JWTZ LAANDAA SEMINA ya Wakuu wa Kamanda wa majeshi ya Nchi kavu Afrika
JESHI LA ULINZI LA WANANCHI WA TANZANIA
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa
Tanzania (JWTZ) linapenda kutoa taarifa kuwa kutakuwa na Semina ya wiki
moja ya Wakuu wa Kamandi wa majeshi ya Nchi kavu Afrika itakayoendeshwa
Mkoani Arusha katika Hoteli ya Mount Meru kuanzia tarehe 13 hadi 19, Mei
2016.
Lengo la Semina hiyo ni
kuwakutanisha Wakuu wa kamandi hizo Afrika ili kujadili na kuendeleza
ushirikiano katika kutafuta ufumbuzi wa matatizo mbalimbali
yanayolikabili bara la Afrika katika Nyanja ya ulinzi.
Kauli Mbiu ya Semina hiyo ni Ujenzi wa Usalama Afrika kupitia Ushirikiano.
Semina hii hufanyika kila mwaka
katika mojawapo ya nchi za Afrika, ili kuwajengea makamanda hao
ushirikiano katika kutatua changamoto mbalimbali za kiulinzi
zinazotokana na mabadiliko katika Nyanja za kiusalama.
Imetolewa na Kurugenzi ya Habari na Mahusiano
Makao Makuu ya Jeshi, Upanga
S.L.P 9203, Dar es Salaam, Tanzania.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni