Alhamisi, 3 Septemba 2015



mgombea wa ubunge jimbo la Ubungo kupitia tiketi ya chama cha Mapinduzi(CCM) Dkt Didas Masaburi amewataka Wapinzani wasiweweseke katika kutafuta mtu anayewaloga kwa kuwa mchawi anatoka ndani ya chama chao kwa tabia zao za kukumbatia makapi ambazo haziendani na matakwa ya wananchi.

Dkt Masaburi amemesema hayo leo jijini Dar es Salaam wakati akizungumza na Waandishi wa habari kwenye ofisi za jimbo hilo zilizopo kata ya Manzese akikanusha kuhusika kuchochea yaliyofanyika juzi na baadhi ya vijana na kudhibitiwa na polisi.

"Haipo kwenye akili yangu na wala haitakuwepo kuwachochea vijana waandamane ingawa maandamano ya amani sioni kosa lake na kama maandamano yanaashiria kuunga mkono jambo na kama maandamano yale hayaendani na kudhuru wananchi na kuharibu mali zao,"alisema Makaburi.

Amesema kuwa anaunga mkono hoja za Dkt Slaa na kama angekuwa Chadema angeandamana kwa kuwa hoja hizo zilikuwa ni za kweli na atamkaribisha Mbowe na kumpongeza pamoja na wote watakaokuwa  tayari kuhamia kwenye chama chao. 

Amesema kuwa aliwapokea vijana waliochoshwa na vitendo viovu vinavyofanywa na viongozi wanaounda Umoja wa UKAWA kwa kuwalazimisha kujiunga na umoja huo na kuwa wao wanataka kukiona chama chao(Chadema). 

Mgombea huyo anaendelea kufafanua kuwa vijana hao walipelekwa na mgombea Udiwani wa Ubungo kupitia Chadema na ndiye aliyewaongoza kufanya maandamano baada ya kukatwa katika kura za maoni na kuomba kujiunga na CCM.

"Huyu mgonbea mara tu baada ya kura za maoni za Chadema alikuja kwangu na kusema yupo tayari kujiunga na kuwa  walimfanyia njama hivyo nimpokee na ataleta wafuasi wengi wa Chadema ili chama kishinde na amejiandaa vyema ambapo baadaye alitoka na kuanza kusema maneno,"alisema Masaburi.

Wakati huohuo wanachama 13 kutoka CUF na Chadema wamehamia rasmi kwenye Chama cha Mapinduzi(CCM).

Naye Halima Said  ambaye ni mgombea wa  Ujumbe viti maalum(Chadema)alisema kuwa ameamua kuhamia (CCM)kutokana na wamekuwa wakipotoshwa na na kuwa kiongozi ambaye pia ni mlezi wa chama hicho hayupo.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni