
Jumatatu, 28 Septemba 2015
MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AONGOZA WANANCHI KUAGA MWILI WA MAREHEMU CELINA KOMBANI, DAR, KUZIKWA KESHO MOROGORO.

Ijumaa, 11 Septemba 2015
UZINDUZI WA MFULULIZO WA VIPINDI VYA MAMA MISITU KUHUSU UZALISHAJI WA MKAA ENDELEVU WAFANYIKA NEW AFRIKA HOTEL LEO JIJINI DAR ES SALAAM
Viongozi mbalimbali wakiwa meza kuu, kutoka kushoto Mkurugenzi wa Taasisi ya Natural Resource Forum (TNRF),
Joseph Olila, Mkurugenzi, Idara ya Misitu na Nyuki wa Wizara ya
Maliasili na Utalii, Gladness Makamba, ambaye alikuwa mgeni rasmi wa
uzinduzi huo, Msaidizi wa Balozi, Ubalozi wa UFINI ambao ni wafadhili wa
mama misitu, Simo-Pekka Parviainen na Ofisa Mradi Ubalozi wa Finland,
William Nambiza.
Jumanne, 8 Septemba 2015
MAKAMO WA RAISI DKT.BILALI ATOA TUZO KWA WAGANGA WASTAAFU.
DKT.AFUNGUA WA MWAKA WA WAGANGA WAKUU DAR
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akihutubia wakati akifungua rasmi Mkutano wa mwaka wa Waganga Wakuu wa Mikoa, Halmashauri na Wakurugenzi wa Hospitali za Rufaa, ulioanza leo Sept 8, 2015 na Maadhimisho ya Miaka 40 ya Mpango wa Taifa wa Chanjo uliofanyika kwenye Hoteli ya Blue Peal Ubungo Plaza jijini Dar es Salaam.
TAKWIMU WATANGAZA MFUMUKO WA BEI MWEZI AGOSTI
Mkurugenzi wa Sensa na Takwimu za Jamii Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS), Iphrahim Kwesigabo (kushoto), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam leo mchana kuhusu mfumuko wa bei wa Taifa kwa mwezi Agosti, 2015. Kulia ni Kaimu Meneja wa Idara ya Takwimu za Ajira na Bei, Ruth Minja.
Alhamisi, 3 Septemba 2015

mgombea wa ubunge jimbo la Ubungo kupitia tiketi ya chama cha Mapinduzi(CCM) Dkt Didas Masaburi amewataka Wapinzani wasiweweseke katika kutafuta mtu anayewaloga kwa kuwa mchawi anatoka ndani ya chama chao kwa tabia zao za kukumbatia makapi ambazo haziendani na matakwa ya wananchi.
Dkt Masaburi amemesema hayo leo jijini Dar es Salaam wakati akizungumza na Waandishi wa habari kwenye ofisi za jimbo hilo zilizopo kata ya Manzese akikanusha kuhusika kuchochea yaliyofanyika juzi na baadhi ya vijana na kudhibitiwa na polisi.
"Haipo kwenye akili yangu na wala haitakuwepo kuwachochea vijana waandamane ingawa maandamano ya amani sioni kosa lake na kama maandamano yanaashiria kuunga mkono jambo na kama maandamano yale hayaendani na kudhuru wananchi na kuharibu mali zao,"alisema Makaburi.
Amesema kuwa anaunga mkono hoja za Dkt Slaa na kama angekuwa Chadema angeandamana kwa kuwa hoja hizo zilikuwa ni za kweli na atamkaribisha Mbowe na kumpongeza pamoja na wote watakaokuwa tayari kuhamia kwenye chama chao.
Amesema kuwa aliwapokea vijana waliochoshwa na vitendo viovu vinavyofanywa na viongozi wanaounda Umoja wa UKAWA kwa kuwalazimisha kujiunga na umoja huo na kuwa wao wanataka kukiona chama chao(Chadema).
Mgombea huyo anaendelea kufafanua kuwa vijana hao walipelekwa na mgombea Udiwani wa Ubungo kupitia Chadema na ndiye aliyewaongoza kufanya maandamano baada ya kukatwa katika kura za maoni na kuomba kujiunga na CCM.
"Huyu mgonbea mara tu baada ya kura za maoni za Chadema alikuja kwangu na kusema yupo tayari kujiunga na kuwa walimfanyia njama hivyo nimpokee na ataleta wafuasi wengi wa Chadema ili chama kishinde na amejiandaa vyema ambapo baadaye alitoka na kuanza kusema maneno,"alisema Masaburi.
Wakati huohuo wanachama 13 kutoka CUF na Chadema wamehamia rasmi kwenye Chama cha Mapinduzi(CCM).
Naye Halima Said ambaye ni mgombea wa Ujumbe viti maalum(Chadema)alisema kuwa ameamua kuhamia (CCM)kutokana na wamekuwa wakipotoshwa na na kuwa kiongozi ambaye pia ni mlezi wa chama hicho hayupo.
Ijumaa, 14 Agosti 2015
JWTZ YAWAPA ONYO KALI WANASIASA
JESHI la Wananchi Tanzania (JWTZ), limekanusha kuwanyang'anya kadi za kupigia kura maofisa na askari wake kama ilivyodaiwa na mmoja wa viongozi wa chama kimoja cha siasa na kutolewa katika vyombo vya habari na mitandao ya kijamii
Amezungumza hayo jana Jijini Dar es Salaam wakati alipokutana na waandishi habari Mkurugenzi wa Habari na Uhusiano wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ), Kanali Ngemela Lubinga alisema madai hayo siyo ya kweli na kuwa jeshi hilo halijafanya hivyo na wala haliwezi kufanya hivyo.
“Wanajeshi hawaruhusiwi kuwa wanachama wa chama chochote cha kisiasa na kuwa mwanajeshi haruhusiwi kuwa shabiki wa chama chochote cha kisiasa”alisema Lubinga.
Lubinga alisema Jeshi la Wananchi Tanzania linafanya kazi zake kama 'professional state organ duniani na kuwa mwanajeshi anayekiuka huchukuliwa hatua za kinidhamu za kijeshi wala si za kiraia.
Alisema Jeshi la Wananchi Tanzania limesikitishwa na kauli hiyo iliyotolewa na kiongozi
huyo na amewatakaWananchi na viongozi wa kisiasa wafanye kazi zao za kisiasa na zisianzishwe hoja nje ya maeneo hayo ya kisiasa kwani lugha hizo za upotoshaji zinaweza kuleta hofu, ukakasi na wasiwasi kwa Wananchi.
Aliongeza kuwa jeshi hilo linaendelea na shughuli zake kama kawaida halipendi litolewe kauli za upotoshaji, kusikoeleweka ufuatwe utaratibu wa kuuliza kupata majibu ya uhakika kwani Wananchi wanaimani na jeshi lao.
Mkurugenzi
wa Habari na Uhusiano wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ),
NAPE:WANAOIKIMBIA CCM NI OIL CHAFU
Na Tinah Reuben
KATIBU mwenezi na itikadi wa CCM Nape Nnauye amekanusha habari zilizozagaa katika mitandao ya kijamii kuwa mgombea wao wa uraisi John Pombe Magufuli amehaidi kuwapatia kompyuta mpakato kila mwalimu pamoja na kila kijiji kupatiwa milioni 50.
Nape amezungumza hayo leo Jijini Dar es salaam alipokuta na Waandishi wa Habari alipokuwa anatoa taarifa hiyo iliyokanusha na kusema kuwa waliotoa taarifa hiyo wanalengo lakuwachafua na kutaka waonekana wameanza kampeni mapema.
Alisema hakuna sehemu ambayo Magufuli aliwahi kuongea kauli hiyo na anawashangaa watu pamoja na mitandao ya kijamii inayoeneza ujumbe huo ambao sio wa kweli hata kidogo.
Aliongeza kuwa wapo watu wasioitakia mema CCM na kwamba wamebaini mbinu hizo chafu na wanazifanyia kazi.
"Watu walianda waraka ule walidai kuona umeandikwa katika ilani ya CCM kitu ambacho sio kweli kwani Ilani imetoka rasmi jana",alisema Nape.
Akitolea ufanunuzi kuhusu kuhama kwa Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Shinyanga Hamis Mgeja,Nape alisema kuwa Mgeja alijitoa baada ya mwanaye wa Kike kushindwa katika mchakato wa Viti maalum mkoa wa Shinyanga.
Alisema kuwa baada ya mwanae kushindwa Mgeja alitaka chama kimbebe mwanae kinyume cha misingi ya chama na alipokataliwa alikasirikia na kutangaza uamuzi wake wa kukihama cham.
"Watu walikimbia CCM wamekimbia kwa mabaya yao pia walionzisha vyama upinzani wote misingi yao ni CCM na kama wanaondoka atushangai.....kwanza walioaznisha hivyo vyama hawajafanikiwa na wanaokwenda hawata fanikiwa,"alisema Nape
Aliongeza kuwa kitendo cha wanachama hao kujiondoa CCM nisawa na fundi anayetoa Dizeli chafu ndani ya injini ya Gari na kuwepa safi.
Alisema kuwa anawashangaa wapinzani wanavyopokea dizeli chafu zinazopelekea injini zao kuwa mbovu na zosizofa kabisa.
Aidha alisema kwa kawadia chama kinautaratibu wa kupokea wanachama wapya hivyo ni kitendo cha kushangaza kuona wapinzani wanapokea wanachama walioshindwa katika vyama vyao.
Jisajili kwenye:
Machapisho (Atom)


