Ijumaa, 21 Oktoba 2016

NHC LAFANYA UHAKIKI WA VIKUNDI VYA VIJANA KATIKA MIKOA YA MWANZA, GEITA NA MARA

Jengo la ofisi linalojengwa na vijana wa kikundi cha Sarorya ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa mradi wa vijana wa kutengeneza matofali ya kufungamana kupitia mashine zilizotolewa na NHC kama msaada kwa vijana. Wa Pili Kulia ni Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Huduma kwa Jamii, Susan Omari ambaye aliongoza ujumbe wa NHC  katika uhakiki wa shughuli zinazofanywa na vijana hao baada ya kupewa msaada wa mashine.
nc2
Kanisa lililojengwa na vijana  wa kikundi cha Hope Revival – Manispaa ya Musoma ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa mradi wa vijana wa kutengeneza matofali ya kufungamana kupitia mashine zilizotolewa na NHC kama msaada kwa vijana.
nc3

nc4
Meneja wa Mkoa wa Mwanza Mhandisi Benedict Kilimba ya utekelezaji wa mradi wa vijana wa kufyatua matofali yanayofungamana kupitia ufadhili wa na NHC wa msaada wa mashine ya kufyatua matofali kwa vijana wa Manispaa ya Ilemela – Mwanza.
nc5
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Huduma kwa Jamii, Susan Omari akiwa katika mahojiano na vyombo vya habari baada ya kuhakiki vikundi vya vijana wa Ukombozi Vijana Magu kwenye eneo lao la kazi wanalotegemea kujenga nyumba.
nc6
Moja ya kazi za vijana wa kikundi cha Sarorya – Halmashauri ya Rorya ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa mradi wa vijana wa kutengeneza matofali ya kufungamana kupitia mashine zilizotolewa na NHC kama msaada kwa vijana.
nc7
Moja ya Nyumba iliyojengwa na vijana wa kikundi cha Ukombozi Vijana – Halmashauri ya Magu.
nc8
 Moja ya Nyumba iliyojengwa na vijana wa kikundi cha Ukombozi Vijana – Halmashauri ya Magu.
nc9
 Nyumba iliyojengwa na kikundi cha Ukombozi Vijana Magu.
nc10
Nyumba iliyogengwa na vijana Ukombozi Vijana Halmashauri ya Magu.
nc11
 Nyumba iliyojengwa na vijana wa kikundi cha JOMUGI Maswa.
nc12
 Nyumba iliyojengwa na vijana wa Misungwi.
nc13
 Nyumba ya mwananchi iliyojengwa na vijana Rorya.
nc14
 Picha ya pamoja na vijana wa kikundi cha Ukombozi Vijana Magu mble ya mojawapo ya nyumba ziliyojengwa na vijana hao
nc15
 Eneo jingine la kazi ya vikundi cha Ukombozi Vijana Magu.
nc16
Eneo la kazi la kufyatua matofali ya vijana wa Misungwi.
nc17
Eneo la kazi la kufyatua matofali ya vijana wa Misungwi.
nc18
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Huduma kwa Jamii, Susan Omari na timu yake ya NHC akikagua matundu kumi  vya choo vilivyojengwa na vijana wa kikundi Jiendeleze – Halmashauri ya Musoma Vijijini.
nc19
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Huduma kwa Jamii, Susan Omari na Ujumbe wa NHC wakipata maelekezo kutoka kwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya wa ya Magu Bw. Lutengano Mwalwiba.
nc20
 Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Huduma kwa Jamii, Susan Omari na Ujumbe wa NHC wakipata maelekezo kutoka kwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti  Bw. Juma Hamsini.
nc21
  Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Huduma kwa Jamii, Susan Omari na Ujumbe wa NHC wakipata maelekezo kutoka kutoka kwa Mkuu wa wilaya ya  Biutiama Bi. Anna Nyamubi.
nc22
 Ujumbe kutoka NHC ukizungumza na Mkurugenzi  Halmashauri ya Mji wa Tarime Bw. Fidelica Myovella.
nc23
Ujumbe wa NHC ukipata maelekeo kutoka kwa Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Rorya Bw. Gasper Mago.

MVUVI AFARIKI AKIVUA BAHARINI MICHEWENI PEMBA

bah
Na Masanja Mabula –Pemba ..
 
MZEE  mmoja anayejulikana kwa jina la Saleh Ali Mbwana mwenye umri wa miaka 45 mkaazi wa Maziwang’ombe Wilaya ya Micheweni  amefariki dunia baada ya kuzama maji   baharini akiwa katika shuhuli zake za  uvuvi .
 
Akidhibitisha kutokea kwa tokeo hilo kamanda wa Polisi Mkoa wa Kaskazini Kamishna Msaidizi Haji Khamis Haji  amesema tukio hilo limetokea oktoba 20  mwaka huu majira ya saa saba za mchana katika bahari ya Maziwang’ombe .
 
Amesema kwamba kabla ya kifo chake , marahemu aliondoka nyumbani kwake kwenda baharini kuvua , na alifikutwa na mauti hayo katika bahari  wakati akitekeleza shuhuli zake za uvuvi.
 
Kkufuatia kutokea kwa tukio hilo Kamanda Haji  amewataka wananchi hususani wanaotoka maeneo ya ukanda wa bahari wanapokwenda kuvua au kulima mwani  kufuatana na wenzao ili patakapo tokea hitilafu waweze kusaidiana .
 
“Wito wangu kwa wananchi ni kuacha kwenda baharini aidha kwa uvuvi au kulima mwani wakiwa mmoja mmoja , bali wafuatane na wenzao ili kuweza kusaidiana panapotokea matatizo ”alisisitiza.
 
 Akizungumza baada ya uchunguzi daktari dhamana wa hospitali ya Wilaya ya Micheweni Dk  Rashid Daudi Mkasha amesema chanzo cha kifo chake kimesababishwa na kukosa hewa  baada ya kukaa nchini ya bahari kwa muda mrefu .
 
Alifahamisha kwamba kitendo cha kukaa chini ya maji  baharini kumesababisha kunywa maji mengi na kupelekea kukosa uwezo wa kuvuta hewa kutokana na maji aliyokunywa bila kutegemea.
 
“Uchunguzi wa kitaalamu umebainisha kwamba kifo kimesababishwa na kunywa maji mengi wakati akiwa chini ya maji ya bahari pamoja na kukosa uwezo wa kuvuta pumzi ”alifahamisha.
 
Mashuda wa tukio hilo  ambao hawakutaka kutajwa majina  yao wameeleza kuwa kabla ya kifo chake Saleh aliondoka nyumbani kwake kuelekea baharini kutafuta riziki na kukutwa na mauti .
Mwili wa marehemu ulikabidhiwa kwa ngudu na jamaa baada ya kufanyiwa uchunguzi na dk wa Serikali ambapo mazishi yake yalifanyika katika maburi ya Maziwang’ombe

NHC LAFANYA UHAKIKI WA VIKUNDI VYA VIJANA KATIKA MIKOA YA MWANZA, GEITA NA MARA

nc1
Jengo la ofisi linalojengwa na vijana wa kikundi cha Sarorya ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa mradi wa vijana wa kutengeneza matofali ya kufungamana kupitia mashine zilizotolewa na NHC kama msaada kwa vijana. Wa Pili Kulia ni Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Huduma kwa Jamii, Susan Omari ambaye aliongoza ujumbe wa NHC  katika uhakiki wa shughuli zinazofanywa na vijana hao baada ya kupewa msaada wa mashine.
nc2
Kanisa lililojengwa na vijana  wa kikundi cha Hope Revival – Manispaa ya Musoma ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa mradi wa vijana wa kutengeneza matofali ya kufungamana kupitia mashine zilizotolewa na NHC kama msaada kwa vijana.
nc3
 Kanisa lililojengwa na vijana  wa kikundi cha Hope Revival – Manispaa ya Musoma ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa mradi wa vijana wa kutengeneza matofali ya kufungamana kupitia mashine zilizotolewa na NHC kama msaada kwa vijana.
nc4
Meneja wa Mkoa wa Mwanza Mhandisi Benedict Kilimba ya utekelezaji wa mradi wa vijana wa kufyatua matofali yanayofungamana kupitia ufadhili wa na NHC wa msaada wa mashine ya kufyatua matofali kwa vijana wa Manispaa ya Ilemela – Mwanza.
nc5
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Huduma kwa Jamii, Susan Omari akiwa katika mahojiano na vyombo vya habari baada ya kuhakiki vikundi vya vijana wa Ukombozi Vijana Magu kwenye eneo lao la kazi wanalotegemea kujenga nyumba.
nc6
Moja ya kazi za vijana wa kikundi cha Sarorya – Halmashauri ya Rorya ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa mradi wa vijana wa kutengeneza matofali ya kufungamana kupitia mashine zilizotolewa na NHC kama msaada kwa vijana.
nc7
Moja ya Nyumba iliyojengwa na vijana wa kikundi cha Ukombozi Vijana – Halmashauri ya Magu.
nc8
 Moja ya Nyumba iliyojengwa na vijana wa kikundi cha Ukombozi Vijana – Halmashauri ya Magu.
nc9
 Nyumba iliyojengwa na kikundi cha Ukombozi Vijana Magu.
nc10
Nyumba iliyogengwa na vijana Ukombozi Vijana Halmashauri ya Magu.
nc11
 Nyumba iliyojengwa na vijana wa kikundi cha JOMUGI Maswa.
nc12
 Nyumba iliyojengwa na vijana wa Misungwi.
nc13
 Nyumba ya mwananchi iliyojengwa na vijana Rorya.
nc14
 Picha ya pamoja na vijana wa kikundi cha Ukombozi Vijana Magu mble ya mojawapo ya nyumba ziliyojengwa na vijana hao
nc15
 Eneo jingine la kazi ya vikundi cha Ukombozi Vijana Magu.
nc16
Eneo la kazi la kufyatua matofali ya vijana wa Misungwi.
nc17
Eneo la kazi la kufyatua matofali ya vijana wa Misungwi.
nc18
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Huduma kwa Jamii, Susan Omari na timu yake ya NHC akikagua matundu kumi  vya choo vilivyojengwa na vijana wa kikundi Jiendeleze – Halmashauri ya Musoma Vijijini.
nc19
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Huduma kwa Jamii, Susan Omari na Ujumbe wa NHC wakipata maelekezo kutoka kwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya wa ya Magu Bw. Lutengano Mwalwiba.
nc20
 Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Huduma kwa Jamii, Susan Omari na Ujumbe wa NHC wakipata maelekezo kutoka kwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti  Bw. Juma Hamsini.
nc21
  Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Huduma kwa Jamii, Susan Omari na Ujumbe wa NHC wakipata maelekezo kutoka kutoka kwa Mkuu wa wilaya ya  Biutiama Bi. Anna Nyamubi.
nc22
 Ujumbe kutoka NHC ukizungumza na Mkurugenzi  Halmashauri ya Mji wa Tarime Bw. Fidelica Myovella.
nc23
Ujumbe wa NHC ukipata maelekeo kutoka kwa Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Rorya Bw. Gasper Mago.

Wakazi wa Bunju Beach wahakikishiwa ulinzi na usalama.

kile1
RPC wa Kinondoni Suzan Kaganda akizungumza na wanajumuiya ya Bunju Beach Community Support wakati wa hafla ya kujumuika pamoja kwa wanajumuiya hao hivi karibuni Jijini Dar es Salaam.Kutoka kulia ni Diwani wa Kata ya Bunju Mhe. Phocas Nato, OCD Kawe, John Malulu na Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo Bw. Kheri Nassor Missinga.
kile2
Makamu Mwenyekiti wa Jumuiya ya wakazi wa Bunju Beach,Bunju Beach Community Support Bi.Vanessa Milinga akisoma risala ya Jumuiya hiyo wakati wa hafla ya kujumuika pamoja kwa wanajumuiya hivi karibuni Jijini Dar es Salaam.
kile3
RPC wa Kinondoni Suzan Kaganda akipeana mkono na Makamu Mwenyekiti wa Jumuiya ya wakazi wa Bunju Beach (Bunju Beach Community Support) Bi. Vanessa Milinga mara baada ya kumkabidhi risala wakati wa hafla ya kujumuika pamoja kwa wanajumuiya hao hivi karibuni Jijini Dar es Salaam. Kutoka kulia ni Diwani wa Kata ya Bunju Mhe. Phocas Nato na Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo Bw. Kheri Nassor Missinga.
kile4
Muasisi wa Jumuiya ya Bunju Community Support Profesa. Joas Rugemalila (kushoto) akigonga cheers na RPC wa Kinondoni Suzan Kaganda wakati wa hafla ya kujumuika pamoja kwa wanajumuiya hao hivi karibuni Jijini Dar es Salaam. Kutoka kulia ni Diwani wa Kata ya Bunju Mhe. Phocas Nato na Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo Bw. Kheri Nassor Missinga.
kile5
RPC wa Kinondoni Suzan Kaganda wakigonga cheers wakati wa hafla ya kujumuika pamoja kwa wanajumuiya hao hivi karibuni Jijini Dar es Salaam. Kutoka kulia ni Diwani wa Kata ya Bunju Mhe. Phocas Nato na Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo Bw. Kheri Nassor Missinga.
…………………………………………………………………..
Na: Mwandishi Wetu.
SUALA la wizi na ujambazi kwa wakazi wa Bunju Beach kubakia kuwa historia baada ya Jeshi la Polisi wilaya ya Kinondoni kuahidi kujenga kituo cha Polisi kitakachokuwa na uwezo wa kuchukua Askari zaidi ya 40.
Hayo yamebainishwa na Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Kinondoni, ACP Suzan Kaganda alipokuwa mgeni rasmi katika hafla ya kuzindua umoja wa Wakazi wa Bunju “Bunju Beach Community Support”
RPC Kaganda amesema kuwa wezi na majambazi wamekula kwao na kuongeza kuwa suala la ulinzi na usalama ni la kila raia kwa mujibu wa sheria.
Awali akisoma risala ya Jumuiya hiyo Makamu Mwenyekiti wa Jumuiya ya kusaidiana ya Wakazi wa Bunju (Bunju Beach Community Support), Vanessa Milinga alisema kuwa Jumuiya hiyo ilianzishwa mwaka 2005 ikiwa na lengo la kuimarisha ulinzi na usalama wa mali na familia za wakazi wa Bunju Beach.
Vanessa amesema kuwa mwaka 2011 walipata usajili ambapo pia wanachama wameongezeka na kupelekea kubadili kuongezeka kwa malengo ambayo ni pamoja na kuanzishwa kwa SACCOSS.
Akizungumzia historia ya Bunju Beach Community Support, Mmoja wa waanzilishi wa Jumuiya hiyo Profesa. Joas Rugemalila amesema kuwa umoja huo umeanzishwa kwa lengo la kuimarisha ulinzi shirikishi, usalama, amani na maendeleo.

MJADALA WA MUSWADA WA SHERIA YA HUDUMA ZA HABARI WAENDELEO MJINI DODOMA CHINI YA KAMATI YA BUNGE YA HUDUMA NA MAENDELEO YA JAMII.

musu1
Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii ikiendelea na majadiliano ya Muswada wa Sheria ya Huduma za Habari leo Oktoba 21,2016 Mjini Dodoma.
musu2
Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii Mhe. Peter Serukamba (kulia) akielezea  jambo kwa wajumbe wa Kamati yake na viongozi na watendaji wa Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo wakati wa majadiliano ya Muswada wa Sheria ya Huduma za Habari leo Oktoba 21,2016 Mjini Dodoma kushoto ni Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye
musu3
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye kushoto) akijibu hoja mbalimbali za wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii wakati wa majadiliano ya Muswada wa Sheria ya Huduma za Habari leo Oktoba 21,2016 Mjini Dodoma kulia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii Mhe. Peter Serukamba
musu4
Naibu Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Anastazia Wambura (katikati) akisisitiza jambo kwa  Kamati ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii wakati wa majadiliano ya Muswada wa Sheria ya Huduma za Habari leo Oktoba 21,2016 Mjini Dodoma.
musu5
Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri  ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt Tulia Ackson (kushoto) akifafanua jambo wakati wa majadiliano ya Muswada wa Sheria ya Huduma za Habari leo Oktoba 21,2016 Mjini Dodoma.
musu6 musu7
Katibu Mkuu Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Prof Elisante Ole Gabriel  akijibu hoja zilizotolewa na baadhi ya wajumbe ambao wanashiriki kuuchambua Muswada wa Sheria ya Huduma za Habari  leo Oktoba 21,2016 Mjini Dodoma.
musu8
Baadhi ya wajumbe wa Kamati ya Kudumu Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii wakifuatilia majadiliano na hoja mbalimbali katika kikao cha kuujadili  Muswada wa Sheria ya Huduma za Habari kinachoendelea Mjini Dodoma leo Oktoba 21,2016.
Picha zote na Idara ya Habari MAELEZO

JAJI KIONGOZI AWATAKA MAJAJI KUTENDA HAKI

Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania Mheshimiwa Ferdinand Wambali akifungua Mkutano wa Majaji Wafawidhi na Majaji waliosikiliza Kesi za Uchaguzi wa mwaka 2015 unaofanyika jijnini Arusha.
mkun1
Baadhi ya Waheshimiwa Majaji Wafawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania wakiwa kwenye Mkutano wa Kutathmini usikilizwaji wa kesi za uchaguzi unaofanyika jijini Arusha.
mkun2
Baadhi ya Waheshimiwa Majaji Wafawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania wakiwa kwenye Mkutano wa Kutathmini usikilizwaji wa kesi za uchaguzi unaofanyika jijini Arusha.
………………………………………………………….
Na Lydia Churi- Mahakama
Majaji wa Mahakama Kuu nchini wametakiwa kufanya kazi yao kwa kuzingatia maadili ya taaluma hiyo wakati wote kwa kuwa watanzania wanaitegemea Mahakama kuwatendea haki kwa sawa na kwa wakati.
Akifungua Mkutano wa Majaji Wafawidhi na Majaji waliosikiliza kesi za Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015 unaotathmini usikilizwaji wa kesi hizo leo jijini Arusha, Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania Mheshimiwa Ferdinand Wambali alisema watanzania wana imani na Mahakama hivyo ni muhimu kwa Majaji hao kutenda haki wakati wote.
Alisema Majaji hao wamekutana ili waweze kupata nafasi ya kujadili changamoto mbalimbali zilizojitokeza wakati wa kusikiliza kesi zilizohusu uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015 na kubadilishana mawazo namna ya kuzimaliza kwa haraka kesi zihusuzo uchaguzi kwa siku za mbeleni.
Alisema jumla ya kesi 53 za Ubunge zilizotokana na Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015 zilifunguliwa katika Mahakama Kuu kanda za Dar es salaam, Dodoma, Iringa, Mbeya, Moshi, Mtwara na Mwanza. Kanda nyingine ni Shinyanga, Songea, Sumbawanga, na Tanga.
Jaji Wambali alisema kati ya kesi hizo, kesi 31 zilimalizika katika hatua za awali na kesi 22 ziliendelea. Mpaka sasa kesi 19 zimemalizika. Aliongeza kuwa kesi tatu bado ziko mahakamani.
Jaji Wambali alisema ni jambo la kujivunia kwa Mahakama ya Tanzania kwa kuwa kesi zote 196 zilizotokana na uchaguzi wa madiwani zilimalizika mapema katika Mahakama  mbalimbali za Hakimu Mkazi nchini.
Alisema katika kipindi cha mwaka mmoja tangu kufanyika kwa uchaguzi Mkuu nchini, zaidi ya asilimia 94 ya kesi za uchaguzi zilizofunguliwa kwenye Mahakama Kuu zimemalizika wakati asilimia 100 ya kesi zote za udiwani zimemalizika.
Jaji Kiongozi amewapongeza Majaji na Mahakimu wote kwa kumaliza kesi kwa ufanisi na kwa wakati licha ya changamoto mbalimbali wanazozipitia Watumishi hao wa Mahakama wakati wanaposikiliza kesi zainazotokana na uchaguzi.
Aidha Jaji Kiongozi alishukuru shirika la Umoja wa Mataifa-UNDP kwa kufadhili mafunzo mbalimbali ya Majaji na Mahakaimu yaliyotolewa kabla na baada ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015. Mkutano wa siku nne wa Majaji Wafawidhi pamoja na Majaji waliosikiliza kesi za uchaguzi ulioanza leo jijini Arusha umefadhiliwa na shirika hilo.

Profesa Semboja: Wadau wa Habari toeni maoni yenu ili mboreshe Muswada wa Habari.

indexNa Daudi Manongi,MAELEZO.
Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Profesa Haji Semboja amewataka wamiliki na wadau wa tasnia ya habari hapa nchini kuusoma na kuelewa madhumuni ya Muswada wa Huduma za Habari kwa ajili kusaidia maoni ambayo yataboresha muswada huo.
Profesa Semboja asema hayo leo jijini Dar es salaam wakati wa mahojiano na mwandishi wa habari hizi.
Amesema ni vema wanahabari na wadau wa habari wakausoma kwa kina na kutoa maoni yao kwani hakuna sababu ya kuuchelewesha muswada huo kwa ajili ya kuimarisha tasnia ya habari.
Profesa Semboja ameipongeza Serikali kwa kuwa na uwazi katika kuuleta muswada huu kwa jamii ili wauone na kuulewa na waweze kutoa maoni yao ili tupate kitu kilicho bora.
Amesema kuwa baadhi ya maeneo yaliyomo katika muswada huo yatasaidia wanahabari kuboresha taaluma yao na kuwa na wanahabari wanaotambulika.
Profesa Semboja amewataka wana habari kuusoma vyema muswada huo na kuacha kuwa na mawazo hasi huku akisisitiza ushiriki wao uwe mkubwa kwani muswada huu unapatikana kwenye mitandao na hivyo unamfikia mtu yeyote kwa urahisi kabisa.
Muswada wa Vyombo vya Habari ulichapishwa na kuwekwa hadharani tangu Septemba 2016, pamoja na mambo mengi mazuri wadau wakuu wote walishiriki katika hatua za ndani za serikali kutoa maoni na kwa sasa wanashiriki katika hatua ya Kamati ya Bunge.