MBUNGE WA KIBAHA VIJIJINI AKABIDHI MADAWATI 537 NA VITABU KWA UONGOZI WA HALMASHAURI


………………………………………………………………………………………..
NA VICTOR MASANGU, KIBAHA
WANAFUNZI wa shule za msingi na
sekondari katika halmashauri ya Kibaha Vijijini Mkoa wa Pwani
waliokuwa wanakabiliwa na chanagamoto ya uhaba wa madawati na viti na
kusababisha baadhi yao kuwa tabia ya utoro kwa sasa wameanza kunufaika
na agizo la Rais Dr.John Magufuli la kutaka wanafunzi wote nchini
kuhakikisha wanasoma wakiwa wamekaa kwenye madawati.
Agizo hilo la Rais
limetekelezwa na Mbunge wa Jimbo la Kibaha Vijijini Hamoud Jumaa
kupitia kupitia fedha ambazo zimepatikana kutokana na kubana matumizi
yasiyo ya lazima katika ofisi yake kwa lengo la kuweza kusaidia katika
kuboresha sekta ya elimu.
Akikabidhi jumla ya madawati
537 Mbunge wa Jimbo hilo kwa uongozi wa halmashauri ya kibaha vijijini
katika halfa fupi zilizofanyika katika shule ya sekondari kilangalanga
iliyopo Mlandizi, amesema kwamba ametoa madawati hao pamoja na vitabu
kwa lengo la kuweza kupunguza kero na kuondokana na adha ambayo
walikuwa wanaipata wanafunzi wa jimbo lake katika siku za nyuma.
Kwa upande wake Afisa elimu
katika halmashauri ya kibaha vijijini Coskansia Mafuru amebainisha
kwamba awali kabla ya agizo la Rais walikuwa wana upungufu wa madawati
1923 kwa shule za msingi, hivyo msaada huo utaweza kumaliza changamoto
zilizokuwa zikiwakabili na kuongeza kiwango cha ufaulu kwa wanafunzi.
Alisema kwamba kukamilisha
agizo ambalo limetolewa na rais litaweza kuwa ni mkombozi mkubwa sana
kwa wanafunzi na wataweza kuongeza kasi ya ufaulu kwani hapo awali
walikuwa wanasoma katika mazingira ambayo sio rafiki kwao na wengine
kusoma wakiwa wamekaa chini.
“Katika kukamilisha zoezi hili
na agizo lililotolewa na Rais kuhakikisha kwamba tunafanya kila jitihada
ili kuweza kuhakikisha wote wanasoma wakiwa wamekaa kwenye madawati na
sio chini hivyo madawati hayo yametokana na kubana matumizi mbali mbali
katika ofisi ya Mbunge hivyo nina imani ni moja ya hatua nzuri katika
kuendelea kuboresha sekta ya elimu katika jimbo langu,”alisema Jumaa.
Pia alisema kwamba pamoja na
agioz hilo pia ataendelea kujitahidi kushirikiana na wa madiwani wote
katika halmashauri ya Kibaha vijiji pamoja na wadau wengine ili kuweza
kuendeleza kutoa sapoti katika kununua mahitaji mengine muhimu ikiwemo
vitabu ambavyo viyaweza kuwapa fursa wanafunzi kuweza kujisomea.
Naye Mkuu wa shule ya sekondari
Kilangalanga Albert Mabiki, pamoja na Mwenyekiti wa halmashauri ya
Kibaha vijijini Mansouri Kisebengo hapa wanazungumza changamoto
zilizokuwa zinawakabili wanafunzi pamoja na kushindwa kufanya vizuri
kutokana na kuwepo kwa mlundikano mkubwa wa wanafunzi pamoja na hali ya
kuwepo kwa utoro.
“Ni kweli changamoto ya watoto
wetu walikuwa wanasoma katika mazingira ya mlundikano, na wakati
mwingine baadhi ya wanafunzi wanakuwa ni watoro hawafiki shuleni nah ii
ni kutokana na kutokuwepo kwa madawati na viti vya kutosha lakini kwa
hali hii na agizo la Rais wetu hakika kwa sasa hata huu utoro
utamalizika katika baadhi ya maeneo.
MADAWATI hayo pamoja na vitabu
ambayo vimetolewa na ofisi ya Mbunge wa jimbo la Kibaha vijijini
vimegharimu kiasi cha zaidi ya shilingi milioni 100 ambapo kata zote
14 ambapo kuna shule za msingi na sekondari zimeweza kupatiwa mgao huo
kwa baadhi ya shulezenye mahitaji makubwa kwa ajili ya kuweza
kutekeleza agizo lililotolewa na Rais.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni