Mashindano ya Chess kuanza 23 April Mwaka huu.

Katibu wa Chama cha Mchezo wa
Chess Tanzania (TCA) Bw. Nurdin Hassuji ambaye pia ni Bingwa wa Taifa wa
mchezo huo akiongea na waandishi wa Habari hawapo pichani kuhusu
mashindano ya mtu mmoja mmoja ya ukanda wa Afrika 4.2 yajulikanayo kama
(2016 Africa Zone 4.2 Individual Chess Championship), kulia ni
Mwenyekiti wa Chama hicho Bw. Geofrey Mwanyika.

Akizungumza hayo mbele ya
waandishi wa habari Mwenyekiti wa chama cha mchezo huo nchini (TCA) Bw.
Geofrey Mwanyika amesema kuwa michuano hiyo iyafanyika katika Hoteli ya
Peacock jijini Dar es salaam Tanzania ikiwa mwenyeji wa mashindano hayo.
Aidha Bw. Mwanyika ameinisha nchi
ambazo zimeleta washiriki wake ni Uganda, Kenya, Rwanda, Burundi,
Djibout, Eritrea,Somalia,Ethiopia, Sudan Kusini na wenyeji Tanzania
“Jumla ya washiriki 32
watachuana katika mashindano hayo ambayo yamegawanyika katika makundi
mawili ya Wanaume na Wanawake na kati ya nchi hizo ambazo zinashiriki
Sudan na Seychells hazijathibitisha kushiriki”. Aliongeza Bw. Mwanyika.
Kwa upande wa Katibu wa TCA Bw.
Nurdin Hassuji ambaye pia ni Bingwa wa Taifa wa mchezo huo amesema kuwa
zawadi za washindi ni Dola 4500 za Kimarekani ambazo zitagawanywa kwa
watakaoshinda.
Aidha Bw. Hassuji amewataka wadau
wa Michezo na waandishi wa habari kujitokeza siku hiyo ili kuipa
sapoti timu yao na kuutangaza mchezo ujulikane na kupendwa zaidi nchini.
Mbali na hayo Bw. Hassuji
amesema kuwa mchezo huo wameupa kipaumbele na kwenda kuufundisha
mashuleni kwa sababu inawasaidia wanafunzi kuweza kufikiri kwa haraka
zaidi na kufanya mwanafunzi awe mwepesi kwenye kupambanua mambo.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni