Jumatano, 1 Juni 2016

Dk Mahiga asikitishwa na watanzania wanaofungwa nje kwa kosa la madawa y...


Serikali imesema watanzania 408 wanatumikia vifungo nje ya nchi na
wengine kukabiliwa na adhabu ya kifo baada ya kusafirisha dawa za
kulevya.

eca86bd9dddf141e387d29


Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na
Kimataifa, Augustine Mahiga alipokuwa akiwasilisha makadirio ya bajeti
ya wizara yake kwa mwaka wa fedha 2016/17.



Akizungumzia Watanzania waliokamatwa kwa dawa hizo Mahiga amesema
wanakabiliwa na adhabu hizo katika magereza mbalimbali duniani baada ya
kukutwa na hatia ya makosa ya kujihusisha na biashara haramu.



Mahinga alitaja idadi yao na nchi ambazo wanashikiliwa kuwa ni Brazil
(41), China (266), Iran (68), India (9), Nepal (4), Oman (3), Thailand
(14) na Umoja wa Falme za Kiarabu (3).





Hakuna maoni:

Chapisha Maoni