MAADHIMISHO YA MIAKA SITA YA CHAMA CHA WATANZANIA WALIOSOMEA CHINA (CAAT)
By Newsroom on May 11, 2016
Chama cha Watanzania Waliosoma
China kwa kiingereza China Alumni Association of Tanzania (CAAT)
kinapenda kukukaribisha katika sherehe ya maadhimisho ya miaka 6
(2010-2016) tokea kilipozaliwa. Sherehe hiyo itafanyika katika ukumbi wa
Cardinal Laurian Rugambwa Social Centre pembezoni mwa kanisa la
Mtakatifu Peter (St Peter), Oysterbay Ijumaa ya tarehe 20-May-2016
kuanzia saa 8 alasiri.
Sherehe hiyo itahudhuriwa na
viongozi wakubwa kutoka serikalini na baadhi ya wageni kutoka ubalozi wa
China. Pamoja na burudani mbalimbali, maadhimisho hayo yatakuwa na
hotuba kutoka viongozi wa serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na
viongozi wa ubalozi wa Jamhuri ya watu wa China. Kwenye sherehe hiyo
pia utafanyika uzinduzi wa tovuti (website) ya CAAT.
Baada ya chakula cha pamoja cha
jioni, vilevile kutakuwa na fursa ya wafanyabiashara, wajasiliamali na
wafanyakazi waajiriwa kuonyesha bidhaa au matangazo ya bidhaa au huduma
wanazotoa. Dhima kuu ya tukio hilo ni;•Utambulisho wa jumuia ya CAAT
ambayo inajumuisha wataalam wa taaluma mbalimbali waliohitimu mafunzo
yao katika Jamhuri ya Watu wa China•Kubaini na Kuainisha fursa
zinazopatikana Tanzania na China kupitia CAAT•
Maonyesho ya bidhaa na huduma
mbalimbali za biashara za wanajumuia. Wote mliopata kusoma China
mnakaribishwa. Hakutakuwa na kiingilio. Unaweza kushiriki kwa
kuthibitisha uwepo wako kwa kupiga simu kwa Katibu Mtendaji wa CAAT kwa
kupitia 0783-992020 au 0715-200090 au email gsoreku@yahoo.com
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni