Serikali yapokea msaada wa madawati 300 toka Ubalozi wa Kuwait nchini Tanzania.
Balozi
wa Kuwait nchini Tanzania Mhe. Jaseem Al Najem akiongea na waandishi wa
habari (hawapo pichani) wakati alipokuwa akikabdhi msaada wa madawati
kwa Waziri wa Mambo ya Njena Ushirikiano wa Afrika Mashariki,
Kikanda na Kimataifa, Balozi Augustine Maiga (hayupo pichani) mapema hii
leo jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Mambo ya Njena
Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Balozi Augustine
Maiga akitoa neno la shukrani kwa Balozi wa Kuwait nchini Tanzania Mhe.
Jaseem Al Najem wakati akipokea msaada wa madawati toka kwa balozi huyo
mapema hii leo jijini Dar es Salaam.
Balozi wa Kuwait nchini Tanzania Mhe. Jaseem Al Najem (katikati) akikabidhi msaada wa madawati kwa Waziri wa Mambo ya Njena
Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Balozi Augustine
Maiga, kushoto ni Mkurugenzi Idara ya Mashariki ya Kati Balozi Abdallah
Kilima mapemahii leo jijini Dar es Salaam.
Balozi wa Kuwait nchini Tanzania Mhe. Jaseem Al Najem (katikati) pamoja na Waziri wa Mambo ya Njena
Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Balozi Augustine
Maiga (kulia) wakiwa wamekalia madawati ambayo yametolewa msaada kwa
serikali ya Tanzania, kushoto ni Mkurugenzi Idara ya Mashariki ya Kati
Balozi Abdallah Kilima mapema hii leo jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Mambo ya Njena
Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Balozi Augustine
Maiga (Katikati aliyekaa) kushoto ni Balozi wa Kuwait nchini Tanzania
Mhe. Jaseem Al Najem na kulia ni Mkurugenzi Idara ya Mashariki ya Kati
Balozi Abdallah Kilima wakiwa katika picha ya pamoja na Mabalozi na
Wakurugenzi toka wizara hiyo mara baada ya kupokea msaada wa madawati
toka ubalozi wa Kuwait nchini Tanzania mapema hii leo jijini Dar es
Salaam.
Picha zote na Eliphace Marwa – Maelezo
———————————————————————–
Na Eliphace Marwa- Maelezo
Serikali
ya Tanzania imepokea msaada wa madawati 300 toka Ubalozi wa Kuwait
nchini Tanzania ikiwa ni sehemu ya kutatua tatizo la uhaba wa madawati
katika shule za msingi hapa nchini.
Akizungumza wakati wa makabidhiano hayo Waziri wa Mambo ya Njena
Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Balozi Augustine
Maiga kwa niaba ya serikali alisema kuwa amesema kuwa kupokea madawati
hayo ni sehemu ya kutekeleza wito wa Waziri Mkuu Kassim Majaliwa.
“Waziri
Mkuu alitutaka sisi katika nafasi zetu tuwashirikishe wadau mbalimbali
ili kuweza kutekeleza adhma ya serikali ya kutatua tatizo la wanafunzi
kukaa chini ili waweze kupata mazingira bora ya kupata elimu, alisema
Balozi Maige.
Balozi
Maigaaliongeza kuwa Kuwait iko tayari kuisaidia nchi ya Tanzania kwa
kuwajengea uwezo wataalam toka Tanzania kwa kuwapa elimu ya mafuta na
gesi kwani Kuwait ina uzoefu mkubwa katika sekta ya mafuta na gesi.
Naye
Balozi wa Kuwait nchini Tanzania Mhe. Jaseem Al Najem alisema kuwa
Serikali ya Kuwait itaendelea kutoa misaada kwa serikali ya Tanzania
kadri itakavyowezekana pindi pale itakapohitajika.
Aidha
Balozi Maiga alitumia muda huo kutoa taarifa kwa waandishi wa habari
kuhusu ujio wa Rais wa Rwanda Paul Kagame hapa nchini siku ya Julai
Mosi ikiwa ni sehemu ya ziara yake ya kikazi.
“Rais
wa Rwanda atawasili hapa nchini Julai Mosi na ataweka saini makubaliano
mbalimbali waliyofikia kati ya Tanzania na Rwanda baada ya hapo Rais
Kagame ataambatana na mwenyeji wake Rais Magufuli mpaka katika viwanja
vya maonesho vya Sabasaba ambapo Rais Kagame atayazindua rasmi maonesho
hayo ya arobaini”, alisema Balozi Maiga.
Aidha
Balozi Maiga aliongeza kuwa Rais Kagame jioni atakaribishwa Ikulu na
mwenyeji wake Rais Magufuli kwa ajili ya dhifa ya kitaifa.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni