WADAU WATAKA SIKU YA MSANII IAZIMISHWE NCHI NZIMA
Wasanii
na wadau wa Sanaa wameomba kuwe na juhudi za halmashauri na mikoa yote
nchini kuunga mkono maazimisho ya siku ya msanii ambayo yamekuwa
yakiadhimishwa kila mwaka hapa nchini.
Wakizungumza
kwa nyakati tofauti kwenye tathmini ya maazimisho ya Siku ya Msanii
maarufu kama Msanii Day iliyofanyika mapema wiki hii ofisi za Baraza la
Sanaa la Taifa (BASATA) zilizoko Ilala Sharif Shamba wadau hao walieleza
kusikitishwa na siku hiyo muhimu kuadhimishwa mkoa wa Dar es Salaam
pekee huku wasanii wa mikoani wakiachwa nyuma.
“Tanzania
ina wasanii wengi, haiwezekani siku hii muhimu kwao iwe inagusa wasanii
wachache tu. Tunaamini halmashauri na mikoa ina nafasi kubwa ya
kuwaunganisha wasanii nchi nzima na kuunga mkono juhudi za Baraza katika
kuadhimisha siku hii” alisema Msanii wa Sanaa za Maonesho Nkwama
Ballanga.
Aliongeza
kuwa kupitia maafisa Utamaduni shughuli za Sanaa zimekuwa zikiendelea
maeneo mbalimbali nchini hivyo lazima kuwe na maelekezo maalum kutoka
Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) ya
kuwataka maafisa Utamaduni kuwaunganisha wasanii wote katika kuadhimisha
siku hii ambayo imekuwa ikiadhimishwa Dunia nzima huku kila nchi ikiwa
na namna yake ya kuadhimisha.
Tunajua
wasanii katika halmashauri zetu wanafanya kazi nzuri sana lakini pia
wana changamoto nyingi zinazowakabili. Kuunga mkono maadhimisho ya siku
yao nchi nzima ni kujenga mfumo wa wao kujipongeza, kujitathimi lakini
pia kuonesha kazi zao mbalimbali kulingana na fani zao” aliongeza
Ballanga.
Kwa
upande wake Msanii Ahmad Dadi wa Kundi la Sanaa za Maonesho la Lumumba
alisema kuwa siku ya Msanii ni muhimu katika kutambua na kuthamini
mchango wa wasanii mbalimbali nchini hivyo lazima kuwe na juhudi za
makusudi za kuifanya yenye kufana na yenye kumgusa kila Msanii nchini.
“Tuna
wasanii wakongwe ambao wamefanya kazi kubwa ya kuitangaza nchi. Hii
ndiyo fursa ya kuwaonesha wasanii wa kizazi cha sasa hali ya Sanaa
ilivyokuwa. Kuwepo kwa majukwaa ya maadhimisho kama haya nchi nzima
kutaonesha thamani ya Sanaa nay a wasanii” alisema Dadi.
Siku ya Msanii mwaka huu imepangwa kuazimishwa Oktoba 29 ambapo inatarajiwa kupambwa na shamrashamra mbalimbali
IMETOLEWA NA KITENGO CHA HABARI NA MAWASILIANO – BASATA
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni