MAJALIWA AKUTANA NA WAWEKEZAJI WA UMEME WA GESI TOKA JAPAN
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akipata ufafanuzi wa mikakati ya uwekezaji kwenye
miundombinu ya umeme wa gesi asilia na jua kutoka kwa Mtendaji Mkuu wa
Kampuni ya KOYO ya Japan, Bw. Norio Shoji wakati alipokutana na ujembe
wa kampuni hiyo ofisini kwake jijini Dar es salaam May 9, 2016. (Picha
na ofisi ya Waziri Mkuu)

Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akiagana na Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya KOYO ya
Japan, Bw. Norio Shoji baada ya kukutana na Mtendaji huyo na ujumbe
wake ofisini kwake jijini Dar es salaam May 9, 2016. Kampuni hiyo
ikishirikiana na Kampuni ya Kitanzania ya SSF Limited inakusudia
kuwekeza kwenye miundombinu ya umeme wa gesi asilia na jua nchini.
(Picha na ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa
Kampuni ya Japan ya KOYO na kampuni ya Kitanzania ya SSF Limited
ambazo kwa pamoja zimekusudia kushirikiana ili kuwekeza kwenye
miundombinu ya umeme wa gesi asilia na jua nchini. Waziri Mkuu alifanya
mazungumzo na viongozi hao ofisini kwake jijini Dar es salaam May 9,
2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni