Jumatatu, 31 Oktoba 2016

SERIKALI YASITISHA KWA MUDA ZOEZI LA UPIGAJI CHAPA KWA NG’OMBE

indexNa Beatrice Lyimo-MAELEZO–DAR ES SALAAM,
Serikali imesitisha kwa muda zoezi la upigaji chapa kwa ng’ombe ili kutoa fusra kwa wadau kujadiliana na kuona namna bora ya la utekelezaji wa zoezi husika na kukabiliana na changamoto zilizojitokeza wakati wa utekelezaji.
 
Kwa mujibu wa taarifa kutoka Wizara ya Kilimo Mifugo na Uvuvi iliyosainiwa na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Bernard Kaali inasema kuwa zoezi hilo limekuwa likitekelezwa katika baadhi ya mikoa kupitia Mamlaka za Serikali za Mitaa.
Taarifa hiyo inasema kuwa zoezi hilo limetokana na sheria Na 10 ya mwaka 2010 ya utambuzi, uandikishaji na utafitiliaji wa mifugo nchini, ambapo sheria hiyo inalenga kuhakikisha ufugaji unakuwa na tija kwa kuwezesha mifugo na biidhaa zake kupenya kwenye masoko ya kimataifa.
 
Aidha, taarifa hiyo inasema kuwa sheria hiyo inasaidia katika kutatua changamoto ya migogoro baina ya wafugaji na watuamiaji wa ardhi pamoja na kudhibiti masuala ya wizi na kuenea kwa magonjwa ya mifugo.
 
Pia inasema kuwa Sheria hiyo inatekeleza uhitaji wa masoko ya kimataifa ya kuwezesha kufuatilia bidhaatoka kwa mlaji hadi kwa mzalishaji hivyo endapo zoezi hilo litatekelezwa na wadau na viongozi wa ngazi zote litakuwa na manufaa kwa wafugaji na taifa kwa ujumla na kupelekea kuleta mapinduzi katika sekta ya kilimo.
 
Hata hivyo zoezi hilo limesitishwa kwa muda muda ili kutoa nafasi kwa Wizara na wadau ikiwemo Mikoa, Mamlaka za Serikali za Mitaa na wafugaji kujipanga ili kutekeleza ubora na ufanisi

Wahariri waukubali Muswada wa Sheria ya Huduma za Habari


nap7
Anitha Jonas – MAELEZO
Wahariri wa vyombo vya habari wameukubali Muswada wa Sheria ya Huduma za Habari baada ya kuusoma kwa umakini nakuona namna gani utasaidia kuinua tasnia ya habari nchini.
Hayo yamebainishwa katika mahojiano maalum  kwa njia ya simu na baadhi ya wahariri wa vyombo vya habari akiwemo Mhariri wa Televisheni ya TV 1, Bw.Said Mwishehe huku akieleza faida za Muswada huo pamoja na kutoa maoni yake kwa kuiomba serikali kuangalia vizuri baadhi ya vipengele na kama kipengele cha 54 na 55 katika Sehemu ya Nane ili kuvipunguzia makali na kuondoa suala la kuonekana kubana uhuru wa vyombo vya habari.
“Kuna umuhimu kwa wadau wa habari kuunga mkono muswada huu badala ya kuupinga kwani una mambo mazuri yatakayosaidia kuboresha tasnia hii ya habari na kuipa heshima kama taaluma nyingine badala ya kuonekana kuwa waandishi wa habari ni watu wababaishaji tu na wasiyo na taaluma iliyo imara,”alisema Bw.Mwishehe.
Pamoja na hayo Mhariri huyo aliendelea kusema amefurahishwa na muswada kwa namna unavyojali maslahi ya waandishi wa habari pale unapoeleza kuwa wamiliki wa vyombo vya habari watahitajika kuwakatia bima waandishi wa habari  kwa hiyo itakuwa jambo la busara kwani waandishi wamekuwa wakifanya kazi katika mazingira magumu yanayohatarisha afya zao pasipo kuwa na bima inayomlinda akiwa kazini.
Aidha, Bw.Mwishehe aliwasihi wadau wa sekta ya habari kutuma maoni yao kwa vile vipengele vya muswada vinavyoonyesha kutokuwa sawa na pia ameiomba serikali kuwa na utayari wa kuyapokea maoni hayo  kwa ajjili ya kuboresha muswada huo na kuufanya bora na wenye tija katika tasnia ya habari nchini.
Naye Mhariri wa Gazeti la Mtanzania, Bw.Revocatus Makaranga alisema Muswada huo wa habari una mambo mazuri yanayoipeleka tasnia mahali pazuri ikiwemo suala la waandishi wa habari kuhitajika kujiendeleza katika elimu ya juu  na hii itasaidia kukuza upeo wa mwandishi na kumfanya awe na uwezo mkubwa na kufanya kazi kwa kujiamini kama ilivyo kwa waandishi wa nchi zilizoendelea.
Bw.Makaranga aliongeza kusema muswada una vipengele ambavyo ipo haja ya serikali kuvifanyia marekebisho ikiwemo suala la adhabu inayotolewa kwa waandishi ya kuwafungia pale wanapokuwa wamekosea.
Pia mhariri huyo ameipongeza serikali kwa muswada huo ambao utaleta picha mpya ya kimaendeleo katika tasnia ya habari ikiwemo suala la  kuanzishwa kwa Mfuko wa mafunzo kwa wanahabari nchini ambapo utasaidia kutoa elimu kwa waandishi mara kwa mara na kuwajengea uwezo wa utendaji.
Kwa upande wake, Mhariri Mkuu wa kituo cha Redio Efm, Bi Scolastika Mazula alisema katika muswada huo wa habari yapo mambo mazuri yenye tija katika sekta ya habari kama suala la kuanzishwa kwa Mfuko wa mafunzo kwa wanahabari ni jambo jema sana kwani utasaidia kutoa fursa za waandishi kujiendeleza kimasomo na kuifanya fani ya habari kuwa na wasomi zaidi tofauti na inavyoonekana kwa sasa.
“Suala la elimu kwa waandishi ni bora liwekwe wazi kisheria kwani tansnia hii ya habari inahitajika kuheshimika kama ilivyo tansia nyingine badala ya kuonekana wababaishaji”, alisema Mazula.
Pamoja na hayo Bi. Mazula aliendelea kutoa maoni yake kuhusu Muswada kwa kusema kuwa  suala la kuanzishwa kwa bodi ni zuri ila ingekuwa vyema kama bodi hiyo itakuwa na asilimia kubwa ya wadau wa habari na ijitegemee na Waziri mwenye dhamana ya habari na Mwanasheria Mkuu wasiwe na mamlaka sana katika bodi hiyo.
Pamoja na hayo naye Katibu wa Jukwaa la Wahariri, Bw.Neville Meena alisema kwa sasa wanajukwaa wameshatoa maoni yao kuhusu muswada huo na watayawasilisha kwa ajili ya kusaidia kuboresha muswada huo na kuufanya uwe na tija na manufaa zaidi katika kuendeleza tasnia ya habari nchini.

ERENGETI NA BUNDA WANUFAIKA NA UWEKEZAJI WA SINGITA GRUMETI.


gru1
Mkurugenzi wa Singita Grumeti Stephen Cunliffe (kulia) akimkabidhi Mkuu wa Mkoa wa Mara Dk. Charles Mlingwa msaada wa madawati 500 yenye Thamani ya Tshs Milioni 112 kwa ajili ya Wilaya za Serengeti na Bunda katika hafla  iliyofanyika  Shule ya Msingi Makundusi Wilayani Serengeti.
gru2
Mkurugenzi wa Singita Grumeti Stephen Cunliffe (kulia) akimkabidhi Mkuu wa Mkoa wa Mara Dk. Charles Mlingwa nyumba ya kuishi mwalimu yenye thamani ya Tshs Milioni 86 iliyojengwa katika Shule ya Msingi Makundusi Wilayani Serengeti.
gru3
Mkuu wa Huduma za Jamii Singta grumeti Richard Ndaskoi (kulia) akimkabidhi Mkuu wa Mkoa wa Mara Dk. Charles Mlingwa msaada wa madawati 500 yenye Thamani ya Tshs Milioni 112 kwa ajili ya Wilaya za Serengeti na Bunda katika hafla  iliyofanyika  Shule ya Msingi Makundusi Wilayani Serengeti
gru4
Madawati yaliyotolewa na Mfuko wa Singita Grumeti kwa ajili ya Wilaya ya Bunda.
…………………………………………………
Mfuko wa Singita Grumeti umeendelea kuwa mstari wa mbele katika kuboresha hali ya elimu katika Wilaya za Serengeti na Bunda.
Hii imedhihirika kwenye halfa ya kukabidhi madawati 500 kwa Mkuu wa Mkoa wa Mara Dk. Charles Mlingwa ili kupunguza uhaba wa madawati katika Wilaya hizo. Aidha Grumeti wamekabidhi nyumba ya kuishi mwalimu iliyojengwa katika Shule ya Msingi Makundusi.
“Tuko hapa kukabidhi madawati haya 500 yenye thamani ya Tshs Milioni 112 kwa Wilaya za Serengeti na Bunda pamoja na nyumba hii yenye thamani ya Tshs Milioni 86” alisema Richard Ndaskoi ambae ni Mkuu wa Huduma za Jamii toka Mfuko wa Singinta Grumeti.
Akipokea misaada hiyo, Dk. Mlingwa alisema “Nawashukuru Singita Grumeti kwa Msaada huu wa madawati pamoja na nyumba hakika mchango wenu katika Mkoa wa Mara unaoneka” Dk Mlingwa amewataka wawekezaji wengine katika Mkoa wa Mara kuchangia madawati katika Wilaya za Serengeti na Bunda kwani bado zina uhaba wa madawati. 
Aidha Dk. Mlingwa ameipongeza Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti kwa kuwa na mahusiano mazuri na wawekezaji waliopo katika Wilaya hiyo “Tukiwawekea mazingira mazuri ya kufanya shughuli zao hata wananchi pia watanufaika na uwepo wa wawekezaji hawa” alisema Dk. Mlingwa.
Naye Mkuu wa Wilaya ya Serengeti, Nurdin Babu pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Bunda, Lydia Bupilipili wote kwa nyakati tofauti wameushukuru Mfuko wa Singita Grumeti kwa msaada huo wa madawati na kuuomba mfuko huo kuendelea kuchangia katika shughuli za maendeleo katika Wilaya za Serengeti na Bunda. “Wilaya hii ina wawekezaji wengi lakini wamekuwa nyuma katika kuchangia shughuli za maendeleo, nawapongeza kwa kuwa mstari wa mbele kusaidia jamii inayowazunguka pamoja na kuchangia katika maendeleo ya Wilaya ya Serengeti” alisema Nurdin Babu.
Aidha Bi. Bupilipili ameuomba Mfuko huo kuanzisha kampeni maalumu ya kuongeza kiwango cha ufaulu kwa watoto wa kike kwa shule za sekondari Wilayani Bunda.
Singita Grumeti wamekuwa wawekezaji wenye tija kwa wananchi wa Wilaya za Serengeti na Bunda licha ya kuwa mstari wa mbele kuchangia katika shughuli za maendeleo, kampuni hiyo pia imekuwa ikitoa ajira kwa wakazi toka wilaya hizo mbili pamoja na kutoa ufadhili wa masomo kwa wanafunzi toka wilaya hizo.

BALE ASAINI MKATABA MPYA REAL MADRID HADI 2022.

Mchezaji namba mbili kwa gharama kubwa ya usajiindexli Gareth Bale amejitia kitanzi katika klabu ya  Real Madrid kwa kusaini Mkataba mpya utakaomuweka hadi 2022.

Bale aliyevunja rekodi ya usajili akitokea timu ya Tottenham Hotspur mwaka 2-13 na baadaye Paul Pogba alivunja rekodi yake na kuwa mchezaji ghali kuliko wote duniani kwa usajili akitokea Juventus na kujiunga na timu yake ya Zamani ya Manchester United chini ya meneja mwenye maneno mengi kuliko wote Ligi Kuu ya Uingrereza, Jose Mourinho mwaka huu.

Tiyari ameisaidia Madrid kushinda vikombe vitano katika misimu mitatu ya nyuma ikiwemo ligi ya mabingwa Ulaya mara 2 huku akifunga magoli 62 katika michezo 135.

Kwa kusaini kwake anaungana na viungo wawili wa timu hiyo Luka Modric na Toni Kroos nao pia walisaini mikataba mipya mwezi huu.

Mkataba wa Bale unatajwa kuwa wa Euro 600,000 kwa wiki huku baada ya makato ya kodi ikiwa Euro 350,000

MUSWADA WA SHERIA YA HUDUMA ZA HABARI UTAIPA HADHI TASNIA YA HABARI.


bwee
Na Ismail Ngayonga-Dar es Salaam.
BUNGE la 11 la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kesho (leo) linatarajia kuanza mkutano wake wa tano, ambapo macho na masikio ya wadau na wananchi mbalimbali yataelekezwa katika mjadala wa miswada mbalimbali ikiwemo ule wa huduma za habari wa mwaka 2016.
Tangu muswada huo uliposomwa kwa mara ya kwanza Bungeni tarehe 16 Septemba mwaka huu, wadau mbalimbali wa habari na wasomi, vyama vya kitaaluma ya habari wamekuwa na mitazamo na misimamo tofuati kuhusu muswada huo.
Miongoni mwa hoja zilizotawala katika mijadala ya wadau ni pamoja na kuongezwa muda wa kujadili muswada huo kwa kina zaidi ili kutoa fursa kwa wadau kuelewa kwa usahihi vipengele vilivyopo katika muswada huo.
Itakumbukwa  mwaka 2006, Serikali iliwasilisha kwa wadau miswada miwili ya Haki ya Kupata Habari na Huduma za Habari ili kuwawezesha kupitia kwa kina vipengele hivyo ili kuboresha uendeshaji na usimamizi wa vyombo vya habari nchini.
Maoni na mapendekezo ya wadau wa habari juu ya muswada wa haki ya kupata habari wa mwaka 2006 yalikamilika na kuwasilishwa Serikalini mwaka 2007 na mapendekezo ya muswada wa huduma za habari uliwasilishwa mwaka 2008.
Kwa kuzingatia uhitaji wa muda mrefu wa sheria hizo, mwezi septemba mwaka huu Serikali iliwasilisha Bungeni muswada wa sheria ya haki ya kupata taarifa, ambayo ilisomwa, kujadiliwa na kupitishwa na Bunge.
Pamoja na dhamira ya dhati ya Serikali ya kuharakisha mchakato wa kutungwa kwa sheria hizo, inasikitisha kuona wadau wa habari wakiwemo baadhi ya wamiliki, wahariri, vyombo vya habari na waandishi wa habari wakibishana katika majukwaa na mitandao ya kijamii.
Inashangaza kuona miongoni mwa wadau wanaobishana kuhusu muswada huo ni miongoni mwa taasisi za kisheria ambazo ziliusoma muswada huo, kuujadili na kuwasilisha maoni yao mbele ya Kamati ya Bunge kabla muswada huo kusomwa kwa mara ya kwanza Bungeni mwezi septemba mwaka huu.
Muswada umeweka wazi wajibu, haki na maslahi ya wamiliki, wahariri, vyombo vya habari na waandishi wa habari ambayo kwa kipindi kirefu yameshindwa kutambuliwa kutokana na kukosekana kwa mfumo wa kisheria.
Sura ya nne ya muswada imeainisha uanzishaji wa Baraza huru la Habari, ambalo wadau wa habari wamekuwa wakilihitaji kwa ajili ya kuanzisha chombo huru cha wanahabari kinachosimamia haki, wajibu usalama na maslahi ya waandishi wa habari.
Kipengele hicho cha muswada kimekusudia kuongeza na kuimarisha wajibu wa vyombo vya habari katika jamii, na kuifanya tasnia ya habari kuaminika na kudhaminiwa na jamii.
Katika katika nchi zinazoendelea ikiwemo Tanzania, vyombo vya habari vimekuwa chachu ya ujenzi wa maadili ya jamii, nguzo ya amani, mshikamano na utulivu, sambamba na kitovu cha mabadiliko ya kifikra na mawazo ndani ya jamii.
Ili kutekeleza wajibu huo wa msingi ni vyema vyombo vya habari  wajibu kuzingatia miiko, maadili na usalama wa nchi kama ilivyobainishwa katika sheria mbalimbali za nchi ikiwemo sheria ya magazeti ya mwaka 1976.
Ibara ya 18 ya katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imeanisha haki na uhuru mawazo:   “Bila ya kuathiri sheria za nchi, kila mtu yuko huru kuwa na maoni yoyote na kutoa nje mawazo yake, na kutafuta, kupokea na kutoa habari na dhana zozote kupitia chombo chochote bila ya kujali mipaka ya nchi”.
Waandishi wa habari wanakumbushwa pia kusoma Ibara ya 31 ya Katiba inayosisitiza kuhusu  madaraka ya  pekee ya mamlaka ya nchi kuhusu ukiukaji wa haki na uhuru.
Tanzania kama zilivyo nchi nyingine duniani zina zimeanisha taratibu za ukomo wa kuzuia utangazaji na uchapishaji wa habari zinazohatarisha usalama wa taifa ikiwemo vita, uasi, mapigano na kadhalika.
Sheria na mikataba ya mbalimbali za kimataifa ikiwemo ibara ya 19 ya mkataba wa kimataifa wa haki za kiraia na kisiasa, umeainisha ukomo wa vyombo vya habari katika masuala ya usalama wa taifa, kashfa na maadili ya taifa.  
Wakati tukielekea katika utungaji wa sheria hiyo, ni wajibu wa wadau wa habari kuwa katika mlengo mmoja, kwa kuwa sheria kiasi kikubwa imekusudia kumkomboa mwandishi wa habari wa Tanzania kuondokana na maslahi duni yaliyopo katika vyombo mbalimbali vya habari.
Aidha kutungwa kwa sheria hizo mbili haki ya kupata habari na sheria ya huduma ya habari ni moja ya dhamira za mipango ya kuendesha shughuli za Serikali kwa uwazi, ikiwa ni utekelezaji wa ahadi iliyotolewa Rais mstaafu Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete Jijini London Uingereza wakati wa mkutano wa OGP mwaka 2013 na 2014.

MAKAMU WA RAIS AFUNGUA TAMASHA LA MAZINGIRA NA MABADILIKO YA TABIA NCHI KATIKA UKUMBI WA NKURUMAH HALL CHUO KIKUU CHA DAR ES SALAAM


 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwasili kwenye ukumbi wa Nkurumah Hall,tayari kufungua mkutano kimataifa unaohusu mabadiliko ya tabia ya nchi unaokutanisha wanasayansi, watafiti na wadau wa mazingira chini ya Usimamizi wa Kigoda cha mwalimu Julius Nyerere cha Mazingira na mabadiliko ya Tabia ya nchini katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
 
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia kwenye ufunguzi wa mkutano kimataifa unaohusu mabadiliko ya tabia ya nchi unaokutanisha wanasayansi, watafiti na wadau wa mazingira chini ya Usimamizi wa Kigoda cha
mwalimu Julius Nyerere cha Mazingira na mabadiliko ya Tabia ya nchini katika ukumbi wa Nkurumah Hall, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
Wajumbe walihudhuria mkutano wakimsikiliza Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan
wakati akihutubia kwenye ufunguzi wa 
mkutano kimataifa unaohusu mabadiliko ya tabia ya nchi unaokutanisha wanasayansi, watafiti na wadau wa mazingira chini ya Usimamizi wa Kigoda cha mwalimu Julius Nyerere cha Mazingira na mabadiliko ya Tabia ya nchini katika
ukumbi wa Nkurumah Hall, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.                     

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan  akikikata utepe kuashiria kuzindia kitabu cha Pastoralism and Climate Change in East Africa kwenye Tamasha la Mazingira na Mabadiliko ya Tabia Nchi unaokutanisha wanasayansi, watafiti na wadau wa mazingira chini ya Usimamizi wa Kigoda cha mwalimu Julius Nyerere cha Mazingira na mabadiliko ya Tabia ya nchini katika ukumbi wa Nkurumah Hall, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiongoza viongozi wengine kuonyesha juu kitabu cha Pastoralism and Climate Change in East Africa kuashiria kimezinduliwa rasmi kwenye Tamasha la Mazingira na Mabadiliko ya Tabia Nchiunaokutanisha wanasayansi, watafiti na wadau wa mazingira chini ya Usimamizi wa Kigoda cha mwalimu Julius Nyerere cha Mazingira na mabadiliko ya Tabia ya nchini katika ukumbi wa Nkurumah Hall, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
                                 ………………………………………………………………..
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amepiga marufuku
uharibifu mkubwa wa mazingira unaendelea katika maeneo mbalimbali nchini ambao unaweza kusababisha nchi kugeuka jangwa.
Makamu wa Rais ametoa kauli hiyo wakati akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya
kufungua mkutano kimataifa unaohusu mabadiliko ya tabia ya nchi unaokutanisha wanasayansi, watafiti na wadau wa mazingira
chini ya Usimamizi wa Kigoda cha mwalimu Julius Nyerere cha Mazingira na mabadiliko ya Tabia ya nchini katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
 
Makamu wa Rais ameonya kuwa jukumu la kuhifadhi mazingira sio la Serikali peke yake bali
ni kila mwananchi na wadau wa mazingira kwa ujumla, hivyo wananchi ni muhimu kwa umoja wao wakaongeza jitihada za kupanda miti katika maeneo yao ili kukabiliana na hali tete ya uhabifu wa mazingira nchini.
“Uharibifu wa mazingira usimame leo na marekebisho ya uharibifu tulioufanya uanze leo na hili ni jukumu la kila Mtanzania” Makamu wa Rais pia ametoa wito maalum kwa viongozi wa ngazi zote nchini kuchukua hatua katika kulinda na kuhifadhi vyanzo vya maji katika maeneo yao ili visitoweke.
 
Makamu wa Rais ametahadharisha kuwa mabadiliko ya tabia ya nchi yameanza kuleta athari si
kwa Tanzania na dunia kwa ujumla hivyo jitihada za makusudi zinahitajika ili kuhakikisha changamoto zinazojitokeza kwa sasa zinakabiliwa ipasavyo.
 
Kwa upande wake,Mkurugenzi wa Kituo cha Mafunzo ya mabadiliko ya Tabia ya nchi,Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Profesa Pius Yanda amesema mkutano huo wa siku TANO utakuwa na jukumu kubwa la kujadili kwa kina namna bora ya kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabia ya nchi. BOFYA HAPA KWA PICH ZAIDI

DK. SHEIN AKUTANA NA UONGOZI WA WIZARA YA NCHI OFISI YA RAIS,TAWALA ZA MIKOA SERIKALI ZA MITAA NA IDARA MAALUM ZA SMZ


mku2
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) akizungumza na Uongozi wa Wizara ya Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa,Serikali za Mitaa na Idara Maalum za SMZ  wakati wa   kikao cha Mpango kazi wa mwaka 2016-2017 katika  utekelezaji wa  robo mwaka ya kwanza ya Julai-Septemba 2016 kilichofanyika leo  Ikulu Mjini Unguja,[Picha na Ikulu.] 31/10 /2016.
mku3
Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja Mhe,Ayoub Mohamed Mahmoud akisoma kazi za Mpango kazi wa mwaka 2016-2017 katika  utekelezaji wa  robo mwaka ya kwanza ya Julai-Septemba 2016 kilichofanyika leo  Ikulu Mjini Unguja, chini ya Mwenyekiti weke Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,(kulia) Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa anayeshuhulikia Idara Maalum za SMZ ACP Sida Muhamed Himid na (kushoto) Mkuu wa Mkoa wa Kusini Unguja Dkt.Idriss Muslim Hija,[Picha na Ikulu.] 31/10 /2016.
mku4
Baadhi ya Wakuu wa Mikoa na Makatibu Tawala katika  Wizara ya Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa,Serikali za Mitaa na Idara Maalum za SMZ  wakiwa katika kikao cha Mpango kazi wa mwaka 2016-2017 katika  kikao  cha robo mwaka ya kwanza ya  Julai-Septemba 2016 kilichofanyika leo   Ikulu Mjini Unguja,chini ya mwenyekiti wakeRais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani),[Picha na Ikulu.] 24/10 /2016.
mku5
Mshauri wa Rais Ushirikiano wa Kimataifa,Fedha na Uchumi Ikulu Mhe,Balozi Mohamed Ramia Abdiwawa,akiuliza suala wakati wa kikao cha  Mpango kazi wa mwaka 2016-2017 cha Wizara ya Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa,Serikali za Mitaa na Idara Maalum za SMZ  katika  utekelezaji wa  robo mwaka ya kwanza ya Julai-Septemba 2016 kilichofanyika leo  Ikulu Mjini Unguja, chini ya Mwenyekiti weke Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,(kushoto) Makamo wa Pili wa Rais Mhe,Balozi Seif Ali Iddi,na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Nd, Radhiya Rashid [Picha na Ikulu] 31/10/2016.
mku6
Viongozi wa Idara mbali mbali katika Wizara ya Wizara ya Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa,Serikali za Mitaa na Idara Maalum za SMZ  wakiwa katika  mkutano wa  siku moja unaozungumzia  Mpango kazi wa mwaka 2016-2017   katika  utekelezaji wa  robo mwaka ya kwanza ya  Julai-Septemba 2016 uliofanyika leo Ikulu Mjini Unguja,chini ya mwenyekiti wake Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani),[Picha na Ikulu.] 31/10 /2016.
mku7
Mkuu wa Wilaya ya Magharibi “B” Unguja Mhe,Mwinyiussi Abdalla Hassan (kushoto) akisisitiza jambo wakati akiwa na Wakuu wa Wilaya nyengine   katika  mkutano wa  siku moja unaozungumzia  Mpango kazi wa mwaka 2016-2017   katika  utekelezaji wa  robo mwaka ya kwanza ya  Julai-Septemba 2016 uliofanyika leo Ikulu Mjini Unguja,chini ya mwenyekiti wake Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani),[Picha na Ikulu.] 31/10 /2016.