HAYATOU AMPONGEZA RAVIA

Rais wa Shirikisho la Mpira wa
Miguu barani Afrika (CAF), Issa Hayatou amemtumia salamu za pongezi
Ravia Idarous Faina kwa kuchaguliwa kuwa Rais wa Chama cha Soka Zanzibar
(ZFA) mwishoni mwa juma lililomalizika.
Katika salamu zake, Hayatou
amesema kwa niaba ya CAF, Kamati ya Utendaji na yeye binafsi
wanampongeza kwa kuchaguliwa kuwa Rais wa Chama cha Mpira wa Miguu
Zanzibar (ZFA).
CAF wanaimani na uzoefu wa Ravia katika uongozi, kuwa ataendeleza uongozi bora kwa faida ya maendeleo ya soka visiwani Zanzibar.
Aidha Hayatou amewatumia pia salamu za pongezi, Mzee Zam Ali na Ali Mohamed kwa kuchgauliwa kuwa makamu wapya wa Rais wa ZFA.
Hayatou amewatakia mafanikio mema
katika nafasi mpya hizo walizochaguliwa na kuahidi CAF itaendelea
kuwapa ushirikiano wa maendeleo ya mpira wa miguu visiwani Zanzibar.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni