Jumatatu, 28 Novemba 2016

WAZIRI MWIGULU AFANYA MZUNGUMZO NA BALOZI WA UINGEREZA NCHINI


mx1
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba akizungumza na Balozi wa Uingereza nchini, Sara Cooke (kulia)  masuala mbalimbali ya ushirikiano kati ya Uingereza na Tanzania. Mazungumzo hayo yalifanyika katika ofisi ya Waziri Mwigulu, jijini Dar es Salaam leo.  Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
mx2
Balozi wa Uingereza nchini, Sara Cooke (wapili kulia) akimfafanulia jambo Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba (katikati), kuhusiana na masuala mbalimbali ya ushirikiano kati ya nchi yake na Tanzania. Mazungumzo hayo yalifanyika katika ofisi ya Waziri Mwigulu, jijini Dar es Salaam leo. Kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Meja Jenerali Projest Rwegasira, na kulia ni Naibu Balozi wa nchi hiyo, Matt Sutherland.  Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
mx3
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba (kushoto) akimshukuru Balozi wa Uingereza nchini, Sara Cooke, mara baada ya kumaliza mazungumzo yao yaliyofanyika ofisini kwa Waziri Mwigulu, jijini Dar es Salaam leo. Balozi huyo alimtembelea Waziri huyo kwa lengo ya kujadiliana masuala mbalimbali ya ushirikiano kati ya Tanzania na Uingereza. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
mx4
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba (kushoto) akiagana na Balozi wa Uingereza nchini, Sara Cooke nje ya jengo la Wizara hiyo, mara baada ya kumaliza mazungumzo yao yaliyofanyika ofisini kwa Waziri Mwigulu, jijini Dar es Salaam leo. Balozi huyo alimtembelea Waziri huyo kwa lengo ya kujadiliana masuala mbalimbali ya ushirikiano kati ya Tanzania na Uingereza. Kulia ni Naibu Balozi wa nchi hiyo, Matt Sutherland. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
………………………………………………………………….
Na Felix Mwagara, MOHA.
WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba amefanya mazungumzo na Balozi wa Uingereza nchini, Sara Cooke na kumuakikishia ushirikiano zaidi kati ya Wizara yake na Ubalozi huo nchini.
Mazungumzo hayo ya zaidi ya saa moja yalifanyika ofisini kwa Waziri Mwigulu, jijini Dar es Salaam leo ambayo yalijadili masuala mbalimbali ikiwemo uimarishaji wa ushirikiano kati ya Wizara na ofisi ya Balozi huyo nchini.
Waziri Mwigulu alimuakikishia Balozi huyo kuwa Tanzania itaendelea kuwa salama kwa kuwa Wizara yake imejipanga vizuri kuendelea kuwalinda raia na mali zao pamoja na wageni wote waishio nchini.
“Mheshimiwa Balozi nashukuru sana kwa kunitembelea, najisikia furaha kwa ujio wako na karibu sana wakati wowote, Wizara yangu pamoja na nchi yangu kwa ujumla tutaendelea kushirikiana nanyi katika masuala mbalimbali,” alisema Mwigulu.
Hata hivyo, Balozi Sara alimshukuru Waziri Mwigulu kwa mazungumzo waliyoyafanya na kumuhakikishia ushirikiano zaidi kati ya Uingereza na Tanzania.
Pia kikao hicho kiliudhuriwa na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Meja Jenerali Projest Rwegasira pamoja na Naibu Balozi wa nchi hiyo, Matt Sutherland.

WAZIRI MKUU MH. KASSIM MAJALIWA AKUTANA NA MKURUGENZI MKUU WA SHIRIKA LA NYUMBA (NHC)


Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Mkurugenzi Mtendaji  wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), Nehemia Mchechu kwenye chumba cha watu mashuhuri cha uwanja wa ndege wa Julius Kambarage Nyerere jijini  Dr es salaam Novemba 28, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
mchec2
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Nyumba la Taifa, Nehemia Mchechu kwenye uwanja wa ndge wa Julius Kambarage Nyerere jijini Dar es salaam Novemba 28, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Wanafunzi wawili wa Shule ya Academic International washinda mitihani ya Cambridge

Wanafunzi wa shule ya Academic International school, Harshvardhan Kabla (kushoto) ambaye ameshika nafasi ya kwanza duniani katika somo la Kompyuta kwa wanafunzi wa “A Level” kwa mitihani ya Cambridge na Abishek Sankaranarayanan(kulia) ambaye ameshinda nafasi ya kwanza kwa somo la hisabati kwa mitihani ya Cambridge kwa wanafunzi wa kidato cha nne wakiwa katika picha ya pamoja katika sherehe maalum ya kuwapongeza.
Mkurugenzi wa Kituo cha Utamaduni wa India, Inder Jit Sagar akimkabidhi cheti na kombe mwanafunzi wa Shule ya Academic International, Harshvardhan Kabla (kulia) kwa kushinda nafasi ya kwanza duniani katika somo la Kompyuta kwa wanafunzi wa “A Level” kwa shule zinazofuata mtahala wa Cambridge.
Mkurugenzi wa Kituo cha Utamaduni wa India, Inder Jit Sagar akimkabidhi cheti na kombe mwanafunzi wa Shule ya Academic International, Abishek Sankaranarayanan(kulia) kwa kushinda nafasi ya kwanza duniani katika somo la Hisabati kwa wanafunzi wa “O Level” kwa shule zinazofuata mtahala wa Cambridge.
Mkurugenzi wa Kituo cha Utamaduni wa India, Inder Jit Sagar (kulia) akiwa katika picha ya pamoja na walimu wawili wa shule ya Academic International, Walter Mlowe ambaye anafundisha somo la Hisabati na Thadei Mwinuka ambaye anafundisha somo la kompyuta. Walimu hao walitunukiwa vyeti kwa kazi nzuri ya ufundishaji.
Mkurugenzi wa shule ya Academic International, Yusuf Kalindaga akizungumza katika hafla maalum ya kuwapongeza wanafunzi , walimu na wafanyakazi wa shule hiyo kwa kufanya vyema katika mitihani ya Cambridge.
Mkuu wa shule ya ya Academic International, Shyama Santhosh ( wa kwanza  kushoto) akisema jambo katika sherehe hiyo ya kuwapongeza wanafunzi hao  na walimu.
 

Baadhi ya wanafunzi wa shule ya Academic International wakishiriki katika hafla hiyo.
Baadhi ya wazazi na wanafunzi wa shule ya Academic International wakiwa katika hafla hiyo 
 
 
Wanafunzi wawili wa shule ya Academic International ya Tanzania wameweka historia katika mitihani ya mtahala wa Cambridge baada ya kushinda nafasi ya kwanza duniani katika masomo ya hisabati na kompyuta.
 
Wanafunzi hao ni Harshvardhan Babla aliyekuwa wa kwanza katika mtihani wa somo la kompyuta kwa wanafunzi wa kidato cha tano Abishek Sankaranarayanan aliyeshinda nafasi ya kwanza katika mtihani wa hisabati kwa wanafunzi wa kidato cha nne.
 
Wanafunzi hao walikabidhiwa vikombe na vyeti na mgeni rasmi, Mkurugenzi wa Kituo cha Utamaduni wa India, Inder Jit Sagar. Pia walimu wa masomo hayo, Thadei Mwinuka ambaye anafundisha somo la kompyuta na Walter Mlowe wa somo la hisabati nao walikabidhiwa vyeti vya pongezi kwa kufanya vizuri.
 
Akizungumza katika halfa maalum ya kuwapongeza wanafunzi hao na walimu wa masomo hayo, Mkuu wa shule hiyo, Shyama Santhosh alisema kuwa wamefarijika na ushindi huo ambao umeiletea sifa shule, walimu nan chi kwa ujumla.
 
“Huu ni ushindi mkubwa kwa shule, walimu nan chi kwa ujumla, mtihani wa Cambridge unafanywa na maelfu ya shule duniani na shule yetu imeibuka katika nafasi ya kwanza kwa masomo hayo mawili, ni jambo la kujivunia sana, hii inaonyesha kuwa walimu wetu wapo makini katika kufundisha,” alisema Santhosh.
 
Mkurugenzi wa shule hiyo, Yusuf Kalindaga amesema kuwa wanajivunia kwa matokeo hao mazuri ambayo yamewafanya kuwa shule pekee Tanzania kushika nafasi hizo za kwanza.
 
“Nimefarijika na kuvutiwa sana na matokeo ya wanafunzi hawa wawili, walimu wetu, Mwinuka ambaye anafundisha somo la kompyuta na Mlowe wa somo la hisabati kwa kufanya kazi kubwa kuhakikisha kuwa wanafunzi wanaowafundisha wanashika mafundisho yao na shule kwa sasa inafarijika kwa matokeo mazuri.
 
Akizungumza katika hafla hiyo Harshvardhan Babla aliyekuwa wa kwanza katika mtihani wa somo la kompyuta aliwapongeza walimu na viongozi wengine wa shule hiyo kwa mafundisho mazuri na kushika nafasi ya kwanza Duniani.
 
Babla alisema kuwa haikuwa kazi rahisi kwa mitihani ilikuwa migumu sana, lakini alizingatia mafunzo na kujibu vizuri maswali na kuibuka katika nafasi ya kwanza. Abishek Sankaranarayanan aliyeshinda nafasi ya kwanza katika mtihani wa hisabati alisema kuwa ushindi huo si faraja kwake tu, bali kwa wanafunzi wote wa shule hiyo, walimu na wafanyakazi wengine.
 
Abishek alisema kuwa amejituma kwa lengo la kushinda na bado anaaamini kuwa atafanya vyema katika mitihani mengine.

RC GAMBO ATOA PIKIPIKI 200 KWA WANDESHA BODA BODA -ARUSHA

boy1

Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Mrisho Gambo (Katikati) akiwasili kwenye Kikao na waendesha bodaboda wa Jiji la Arusha.
boy2
Baadhi ya waendesha boda boda wakifuatilia kikao kilichoitishwa na Mkuu wa Mkoa wa Arusha
boy3
Kaimu Katibu Tawala wa Wilaya Ndg. Polycarp Nkuyumba(aliyesimama) akiwakaribisha viongozi na wadau kwenye Kikao na waendesha boda boda wa Wilaya ya Arusha.
boy4
Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Mrisho Mashaka Gambo (aliyesimama) akiongea na madereva wa boda boda kuwaelezea mpango wa Serikali wa kuwapatia Pikipiki 200.
boy5
Lucas Malusu ni dereva wa boda boda Kutoka Kata ya Elerai (aliyesimama katikati) akitoa maoni yake katika kikao chao na Mkuu wa Mkoa wa Arusha.
boy6
Serafini Shirima(aliyesimama) ni dereva wa boda boda kutoka Kata ya Levolosi akichangia uanzishwaji wa umoja wa wandesha boda boda Wilaya ya Arusha (UBOJA)
boy7
Viongozi wa mpito waliochanguliwa kusimamia taratibu za uanzishjwaji wa Umoja huo pamoja na utoaji wa Pikipiki wa vijana nane wa Kila Kata.
boy8
Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Mrisho Gambo (aliyesimama mbele) akihitimisha kikao chake na waendesha boda boda wa Wilaya ya Arusha.
…………………………………………………….
Nteghenjwa Hosseah
Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Mrisho Mashaka Gambo amekutana na waendesha bodaboda wa Jiji la Arusha na kuwajulisha kuhusu mpango wa Serikali wa kuwakwamua kiuchumi kwa kuwawezesha kupata Pikipiki bila Riba wala dhamana.
Rc Gambo amekuja na Mpango huu wa Kuinua uchumi wa Vijana kwa kuwapatia Pikipiki  baada ya kukutana na kundi hili la waendesha boda boda  kwa mara na kusikiliza malalamiko yao huku miongoni mwa kero yao kubwa ni kutozwa fedha nyingi na wamiliki wa boda boda hizo.
Akiongea na waendesha boda boda Rc Gambo alisema ninaona jinsi mnavyojituma katika kujitafutia riziki lakini hamthaminiki na kazi hii imekua ikidharaulika, sasa  muda umefika kwa  kazi hii kuwa ya heshima mbele ya Jamii, kila kijana aliyepo katika biashara hii ataweza kumiliki Pikipiki yake na sio kuendesha Pikipiki za watu ambao wamekuwa wakiwanyonya kila siku kwa kuwatoza Fedha nyingi na wao kuzidi kuneemeka wakati ninyi mnazidi kuwa masikini.
“Kundi hili limekuwa likitumiwa kwa maslahi ya watu wachache kwa kuwa wamekuwa wakipewa Pikipiki hizo kwa faidi kubwa na mmiliki anapokea Fedha zaidi yya mara mbili ya bei ya kununulia Pikipiki hiyo ndipo aamue kummilikisha kijana pikipiki hiyo au aamue kuendelea kupokea Fedha kwa kipindi chote wakati ninyi mnapata tabu barabarani huko na mnaambulia Fedha kidogo kiasi ambacho hamuwezi fikia hatua ya kumiliki Pikipiki zenu” Alisema Gambo.
Aliongeza kuwa Serikali ya Mkoa wa Arusha imeona ni vyema ikawajengea uwezo vijana waliopo katika kazi hii kwa kuwapa mafunzo na kuwapatia Pikipiki ambazo mtatakiwa kurejesha kiasi cha Fedha halali iliyonunuliwa Pikipiki hiyo kisha kumilikishwa chombo bila ya riba yeyote wala dhamana.
Aliendelea kusema utoaji wa Pikipiki hizi utazingatia Kata zote zilizopo katika Jiji la Arusha ili Pikipiki ziweze kuwafikia walengwa na zoezi hili litaendelea kwa vijana wengine kadiri ya mahitaji; Tutaongeza usimamizi kwa wote watakaopata Pikipiki hizi ili waweze kurejesha  Fedha  kama inavyotakiwa na tuweze kuwanunulia vijana wengine hatimaye tuwafikie vijana wote wenye uhitaji wa kumiliki na kufanya biashara ya bodaboda.
Serafini  Shirima ni dereva wa boda boda Kata ya Levolosi akizungumza katika Kikao hicho alisema kwa mara ya kwanza Katika Mkoa huu wamepata mlezi anayetambua na kuthamini kazi ya boda boda na aliyethubutu kuwatafutia Pikipiki za bei nafuu ili kuongeza kipato cha vijana wa Arusha.
Shirima alishauri kuundwa kwa kamati ya mpito itakayosimamia na kuratibu mchakato mzima wa vijana watakaoanza kupewa Pikipiki hizo na kukamilisha taratibu zote za uanzishaji wa umoja wa wandesha Boda boda utakaofahamika kwa jina la (UBOJA) chini ya Mlezi Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Gambo.
RC Gambo alikamilisha Kikao hicho kwa kusimamia uchaguzi wa viongozi wa mpito kutoka katika Kila Kata na hatimaye kupatikana viongozi watano watakaoratibu mpango wa awali wa utoaji wa Pikipiki kwa vijana.
Pikipiki zitakazotolewa katika awamu ya kwanza ni 200 zikiwa na  thamani ya Tsh Mil 400 na zitatolewa sanjari na Bima kubwa(Comprehensive Insurance) kwa vijana 200 ambapo kila Kata itatakiwa kutoa vijana 8.
Vijana wa Arusha watakabidhiwa Pikipiki hizi na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassimu Majaliwa   tarehe 03/12/2016 kwenye uwanja wa Sheikh Amri Abeid.

MAKINDA:AWATAKA WANAWAKE WASIKATE TAMAA BALI WAPIGANIE HAKI ZAO


img_0989
Spika Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Mhe.Anne Makinda aliyekuwa mgeni rasmi kwenye Kongamano la kwanza la kitaifa la haki za Wanawake.
img_0962
Afisa Mtendaji Mkuu wa shirika la msaada wa kisheria Legal Services Facility (LSF).
img_1000
Mkurugenzi mtendaji wa shirika la kutetea haki za binadamu Dr.Hellen Kijo Bisimba akiongea katika kongamano hilo.
………………………………………………………………………………
Na.Alex Mathias,Dar es salaam.
Wanawake wa kitanzania wametakiwa kupigania haki zao bila kujali vikwazo wanavyokutana navyo katika mchakato wa kukabiliana na ukatili wa kijinsia katika kada zote, huku wakisaidiana na kujiamini katika kufikia lengo lao la kuhakikisha haki za wanawake zinasimamiwa.
Hayo yamesemwa na spika mstaafu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, mhe, Anne Makinda, jijini Dar es salaam wakati akifungua kongamano la kwanza la kitaifa la haki za wanawake.
Mhe, Makinda alisema kuwa wanawake waache kuwa nyuma badala yake wasimame kuzipigania haki zao na kuhakikisha kuwa malengo ya kumkomboa mwanamke yanafikiwa bila kukatishwa tamaa na vikwazo vilivyopo ikiwemo mfumo dume unao zaa unyanyasaji wa kijinsia.
“Bila kusimama sisi wenyewe na kuzipigania haki zetu, hakuna anaeweza kutusaidia, hata mimi nisingesimama mwenyewe nisingeweza kufikia nafasi nilizozifikia katika maisha yangu” Alisema mhe, Makinda.
Mhe, Makinda pia aliitaka serikali kuweka mikakati ya namna ya kusaidia mashirika yasiyo ya kiserikali yanayojihusisha na kutetea haki za wanawake nchini badala ya kutegemea wahisani pekee kwakuwa wao hufanya hivyo kwa kipindi maalum na baada ya hapo mashirika hayo hubaki bila msaada.
Kongamano hilo limeandaliwa na mfumo wa msaada wa kisheria (LSF) na kushirikisha wadau mbalimbali wa kutetea haki za wanawake nchini na kauli mbiu katika kongamano hilo ni “Jitambue, Jiamini,Simamia haki yako”
Awali akizungumza kwemye kongamano hilo, afisa  mtendaji mkuu wa LSF, Kess Greonerndijk, alisema kuwa wameamua kusaidia mapambano dhidi ya ukatili kwa wanawake na kusimamia haki zao kwakuwa bado kuna uhitaji mkubwa wa kufanya hivyo kutokana na matukio mengi ya kikatili yanayo ripotiwa kufanywa dhidi ya wanawake

STATEMENT FOR HON. PROF. MAKAME MBARAWA ON THE GLOBAL SUSTAINABLE TRANSPORT CONFERENCE, ASHGABAT, TURKMENISTAN


Mhe. Prof. Makame Mbarawa akiwa katika mazungumzo na Naibu Waziri wa Usafirishaji wa Oman Dkt. AHMED MOHAMMED SALEM AL-FITAISI pembezoni mwa mkutano wa wadau wausafirishaji unaoendelea nchini Turkeministan.
rawa2
STATEMENT FOR HON. PROF. MAKAME MBARAWA, MINISTER FOR WORKS, TRANSPORT AND COMMUNICATION OF THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA ON THE GLOBAL SUSTAINABLE TRANSPORT CONFERENCE, ASHGABAT, TURKMENISTAN ON 26TH NOVEMBER 2016
Your Excellency Ban Ki-moon, United Nations Secretary General;
Excellencies Heads of State and Government,
Excellencies High Commissioners, Ambassadors and other Members of the Diplomatic Corps;
Government Officials present here;
Distinguished Delegates;
Ladies and Gentlemen.
I am delighted to join all of you today in the first ever Global Sustainable Transport Conference. Before I proceed, let me extend Tanzania’s appreciation to the Goverment of Republic of Turkmenistan and people of Turkmenistan for their warm welcome and efforts they have taken to make this conference a success.
I also wish to commend H.E. Ban Ki-moon  for the initiative he took to conven the high-level event on a subject that is of great concern to all nations and people of the world – Sustainable transport sector.
Distinguished Delegates;
Ladies and Gentlemen.
Historically, transport has always been a driver of trade, economic growth, job creation and development. Nowadays, it is still a crucial component of innovative, socially-oriented, dynamic and sustainable progress. The main features of modern transport are its competitiveness, accessibility, environmental and safety.
Transport hubs and multimodal logistical centers are being built worldwide to connect people, services, producers and manufacturers. Connectivity – national and international – as a combination of transport, logistical, customs, financial and other services has become today’s paradigm of economic progress.
Excellencies,
Ladies and Gentlemen;
2016 is a significant year for transport as we begin to implement the 2030 Agenda for Sustainable Development. The inclusion of transport issues in the Sustainable Development Goals (SDGs) is testament to the growing recognition that transport is essential for sustainable development. Transport plays a major role in this regard: poverty eradication, good health, sustainable cities and communities and climate action are some of the SDGs where Transport can make a difference.
Excellencies,
Ladies and Gentlemen;
The expert panel report delivered to the United Nations Secretary General Ban Ki-moon on 28th October, 2016 reaffirms the central role of sustainable transport systems to advance sustainable development. To achieve the SDGs, governments will need to invest in a transport system that enhances our quality of life and meets our current and future mobility needs. The transport systems should provide seamless mobility, transport and multimodal solutions between sea, lakes, air, roads and rivers to both urban and rural areas.
The future transport systems must be ready for the fourth industrial revolution where products, services and information technology merge and move together. We must make full use of multiple transport modes to facilitate the safe movement of people, goods, and information nationally, regionally and internationally.
Excellencies,
Ladies and Gentlemen;
I commend the report of the same expert panel on “Mobilizing Sustainable Transport for Development”. This report addresses the existing inefficiencies and unsustainable investments in global, national and local transport systems. The report provides 10 recommendations on how governments, businesses and civil society should re-direct resources in the transport sector to advance sustainable development.
Modern transport systems must have users at their core. They must give due consideration to mobility; accessibility; affordability; safety; sustainability; equity; efficiency; liability; and environmental protection. It is a tall order. For example, to ensure mobility, the users must have reliable, integrated, and flexible travel choices. Transport systems should enhance public safety and security in all modes of travel; they must avoid a disproportionately adverse impact on low income, elderly, minority, or disabled populations. They must also provide equitable levels of funding and transportation services to all areas, communities, and socio-economic groups.
In the spirit of the Sustainable Development Goals: We must leave no one behind when talking about transport solutions. Transport systems must also support liveable community concepts and efforts and reflect community values while integrating land use and transportation planning.
Excellences,
Ladies and Gentlemen;
The transport sector is the largest consumer of petroleum products and a major source of air pollution, greenhouse gases and ozone-depleting substances. While many initiatives are being taken to address these issues, much needs to be done to ensure the environmental sustainability of the sector. This includes promoting energy efficient modes of transportation and improving the efficiency of freight logistic services.
I see many opportunities in transport to cut emissions of greenhouse gases. It is not only good for our climate. Innovations in sustainable transport have proven to bring economic added value as well.  According to the International Energy Agency, the world can save no less than 70 trillion dollars between now and 2050 when we switch to sustainable transport and mobility.
Excellences,
Ladies and Gentlemen;
Tanzania attaches utmost importance to the outcomes of this conference and will continue to be actively and positively engaged into its work for the benefit of dynamic and sustainable development and increased regional connectivity.
Let me concluded, by assuring you that Tanzania stands ready to cooperate with its regional blocks and the entire world to fulfil this commitment and turn this vision into a reality.
Excellences,
Ladies and Gentlemen;
I wish us all a very fruitful conference and thank you for your attention.

Waziri Nape akutana na Mshauri wa Masuala ya Utamaduni kutoka Ubalozi wa Iran kujadili masuala mbalimbali ya kiutamaduni.

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye (kulia) akimkaribisha ofisini kwake Mshauri wa masuala ya Utamaduni kutoka Ubalozi wa Iran Bw. Ali Bagheri alipowasili kwa ajili ya kujadili masuala mbalimbali ya kiutamaduni leo Jijini Dar es Salaam
nau2
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye (kulia) akizungumza masuala mbalimbali ya kiutamaduni na Mshauri wa masuala ya Utamaduni kutoka Ubalozi wa Iran Bw. Ali Bagheri alipomtembelea ofisini kwake leo Jijini Dar es Salaam
nau3
Mshauri wa masuala ya Utamaduni kutoka Ubalozi wa Iran Bw. Ali Bagheri (kulia) akizungumza na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye masuala mbalimbali ya kiutamaduni alipomtembelea ofisini kwake leo Jijini Dar es Salaam
Picha na: Genofeva Matemu