Jumapili, 8 Mei 2016

JAMES MBATIA NA JOSEPH SELASINI WATEMBELEA WAHANGA WA MAAFA YALIYOTOKANA NA MVUA ROMBO.

Wabunge James Mbatia (Jimbo la Vunjo ) na Joseph Selasini wakiwa ofisini kwa
Mkuu wa wilaya ya Rombo Lembris Kipuyo wakimsikiliza Mkurugenzi wa Idara
ya Maafa nchini Brigedia Jenerali Mbazi Msuya alipofika kutembelea
wahanga wa mvua zilizonyesha hivi karibuni na kusababisha maafa.
Mbunge wa Jimbo la Rombo Joseph Selasini (kulia) akijaribu kutoa maelezo namna
ambavyo wakazi wa kijiji cha Manda juu wilyani humo walivyo pata maafa
yaliyotokana na kunyesha kwa mvua kubwa Aprili 24 na 25 mwaka huu.
Mbunge wa Jimbo la Vunjo ,James Mbatia akitoa pole kwa wakazi wa kijiji cha
Manda juu wilayani alipokua akielekea kujionea namna ambavyo baadhi ya
familia zilivyo athirika na mvua katika kjiji hicho na mtoto mmoja
kupoteza maisha baada ya kifusi kuporomoka na kuangusha nyumba
aliyokuwemo.
Mbunge wa Jimbo la Rombo ,Joseph Selasini (kushoto) akiongozana na Mkuu wa
wilaya ya Rombo ,Lembris Kupuyo wakielekea kuijionea athari ya mvua hizo.
Mbunge Mbatia akizungumza jambo mara baada ya kufika katika eneo lililokuwa na
nyumba iliyobomoka baada ya kuporomokewa na kifusi na kusababisha kifo
cha mtoto mmoja katika kijiji cha Manda juu wilayani Rombo.
Continue reading →

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni