KIKAO CHA KAMATI YA NIDHAMU MEI 3, 2016
Kikao
cha Kamati ya Nidhamu ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)
kinafanyika kesho Jumanne Mei 3, 2016 kwenye ukumbi wa ofisi za
shirikisho zilizoko Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume, Ilala jijini Dar es
Salaam.
Kikao hicho cha kupitia mashauri
mbalimbali yaliyowasilishwa TFF, ilikuwa kifanyike Jumapili Mei Mosi,
lakini kiliahirishwa kwa sababu ya wajumbe wengi walikuwa na udhuru.
Wadau watakaojadiliwa kesho ni
pamoja na Kocha Mkuu wa Azam FC ya Dar es Salaam, Stewart Hall na
wachezaji wake wakiwamo John Bocco, Shomari Kapombe, Aishi Manula na
Kipre Tchetche.
Wengine ni nyota wa Young
Africans SC ya Dar es Salaam ambao ni Amissi Tambwe na Donald Ngoma
wakati kutoka timu ya JKT Rwakoma ya Mara wamo Paulo Jinga, Zephlyn
Laurian na Idrisa Mohamed.
Wengine ni Ismail Nkulo, Said
Juma, Idd Selaman na Edward Amos wa Polisi Dodoma, kadhalika Abel
Katunda wa Transit Camp ya Dar es Salaam na daktari wa Coastal Union ya
Tanga, Dk. Mganaga Kitambi.
Pia Herry ‘Mzozo’ Chibakasa wa
Friends Rangers ya Dar es Salaam naye atajadiliwa na Bunu Abdallah
ambaye ni Kocha Msaidizi wa JKT Oljoro ya Arusha.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni