Jumatatu, 17 Oktoba 2016

MHE. KAIRUKI AWAHIMIZA WATUMISHI WA UMMA MKOANI MWANZA KUJISAJILI VITAMBULISHO VYA TAIFA KABLA YA MUDA KWISHA


jam1
Afisa Usajili wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa Mkoa wa Mwanza Bw. Daud Hashimu Abdallah akiwasilisha taarifa ya usajili wa watumishi wa umma  kwa ajili ya kupatiwa Vitambulisho vya Taifa kwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimeti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Angellah J. Kairuki  (hayupo pichani)  wakati wa ziara ya  kikazi  ya waziri huyo  mkoani  Mwanza kwa ajili ya kukagua na kufanya tathmini ya zoezi la usajili wa watumishi  wa umma ili kupata Vitambulisho vya Taifa.
jam2
Mkurugenzi wa Halimashauri ya Wilaya Misungwi Bw. Eliurd L. Mwaiteleke (kulia) akimuongoza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimeti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Angellah J. Kairuki (katikati) kwenda katika moja ya kituo cha kusajili watumishi wa umma kwa ajili ya kupatiwa Vitambulisho vya Taifa wakati wa ziara ya waziri huyo ili kuona namna zoezi hilo linavyoendeshwa katika Halimashauri ya Wilaya Misungwi.
jam3
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimeti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Angellah J. Kairuki akipewa ufafanuzi  na Afisa Usajili wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa wa Halimashauri ya Wilaya Misungwi Bw. Abbasi Iwodya (kulia) juu ya taarifa zinazowasilishwa na watumishi wa umma kwa ajili ya  kupatiwa Vitambulisho vya Taifa wakati wa ziara ya  kikazi  ya waziri huyo  aliyoifanya katika Halimashauri ya Wilaya Misungwi.
jam4
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimeti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Angellah J. Kairuki (Mb) akizungumza na mmoja wa watumishi  aliyekuwa akijisajili  kwa ajili ya kupata Kitambulisho cha Taifa wakati wa ziara ya waziri huyo ya kukagua na kufanya tathmini ya zoezi hilo katika Halimashauri ya Wilaya Misungwi.
jam5
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimeti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Angellah J. Kairuki (Mb) akikagua viambatanisho vya malalamiko yaliyowasilishwa na mmoja wa watumishi wa Halimashauri ya Wilaya Misungwi wakati wa ziara ya  kikazi  ya waziri huyo  aliyoifanya katika Halimashauri hiyo ili kukagua na kufanya tathmini ya zoezi la usajili wa watumishi wa umma  kwa ajili ya kupatiwa Vitambulisho vya Taifa mkoani Mwanza.
jam6
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimeti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Angellah J. Kairuki (Mb) akipokea malalamiko ya mtumishi wa Halimashauri ya Wilaya Misungwi wakati wa ziara ya  kikazi  ya waziri huyo  aliyoifanya katika Halimashauri hiyo ili kukagua na kufanya tathmini ya zoezi la usajili wa watumishi wa umma  kwa ajili ya kupatiwa Vitambulisho vya Taifa mkoani Mwanza.
jam7
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimeti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Angellah J. Kairuki (Mb) akizungumza na watumishi wa Halimashauri ya Wilaya Misungwi wakati wa ziara ya  kikazi  ya waziri huyo  aliyoifanya katika Halimashauri hiyo ili kukagua na kufanya tathmini ya zoezi la usajili wa watumishi wa umma  kwa ajili ya kupatiwa Vitambulisho vya Taifa mkoani Mwanza.
jam8
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimeti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Angellah J. Kairuki (Mb) akishuhudia mtumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ilemela akisajiliwa  kwa ajili ya kupata Kitambulisho cha Taifa wakati wa ziara ya waziri huyo ya kukagua na kufanya tathmini ya zoezi hilo katika Halimashauri hiyo.
jam9
Baadhi ya watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Nyamagana waliojitokeza kwa ajili ya kujisajili ili kupata Vitambulisho vya Taifa wakimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimeti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Angellah J. Kairuki (Mb) (hayupo pichani) wakati wa ziara ya kikazi ya waziri huyo aliyoifanya katika Halmashauri hiyo ili kukagua na kufanya tathmini ya zoezi hilo.
jam10
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimeti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Angellah J. Kairuki (Mb) akishuhudia usajili wa watumishi wa umma wa Halmashauri ya Wilaya ya Nyamagana kwa ajili ya kupata Vitambulisho vya Taifa wakati wa ziara ya kikazi ya waziri huyo aliyoifanya katika Halmashauri hiyo ili kukagua na kufanya tathmini ya zoezi hilo.
jam12
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimeti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Angellah J. Kairuki (Mb) akisisitiza juu ya ukamilishaji wa zoezi la usajili wa watumishi wa umma mkoani Mwanza wakati wa ziara ya kikazi ya waziri huyo mkoani humo, aliyoifanya kwa lengo  la kufanya tathmini ya zoezi hilo . Kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Bw. John Mongella akimsikiliza.

NHIF endelezeni huduma za upimaji afya- Wananchi


if1
Meneja wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Mkoa wa Shinyanga na Simiyu Bw. Imanuel Amani akitoa elimu kwa mwananchi mkoani Simiyu aliyefika katika banda la Mfuko kujua namna ya kujiunga.
if2
Wananchi mbalimbali wakiendelea kuhudumiwa katika banda la Mfuko lililotoa huduma za upimaji wa afya bure katika maadhimisho ya wiki ya Vijana mkoani Simiyu.
if3
Ofisa Masoko na Elimu kwa Umma, Grace Michael akitoa huduma ya uelimishaji wa wananchi waliotembelea banda la Mfuko.
if4
Huduma za upimaji zikiendelea.
if5
Taifa wa Bima ya Afya Mkoa wa Shinyanga na Simiyu Bw. Imanuel Amani akizungumza na wananchi waliofika kupata huduma za upimaji.
if6
Wananchi walifurika katika banda la Mfuko kwa lengo la kupata huduma.
if7
Wananchi wakijiandikisha kupata huduma.
………………………………………………………..
Na Mwandishi Wetu, Simiyu
WANANCHI wa Mkoa wa Simiyu wameuomba Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya kuendelea kutoa huduma ya upimaji wa afya bure katika maeneo ya vijijini ili wananchi walioko huko wanufaike nazo.
Rai hiyo waliitoa mwishoni mwa wiki iliyopita katika kilele cha Maadhimisho ya wiki ya Vijana iliyofanyika mkoani humo ambapo Mfuko ulitoa huduma za upimaji wa afya zikiambatana na uhamasishaji wa wananchi kujiunga na huduma zake.
“Kama unavyoona wananchi walivyojaa hapa kupata huduma za upimaji…hii ni ishara kwamba huduma hizi zinatakiwa zaidi hasa huko vijijini ambako fursa kama hizi imekuwa ni ngumu kuzipata hivyo Mfuko uangalie namna ya kuendelea kutuletea hii huduma,” alisema Mkazi wa Bariadi Bw. Masunga Maduhu.
Hata hivyo walipongeza kitendo kilichofanywa na Mfuko cha kutoa huduma katika maadhimisho hayo ambayo imesaidia wananchi wengi zaidi kutambua hali ya afya zao lakini pia wamenufaika na elimu kutoka kwa wataalam ya namna ya kuepukana na maradhi yasiyoambukiza.
Mfuko ulitoa huduma za vipimo vya shinikizo la damu, kiwango cha sukari, uzito na urefu ambapo jumla ya wananchi 1,311 walipata huduma ya upimaji wa afya. Kati ya wananchi hao 175 walionekana kuwa na matatizo ya uzito, wananchi 30 matatizo ya sukari na wananchi 43 matatizo ya shinikizo la damu.
Kwa upande wake Meneja wa NHIF Mkoa wa Shinyanga na Simiyu Bw. Imanuel Amani alisema kuwa huduma za upimaji hufanywa mara kwa mara katika maeneo mbalimbali hivyo akawaomba wananchi wanapokutana na fursa kama hizo wazitumie.
“NHIF tuna mpango wa elimu ya Kata kwa Kata ambayo mbali na uhamasishaji huwa tunatoa huduma za upimaji wa afya hivyo Mfuko umetoa kipaumbele kikubwa katika suala hili,” alisema.

WAZIRI MKUU ACHOSHWA NA MADUDU BODI YA KOROSHO


kimo1
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ahutubia wananchi wa wilaya ya Nachingwea katika kiwanja cha Sokoine waziri mkuu alipokea malalamiko kutoka kwa wananchi kuhusiana na biashara ya korosho  Ikamlazimu waziri mkuu kumuagiaza Waziri wa kilimo afanye mapitio makini kweznye bodi nzima ya korosho
kimo2 kimo3
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa apokea hundi ya mfano ya zaidi  shilingi milioni kumi nasita kutoka kwa Mkuu wa Mkoa walindi kwa ajili ya Rambirambi kwa wananchi wa mkoa wa Kagera kulia kwa waziri mkuu ni mkewe Mary Majaliwa  waziri mkuu yupo mkoani Lindi katika ziara ya kikazi katika wilaya ya Nachingwea na Ruwangwa  
Picha na Chris Mfinanga
………………………………………………………………………………………………..
*Aagiza ifanyiwe marekebisho makubwa
*Aishangaa kung’ang’ania minada
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amemuagiza Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Dk Charles Tizeba kuifanyia marekebisho makubwa Bodi ya Korosho na menejimenti yake  baada ya kushindwa kusimamia zao hilo ipasavyo.
Amesema Serikali itafanya mapitio ya bodi zote za mazao ya biashara na imeanza na zao la korosho kisha zao la pamba, tumbaku, kahawa, katani na chai. Katika tathmini na mapitio hayo , bodi itakayobainika kushindwa kutekeleza majukumu yake itavunjwa.
Waziri Mkuu alitoa agizo hilo jana jioni (Jumapili, Oktoba 16, 2016) wakati akihutubia wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye uwanja cha Sokoine wilayani Nachingwea mkoani Lindi.
Alisema anaishangaa bodi hiyo kuacha kutekeleza majukumu yake na kuingilia minada ya korosho na kuzuia baadhi ya wafanyabiashara wasiweze kununua zao hilo hali inayoashiria kuwepo kwa watu waliopangwa kununua bila ya kufuata utaratibu.
“Bodi leo wamejipa jukumu la kusimamia minada ! sio kazi yao ni kazi ya chama kikuu, zao la korosho linalimwa kutoka mkoani Ruvuma hadi Tanga, mtasimamia minada mingapi viachieni vyama vikuu. Vyama vikuu vikiharibu walalamikaji waje kwenu kama sehemu ya rufaa. Sasa nyinyi mnasimamia minada mnaharibu walalamikaji watakwenda kwa nani  ?  kwa nini mng’ang’anie kwenda kwenye minada,” alihoji Waziri Mkuu.
Waziri Mkuu alisema Ijumaa (Oktoba 14,2016) bodi hiyo  ilisitisha mnada wa korosho Lindi kwa sababu wanunuzi hawakuweka bondi (dhamana ya mauzo) na alishatoa maagizo ya kuwataka wanunuzi wasiruhusiwe kununua hadi waweke asilimia 25 ya malipo.
Alisema maagizo hayo aliyatoa tangu mwezi Aprili ila  watendaji wa bodi hiyo hawakuyafanyia kazi kwa wakati na badala yake waliwazuia wafanyabiashara waliotaka kununua korosho Lindi kwa madai ya kutokuwa na bondi huku wakiwaruhusu wa Mtwara.
“Kama kule walinunua bila bondi kwa nini wasiwaruhusu na Lindi wakanunua bila  bondi ili nijue kwamba mliamua kugoma kuteleza maelekezo ya Serikali? Au hamkumtaka aliyeshinda  nyie  mlikuwa mnamtaka nani nitashughulika na nyie,” alisisitiza.
Aliongeza kuwa “Nimesema tukitoa maelekezo lazima yatekelezwe na atakayeshindwa hatufai, Mheshimiwa mbunge umelalamika juu ya bodi hawa ndio wabeba maelekezo hatujawahi kuona bodi ya korosho ikienda vijijini kuzungumza na vyama vikuu hata mara moja,”.
Akizungumzia kuhusu suala la wakulima kulazimishwa kufungua akaunti  za kupitishia malipo yao alisema wasiwalazimishe.“Waelimisheni wakulima umuhimu wa kufungua akaunti lakini si kwa kuwalazimisha wote wawe na akaunti hadi yule mwenye kilo tano…na akaunti yenyewe inafunguliwa kwa sh. 100,000,” alisema.
Alisema “’wanashindwa kutekeleza niliyowaagiza, halafu wanasingizia utendaji wao mbovu kuwa ndio maagizo yangu,’ niliwaagiza wapi,” alihoji na kuongeza kuwa  “yapo makundi yanafanya mambo yanavyotaka alafu yakiwazidi mambo wanasingizia viongozi wajuu na ndio wale wanaosema kila kitu nimeagizwa kutoka juu, juu wapi?
“Lazima tuendelee kudhibiti nidhamu ya vyombo vya tunavyoviunda kwa ajili ya kuwahudumia wananchi. Tutaendelea kusimamia nidhamu kwa taasisi zinazowahudumia wakulima nchi nzima,” alisisitiza.
Wakati huo huo Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Bw. Godfrey Zambi alimkabidhi Waziri Mkuu msaada wa sh. milioni 16.3 pamoja na nguo kwa ajili ya kusaidia  wananchi walioathirika na tetemeko la ardhi lililotokea mkoani Kagera Jumamosi, Septemba 10, mwaka huu na kusababisha vifo vya watu 17 na wengine 440 walijeruhiwa.

WATANZANIA WATAKIWA KUTUMIA MABARAZA YA ARDHImaba1

Kaimu Msajili wa Mabaraza ya Ardhi na Nyumba ya Wilaya, Bibi. Amina Rashid Ntibampemba akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mafanikio ya Mabaraza hayo leo Jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mboza Lwandiko.
maba2
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini kutoka Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Bi. Mboza Lwandiko akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu hali ya Mabaraza ya Ardhi na Nyumba ya wilaya leo Jijini Dar es Salaam.
………………………………………………………..
Na Georgina Misama – MAELEZO
Wizara ya Ardhi, Nyumba naMaendeleo ya Makazi imewataka watanzania kutumia Mabaraza ya Ardhi na Nyumba ya Wilaya  katika kutatua matatizo mbalimbali yanayohusu Nyumba na Makazi.
Hayo yamesemwa leo na Kaimu Msajili Mabaraza ya Ardhi na Nyumba ya Wilaya Bi Amina Rashidi wakati akiongea na waandishi wa habari katika ukumbi wa Idara ya habari Maelezo.
“Mabaraza ya Ardhi na Nyumba ndiyo chombo pekee kilichoundwa kwa ajili ya kutatua matatizo yote yanayohusu ardhi na nyumba” alisema Amina.
Akitaja baadhi ya mashauri yanayosikilizwa kwenye Mabaraza hayo Amina alisema mashauri yanayotokana na milki pandikizi (double allocation) au mashauri ya wananchi wanaopakana kwa mmoja wao kutaka kujipanulia eneo. Yapo pia mashauri ya wenye nyumba na wapangaji yanayofunguliwa kwa kukiukwa kwa mikataba.
Aidha, Amina alifafanua kwamba uendeshaji wa mashauri katika Mabaraza ya Ardhi na Nyumba ni wakirafiki nasio unaofuata taratibu za Mahakama za kawaida. Wajumbe wa Baraza wanatoka miongoni mwa wanajamii wa eneo ambalo Baraza limeundwa.
Nae Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini kutoka Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya makazi  Bi. Mboza Lwandiko alitolea ufafanuzi wa dhamira ya wizara yake katika kuhakikisha inapambana na ongezeko la mashauri kwa kuunda Mabaraza mapya yapatayo 20 kila mwaka.
“Katika mwaka wa fedha 2016/2017 Wizara itakamilisha taratibu za kuunda Mabaraza(44) kati ya Mabaraza mapya 47 yaliyoundwa na tangazo la serikali la mwezi Aprili, 2016” alisema Mboza.
Tayari takribani mashauri elfu 43 yamesikilizwa kati ya mashauri elfu 59 yaliyofunguliwa kwa kipindi cha kuanzia Oktoba 2004 na Septemba 2016.

OMEGA MINISTRY CHURCH OF ALL NATIONS YAANDAA SEMINA YAKUOMBEA TAIFA


omi1
Nabii Samson Rolinga wa Kanisa la Omega Ministry akizungumza na waandishi wa habari kuhusu Semina ya kuliombea taifa leo Jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mchungaji Samson Shango Donalds wa Kanisa la Ukombozi Missions Kanda ya Ziwa.
omi2
Mchungaji Samson Shango Donalds wa Kanisa la Ukombozi Missions Kanda ya Ziwa akizungumza na waandishi wa habari kuhusu Semina ya kuliombea taifa leo Jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Nabii Samson Rolinga wa Kanisa la Omega Ministry.
…………………………………………………………..
Lilian Lundo, MAELEZO.
KANISA la Omega Ministry of All Nations lenye makao yake Makuu Mbezi Afrikana, Jijini Dar es Salaam limeandaa Semina ya Injili ya Neno la Mungu la kuiombea Taifa na Viongozi wa Nchi, inayotarajiwa kufanyika Urafiki Nyangumi Jijini Dar es Salam Octoba 21 mpaka 23 mwaka huu.
Nabii Samson Rolinga ameyasema hayo leo Jijini Dar es Salaam alipokuwa akiongea na waandishi wa habari kuhusu Semina hiyo yenye lengo la kuiombea Taifa, Viongozi wa Nchi na kuwafungua watu katika vifungo mbalimbali.
“TutaliombeaTaifa lirudi katika misingi ya Mungu, vile vile tutawaombea watu waliofungwa na nguvu za giza na magonjwa kama vile kanda, ukimwi na utasa,” alifafanua Nabii Rolinga.
Amesema magonjwa yapo lakini pia yapo magonjwa ambayo yanatengenezwa na watu ilikumdhoofisha mtu, hivyo katika semina hiyo kutafanyika maombi ya kuombea magonjwa hayo pamoja na matatizo yote yanayotokonana roho za kurithi.
Vile vile amesema kuwa kumekuwa na matatizo mengi sana ambayo watu hawana majibu ya matatizo hayo mfano vijana wengi kutokuwa na kazi na kukata tama huku wakijraribu kupambana na matatizo hayo kwa njia ya mwili.
Nabii Rolinga amesema kuwa lengo lake nikuonyesha chanzo cha matatizo na kuyatatua kwa njia ya maombi pamoja na kueleza namna ufalme wa giza unavyofanya kazi.
Kwa upande wake Nabii Donald kutoka Mwanza amesema kuwa atakuwepo katika semina hiyo ambayo itashughulikia matatizo ya Roho, kuvunja yanayoonekana katika ulimwengu wa Roho pamoja na kuombea nchi na Utawala wa nchi.
Aidha amesema kuwa watumishi wa Mungu wana jukumu kubwa la kuwaombea Viongozi wa Nchi na Rais ili Mungu awasimamie katika majukumu yao ya kila siku ya kuliongozaTaifa.

SOMA JARIDA LA WIZARA YA HABARI KATIKA LINK ILIYOPO CHINI

jari1 jari2

DKT. CHARLES MWIJAGE AITAKA NBS KWA KUSHIRIKIANA NA WADAU WA MAENDELEO KUFANYA TAFITI YA VIWANDA VIDOGO NCHINI


nba1
Baadhi ya Maafisa Wandamizi wa Serikali kutoka Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, na Ofisi ya Taifa ya Takwimu wakifuatilia mada mbalimbali zilizokuwa zikiwakilishwa wakati wa uzinduzi matokeo ya sensa ya uzalishaji viwandani ya mwaka 2013 leo Oktoba 17, 2016 Jijjini Dar es Salaam.
nba2
Baadhi ya wawakilishi kutoka taasisi mbalimbali nchini wakifuatilia mada mbalimbali zilizokuwa zikiwakilishwa wakati wa uzinduzi matokeo ya sensa ya uzalishaji viwandani ya mwaka 2013 leo Oktoba 17, 2016 Jijjini Dar es Salaam.
nba3
Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Dkt. Adelhelm Meru akizungumza wakati wa uzinduzi wa matokeo ya sensa ya uzalishaji viwandani ya mwaka 2013 leo Oktoba 17, 2016 Jijjini Dar es Salaam.
nba4
Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Dkt. Charles Mwijage (katikati) akifuatilia mada mbalimbali zilizowasilishwa na wadau mbalimbali wakati uzinduzi wa matokeo ya sensa ya uzalishaji viwandani ya mwaka 2013 leo Oktoba 17, 2016 Jijjini Dar es Salaam. Wengine katika picha kutoka kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu, Dkt. Albina Chuwa
nba5
Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Dkt. Charles Mwijage (kulia) akiteta jambo na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Dkt. Adelhelm Meru wakati wa uzinduzi wa matokeo ya sensa ya uzalishaji viwandani ya mwaka 2013 leo Oktoba 17, 2016 Jijjini Dar es Salaam.
nba6
Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Dkt. Charles Mwijage akizungumza na wadau mbalimbali wa maendeleo na Viongozi waandamizi wa Serikali wakati wa uzinduzi wa matokeo ya sensa ya uzalishaji viwandani ya mwaka 2013 leo Oktoba 17, 2016 Jijjini Dar es Salaam.
nba7
Baadhi ya Maafisa Wandamizi wa Serikali kutoka Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, na Ofisi ya Taifa ya Takwimu wakifuatilia mada mbalimbali zilizokuwa zikiwakilishwa wakati wa uzinduzi matokeo ya sensa ya uzalishaji viwandani ya mwaka 2013 leo Oktoba 17, 2016 Jijjini Dar es Salaam.
nba8
wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Dkt. Charles Mwijage akiwa ameshika vitabu mbalimnbali vya taarifa ya utafiti kuhusu matokeo ya sensa ya uzalishaji viwandani ya mwaka 2013 leo Oktoba 17, 2016 Jijjini Dar es Salaam.
nba9
Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Dkt. Charles Mwijage (kushoto) akimkabidhi taarifa ya kitabu cha utafiti kuhusu matokeo ya sensa ya uzalishaji viwandani ya mwaka 2013 kwa Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia viwanda (UNIDO), Gerald Runyoro leo Oktoba 17, 2016 Jijjini Dar es Salaam
(PICHA NA ISMAIL NGAYONGA- MAELEZO)
……………………………………………………..
Na Beatrice Lyimo
MAELEZO-Dar es Salaam
SERIKALI imeitaka Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) kwa kushrikiana na wadau wa maendeleo nchini ikiwemo Shirika la Maendeleo ya Viwanda Duniani (UNIDO) na Shirikisho la Viwanda Nchini (CTI) kuendelea kufanya utafiti ili kubaini idadi na maendeleo ya viwanda vidogo vilivyopo nchini.
Hayo yamesemwa leo Jijini NA Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Dkt Charles Mwijage wakati wa uzinduzi wa matokeo ya Sensa ya Uzalishaji bidhaa Viwandani mwaka 2013.
Dkt Mwijage alisema kuwa katika mataifa yanayoendelea duniani ikiwemo Korea Kusini, Malaysia na Singapore uchumi wa nchi hizo umeweza kukua kwa kiwango kwa juu zaidi kutokana na kuweka mkazo katika kuendeleza viwanda vidogo na vya kati.
Alisema katika kuharakisha kasi ya maendeleo ya vidogo yanapatikana nchini, Wizara yake imekusudia kuwajengea hamasa Watanzania kupendelea kujenga viwanda vidogo vidogo na vya kati, kwani kukua kwa sekta ya viwanda nchini kutaisaidia kuinua uchumi wan chi.
“Asilimia 25- 40 ya mazao ya kilimo yanayovunwa huharibika kabla ya kufikishwa kiwandani, katika kukabiliana na hali hiyo Serikali imekusudia kujenga viwanda vidogo vidogo ili kuwawezesha wakulima wapate sehemu nzuri zaidi za kuhifadhi mazao yao” alisema Mwijage.
Aidha, Dkt Mwijage alisema, sekta ya viwanda vidogo vidogo nchini imeendelea kukua kwa kasi nchini ambapo hadi sasa kuna jumla ya viwanda 3800 vilivyoanzishwa nchini kuanzia Novemba 2015 hadi octoba, 2016.
Katika hatua hiyo Dkt Mwijage alisema kuwa Wizara yake inaendelea kuhamasisha Sekta binafsi kuwekeza katika Sekta ya viwanda vidogo, vya kati na vikubwa ikiwa jukumu kuu la Serikali ni kuhakikisha nchi inakuwa salama na inajenga mazingira wezeshi kwenye sekta binafsi kuzalisha na kufanya biashara.
Naye Mkurugenzi Mkuu Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) Dkt Albina Chuwa alisema kuwa matokeo hayo yanaonyesha mafanikio katika sekta ya viwanda ikiwemo kuongezeka kwa ajira zipatazo 264,223 nchini na kuchangia uchumi kwa takribani Shilingi bilioni 8.0 kwa mwaka 2013.
Alisema kuwa Takwimu za matokeo ya sense ya uzalishaji viwandani ni rasmi na kuwataka watunga sera, wanasiasa, viongozi, sekta binafsi na watu binafsi kutumia  matokeo hayo kwa lengo la kuboresha Sekta ya viwanda nchini.