugharamia
tatifi mbalimbali kwa ajili ya kupata ubora wa zao hilo.
Akijibu kuhusu suala la madai ya
wakulima ambao korosho zao zimepotea ghallani, amesema mfumo wa uuzwaji
wa zao hilo wa stakabadhi ghalani ni wa kiushirika na unasimamiwa na
Mrajisi ni vema wakulima wakadai haki yao katika mikutano ya ushirika
wao na kama hawaridhiki na majibu waende mahakamani ili kupata haki yao.
Amesema kwa sasa Serikali
itahamishia nguvu zake katika kusimamia mazao mengine ya pamba, tumbaku
na kahawa kama walivyofanya kwenye zao la korosho ili wakulima wa mazao
hayo nao wapate tija.
Akijibu swali la Mheshimiwa
Joseph Kekunda (Sikonge-CCM) aliyetaka kujua Serikali inampango gani wa
kutatua migogoro ya wakulima na wakulima ,Waziri Mkuu amesema Serikali
imechukua hatua mbalimbali katika kuhakikisha inakomesha migogoro hiyo
ambazo ni pamoja na kupima maeneo na kuweka mipango bora ya matumizi ya
ardhi.
Pia kuweka mipaka katika maeneo
mapya na kutumia ranchi zilizopo kwa ajili ya wafugaji wakubwa na kwamba
itatenga maeneo ya kilimo na kuyabainisha kwa wananchi ili kuepuka
muingiliano uliopo hivi sasa.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni