Jumatano, 1 Juni 2016

DKT SHEIN KUZUNGUMZA NA MABALOZI WILAYA MJINI LEO

zan11 
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dkt.Ali Mohamed Shein akizungumza na wanachama cha Mapinduzi CCM Wilaya ya Mjini Mkoa wa Mjini Kichama,  wakati alipokua akiwapongeza wanachama hao baada ya ushindi wa Uchaguzi marudio uliomalizika mwezi wa Machi mwaka huu,mkutano ulifanyika leo katika ukumbi wa CCM Mkoa Amani,[Picha na Ikulu.] 01/06/2016.
zan12 
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dkt.Ali Mohamed Shein akizungumza na wanachama cha Mapinduzi CCM Wilaya ya Mjini Mkoa wa Mjini Kichama,  wakati alipokua akiwapongeza wanachama hao baada ya ushindi wa Uchaguzi marudio uliomalizika mwezi wa Machi mwaka huu,mkutano ulifanyika leo katika ukumbi wa CCM Mkoa Amani,[Picha na Ikulu.] 01/06/2016.
zan1zan2Wanachama cha Mapinduzi wa Wilaya ya Mjini Mkoa wa Mjini Kichama,wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dkt.Ali Mohamed Shein,wakati alipokua akiwapongeza wanachama hao baada ya ushindi wa Uchaguzi marudio uliomalizika mwezi wa Machi mwaka huu,katika mkutano ulifanyika leo katika ukumbi wa CCM Mkoa Amani,[Picha na Ikulu.] 01/06/2016.
zan3 
Katibu wa CCM Wilaya ya Mjini Kichana Bi,Fatuma Shomari Juma alipokuwa akisoma risala ya Chama Wilaya ya Mjini Kichama wakati wa mkutano wa kuwashukuru na kuwapongeza wanachama cha Mapinduzi Wilaya hiyo uliofanywa leo na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dkt.Ali Mohamed Shein,katika ukumbi wa CCM Mkoa Amani, [Picha na Ikulu.] 01/06/2016
zan6Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Mjini Kichama Bw. Juma Fakih Choum akiwasalimia wanachama cha mapinduzi waialaya hiyo wakati wa mkutano wa kuwashukuru na kuwapongeza wanachama cha Mapinduzi Wilaya hiyo uliofanyika leo katika ukumbi wa CCM Mkoa Amani na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dkt.Ali Mohamed Shein, [Picha na Ikulu.] 01/06/2016.
zan7 
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dkt.Ali Mohamed Shein akiteta jambo na Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Mjini Kichama Bw. Juma Fakih Choum  wakati wa mkutano wa kuwashukuru na kuwapongeza wanachama cha Mapinduzi Wilaya hiyo uliofanyika leo katika ukumbi wa CCM Mkoa Amani, [Picha na Ikulu.] 01/06/2016.
zan8Mwanachama cha Mapinduzi wa Wilaya ya Mjini Mkoa wa Mjini Kichama Bi.Rukia Omar kutoka    jimbo la Kikwajuni alipokuwa akitoa mchango wake wakati Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dkt.Ali Mohamed Shein,alipowapongeza na kuwashukuru Wanachama hao baada ya ushindi wa Uchaguzi marudio uliomalizika mwezi wa Machi mwaka huu,katika mkutano ulifanyika leo katika ukumbi wa CCM Mkoa Amani,[Picha na Ikulu.] 01/06/2016.
zan9Mwanachama cha Mapinduzi wa umoja wa Vijana UVCCM Ashrak Saleh Zingo katika shehia ya kiponda mji Mkongwe wa Zanzibar alipokuwa akitoa mchango wake uliogusia zaidi uvunywaji wa katiba ya Zanzibar unaofanywa na Wanachama cha Upinzania,mchango huo aliuotoa leo katika ukumbi wa CCM Mkoa Amani wakati wa Mkutano wa Kuwashukuru Viongozi wa Mashina,wenyeviyi wa Matawi na Maskani uliofanywa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dkt.Ali Mohamed Shein, [Picha na Ikulu.] 01/06/2016.
zan10Wanachama cha Mapinduzi wa Wilaya ya Mjini Mkoa wa Mjini Kichama,wakinyoosha mikono juu kuunga mkono hotuba ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dkt.Ali Mohamed Shein,wakati alipokua akiwashukuru kuwapongeza wanachama hao baada ya ushindi wa Uchaguzi marudio uliomalizika mwezi wa Machi mwaka huu,katika mkutano ulifanyika leo katika ukumbi wa CCM Mkoa Amani,[Picha na Ikulu.] 01/06/20

Tatizo la hewa ya Ukaa kupungua hapa nchini.

By Newsroom on June 1, 2016
nyu 
Frank Mvungi-Maelezo
Wakala wa Taifa wa Utafiti wa Nyumba Bora na Vifaa vya Ujenzi (NHBRA) umeanza kufanya utafiti utakaosadia kupunguza kiwango cha Hewa ya Ukaa (green house gases) kinachozalishwa  kutokana na shughuli za ujenzi ili  kupunguza uharibifu wa mazingira.
Akizungumza na Waandishi wa Habari leo jijini Dar es salaam Mhandisi Heri Hatibu kutoka wakala huo amesema utafiti utasaidia kupunguza gharama za Ujenzi hapa nchini.
Akizungumzia Malengo ya Utafiti huo Hatibu amesema kuwa, utasaidia kupunguza kiwango cha nishati kinachotumiwa kwenye nyumba kwa ajili ya kupooza hewa hivyo kuokoa fedha inayoweza kutumika kufanya mambo mengine.
“Sekta ya Ujenzi inachangia asilimia 40 ya hewa ya ukaa hivyo lengo la utafiti huu ni kusaidia kuondoa tatizo hili mara baada ya utafiti wetu kukamilika.” Alisisitiza Mhandisi Hatibu.
Aidha Hatibu amesema kuwa, utafiti huo utawezesha kusanifu majengo yatakayotumia nishati kidogo kwenye hatua ya ujenzi na hata wakati wa matumizi ya majengo husika. Pia utachochea matumizi ya vifaa vya Ujenzi vinavyopatikana katika maeneo ya karibu na shughuli za ujenzi.
Pia utafiti huo utasaidi kutoa elimu kwa wadau wa ujenzi kuhusu nishati mbadala katika kutekeleza shughuli za ujenzi, ikiwemo kuacha kukata miti.
Vile vile wananchi wataelimishwa kuhusu njia bora za uchomaji wa matofali ili waweze kutumia vifaa vingine badala ya kukata miti kwa ajili ya uchomaji matofali.
Matokeo ya utafiti huo unaotarajiwa kukamilika kabla ya mwisho wa mwaka huu yatasaidia wadau wa sekta hii kupanga mipango ya ujenzi itakayosaidia kupunguza athari katika mazingira zinazosababishwa na matumizi makubwa katika uzalishaji vifaa vya ujenzi na hata katika ujenzi.Utafiti huo unafanyika katika Mikoa ya Dar es salaam, Dodoma, Morogoro na Tanga.

TAARIFA KUTOKA CHAMA CHA WAANDISHI WA HABARI ZA MICHEZO (TASWA)

index
 
KAMATI ya Utendaji ya Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo Tanzania (TASWA) imemteua Makamu Mwenyekiti wa TASWA, ambaye pia Mhadhiri Msaidizi wa Shule Kuu ya Uandishi wa Habari na Mawasiliano kwa Umma (SJMC) ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Egbert Mkoko kuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Tuzo za Wanamichezo Bora Tanzania mwaka 2015/2016.
 
Pia TASWA imeteua wajumbe tisa wa kamati hiyo. Majina yao na vyombo vyao katika mabano ni Mahmoud Zubeiry (Bin Zubeiry Sports- Online), Jane John (TBC), Baruani Muhuza (Azam Media), Limonga Justine (Redio Uhuru), Maulid Kitenge (E-FM Redio), Deogratias Rweyunga (Redio One/ITV), Shaffih Dauda (Clouds Media), Asha Muhaji (Bingwa) na Nelly Mtema (Daily News).
 
Kamati inaweza kuongeza wajumbe wengine au kupunguza kwa kadri itakavyoona inafaa. Utaratibu wa kuizindua kamati hiyo unaandaliwa na sekreterieti ya TASWA. Jukumu la kamati itakuwa ni kuandaa utaratibu wa kuwapata wanamichezo watakaowania tuzo hiyo na pia kuteua washindi kwa kila mchezo.
 
Tuzo za Wanamichezo Bora zinazotolewa kila mwaka na TASWA zimepangwa kufanyika Agosti 26, mwaka huu, Dar es Salaam zikihusisha michezo mbalimbali.
 
B; ZIARA YA MAFUNZO NAIROBI
 
TASWA kwa kushirikiana na Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo Kenya, vimeanzisha program ya ziara ya mafunzo na kubadilishana uzoefu baina ya vyama hivyo viwili, ikiwa katika makundi tofauti ya wahariri/waandishi waandamizi na kundi lingine la waandishi wa habari chipukizi.
 
Kwa kuanzia wahariri wa habari za michezo 18 au wale wenye uzoefu katika uandishi usiopungua miaka kumi kutoka vyombo mbalimbali vya habari nchini wataenda Nairobi kwa ziara ya mafunzo kuanzia Julai 6-9 mwaka huu.
Tunaamini wakirudi wataendelea kuwa waalimu wazuri kwa wale chipukizi, ambao nao watapata fursa kama hiyo siku za usoni.
Ahsanteni,
Amir Mhando
Katibu Mkuu TASWA
01/06/2016

Hifadhi ya Selous yapoteza asilimia 90 ya Tembo wake


Hifadhi ya Taifa ya  wanyamapori ya Selous iliyopo kusini mwa Tanzania imepoteza asilimia  90 ya Tembo waliopo katika hifadhi hiyo kutokana na ujangili uliokithiri.
Ripoti ya mfuko wa hifadhi ya wanyapori na mazingira duniani (WWF) imesema kufikia mwaka 2022 kama hakutakuwa na hatua zozote kali zitakazochukuliwa kuwalinda tembo kutokana na ujangili  basi  watatoweka kabisa.
Ripoti hiyo imeendelea kusema kuwa kwa miaka ya nyuma mbuga ya Selous ilikuwa mojawapo ya mbuga kubwa kabisa katika bara la afrika yenye tembo wengi ambapo kulikuwa na tembo zaidi ya 110000 lakini kutokana na ujangili uliokithiri katika miaka 40 iliyopita tembo hao wamepungua na kubakia 15000 tu uku mahitaji makubwa ya pembe za ndovu katika nchi ya china yakitajwa na ripoti hiyo kuwa kichocheo kikubwa cha ujangili na mauaji ya idadi kubwa ya tembo hao.
Aidha ripoti hiyo inaonyesha hathari kubwa  kiuchumi itakayotokea  kutokana na kwamba Tanzania kupitia Mbuga ya Selous inaingiza dola milioni 6 kwa mwaka ikilinganishwa na Sekta ya Viwanda inayochangia dola bilioni 5 katika pato la Taifa.
Pamoja na Hayo Serikali ya awamu ya tano  kupitia Wizara ya Maliasili na Utalii imeweka mikakati madhubuti ikiwemo kuunda kitengo chake cha intelijensia na kuunda kanda nane za doria za ushirikiano katika mifumo ya ikolojia ya mbuga ya Selous ambayo imeanza kuwa na mafanikio  ikiwa ni pamoja na kushirikiana na wadau wa uhifadhi kuwezesha upatikanaji wa vitendea kazi na zana kwa ajili ya doria.
Mwaka 2014 Shirika la Kimataifa la Sayansi,Elimu na Utamaduni la umoja wa mataifa(UNESCO) liliiweka Mbuga ya Selous katika Urithi wa asili ulio hatarini Duniani.

Mfuko wa sheria yatoa ruzuku bilioni 18 kwa mafunzo ya wasaidizi wa sheria

LE1 
Kaimu Afisa Mtendaji wa Legal Services Facility (LSF), Bi Scholastica Jullu akizungumza na waandishi wa habari jinsi wasaidizi wa kisheria wanavyosaidia kubadilisha maisha ya watanzania 
LE2 
Jopo la viongozi wa LSF wakionyesha ripoti jinsi wasaidizi wa sheria walivyotatua matatizo ya wananchi nchini, kutoka kushoto ni Meneja Mawasiliano,  Renatus Sona, Afisa Mradi na Haki za wanawake, Bi Fortunata Kitokevya, Kaimu Afisa Mtendaji, Bi Scholastica Jullu, wa pili kulia Meneja Ufuatiliaji na Matokeo, Juma Mwenga na mwisho kulia ni Bw. Masele

MFUKO wa msaada wa kisheria (LSF) umetoa ruzuku kiasi cha shilingi za kitanzania bilioni 18 kwa mashirika yasiyo ya kiserikali yanayojishughulisha utoaji wa msaada wa kisheria kwa ajili ya  mafunzo kwa wasaidizi wa sheria 4,000 nchi nzima.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Kaimu Afisa Mtendaji, Bi Scholastica Jullu amesema kwamba ruzuku imetolewa kuanzia 2012 kwa mashirika hayo ili kuweza kutoa mafunzo kwa wasaidizi wa sheria katika kutatua matatizo yanayowakabili wananchi hasa wa vijijini.
“Dhumuni la uanzishwaji wa mfuko huu ni kulinda haki za binadamu kupitia ujengaji uwezo wa kisheria na kuongeza upatikanaji wa huduma za kisheria kwa watu masikini na wanajamii wengine walio katika hatari ya kukosa haki zao hususani wanawake nchini,” aliongeza Bi Jullu
Tangu kuanzishwa kwake mwaka 2011, LSF imechangia katika kukuza na kulinda haki za binadamu huku ikiweka msisitizo katika ulinzi w haki za wanawake na makundi maalum.
Amesema kwamba kutokana na mafunzo waliopata wasaidizi wa kisheria nchini imewezesha upatikanaji wa huduma za usaidizi wa sharia kwa watanzania takribani milioni thelathini na tano (35 milioni).
Alifafanua kwamba katika kipindi cha kuanzia mwaka 2013 mpaka mwaka 2015 takribani watu 90,000 walipata huduma za msaada wa kisheria na watu 300,000 walifikiwa na elimu ya sheria nchini nzima.
Mambo ambayo wasaidizi wengi wa sheria wanayokutana nayo ni matatizo ya ardhi, ndoa, mirathi, watoto na jinsi ambao asilimia 80 yalishughulikiwa na asilimia 9 tu yalipelekwa kwenye vyombo vingine vya utoaji haki kama vile mahakama, mabaraza ya usuluhishi, serikali za mitaa na polisi.
Bi Jullu alisisitiza mchakato umeanza kwa wadau wa sheria, mashirika yasiyo ya kiserikali na serikali ili kuja na sheria itakayowatambua wasaidizi wa kisheria kwenye mifumo ya serikali.
Kwa upande wake, msaidizi wa kisheria kutoka wilaya ya ilala, Bi Beatrice Bange amesema kwamba changamoto kubwa ni uelewa mdogo wa watanzania wengi kuhusu huduma za wasaidizi wa kisheria na msaada wa kisheria.
Aliongeza kwamba matatizo mengi anayokutana nayo katika wilaya ya ilala ni ndoa, mirathi na matatizo ya ajira kwa wafanyakazi wa kada ya chini.
Utafiti uliofanywa na shirika hilo mwaka jana ulionyesha kuwa zaidi ya asilimia 70 ya watanzania hawana uelewa kuhusu msaada wa kisheria na uwepo wa wasaidizi wa sheria.

TOUR 2016 MALAWI




city in malawi copy
Wakati siku za kuanza msimu mpya wa ligi kuu ya soka Tanzania bara zikiendelea  kuhesabika  kufuatia  hitimisho la msimu jana mwishoni mwa mwezi Mei mwaka huu  na   Yanga kuibuka mabingwa, ratiba ya mwanzo ya michezo ya kirafiki ambayo kikosi cha Mbeya City Fc  kitacheza kwa ajili ya matayarisho ya 2016/17 imetoka.
Kwenye ratiba hiyo, City  imepaga kucheza michezo mitatu ugenini, ambapo itaanza kwa kushuka ‘dimbani’ Kamuzu Stadium jijini Blantyre Juni 18  kucheza na vigogo wa soka nchini Malawi, Big Bullets.
KUPATA SAUTI  NA KUJUA ZAIDI KUHUSU  RATIBA KAMILI YA MICHEZO YA KIRAFIKI 2016
FUNGUA  LINK HII:  http://mbeyacityfc.com/tours/

Jumatatu, 30 Mei 2016


Na Saleh Ally
KWANZA anza kwa kujiuliza kama ungekuwa wewe ndiye Kocha wa Atletico Madrid, Diego Simeone ungejisikiaje? Hakika ni maumivu makali ya moyo.

Lazima ungehisi au kuamini hauna bahati hata kidogo na hasa linapofikia suala la Ligi ya Mabingwa Ulaya. Ndani ya miaka mitatu, Simeone amekiongoza kikosi chake kucheza fainali mara mbili dhidi ya timu moja.

Fainali ya kwanza msimu wa 2013/14 ilikuwa dhidi ya Real Madrid kama ile ya 2015/16.  Zote mbili wamepoteza, moja wakianza kufunga Madrid wakasawazisha, ya usiku wa kuamkia jana wakaanza kufungwa, wakasawazisha na kung’olewa kwa mikwaju ya penalti 5-3.

Mtu asiye na bahati kwa Lugha ya Kihispania anaitwa sin suerte. Unaweza ukampa jina hili Simeone raia wa Argentina anayeonekana ni mtu asiyekata tamaa na kila kitu.

Simeone ni kocha aliyeshinda makombe kadhaa makubwa na muhimu akiwa na Atletico Madrid. Amechukua ubingwa wa La Liga, Copa del Rey, Super Cup Hispania, Europa Cup na Uefa Super  Cup pia.
Si mgeni wa makombe tokea akiwa mchezaji hadi kocha. Lakini kombe pekee ambalo linaonekana kumteleza kila anapojaribu ni lile la Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Rekodi yake na kikosi cha Atletico Madrid inamfanya aonekane mmoja wa makocha bora kabisa kuwahi kuifundisha timu hiyo aliyowahi kuichezea pia.

Tokea ajiunge nayo mwaka 2011, ameiongoza katika mechi 260. Ameshinda 164, sare 52 na kapoteza 44, hii inamfanya awe na wastani wa juu kabisa wa 63.1% ya ushindi. Huu ni wastani wa juu kwa kocha anayefundisha timu kubwa zinazoshiriki michuano yenye ushindani wa juu.


Ukiachana na rekodi za mafanikio yanayopatikana baada ya mchezo, angalia mchezo wenyewe. Mfano, fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Madrid pale jijini Milan, Italia.

Kikosi chake kilicheza vema zaidi, ingawa mwenyewe mwisho alisisitiza kwamba kuna mambo walizidiwa ambayo ndiyo yalifanya wapinzani wao mwisho wabebe ubingwa huo mbele yao.

Simeone anakubali kuwa ana maumivu ya moyo, huenda maumivu hayo yametambaa kwa mashabiki wengi wa soka duniani kote wakiwemo wale ambao si mashabiki wa Atletico Madrid, lakini wanaumia kwa kuwa wanajua kocha huyo Muargentina anaifanya kazi yake kwa ufasaha.

Wanajua kikosi chake kufikia kucheza namna hiyo ni mtu anayejituma, anayefanya jambo kwa juhudi kubwa lakini inaonekana mafanikio yanamkimbia hasa katika Ligi ya Mabingwa.

Kabla ya mechi ya fainali ya Ligi ya Mabingwa jijini Milan, Ronaldo de Lima alipata nafasi ya kumzumngumzia Simeone ambaye alicheza naye timu moja wakiwa Inter Milan ya Italia pia.

Ronaldo alianza kwa kupinga tabia ya Simeone kupandikiza hasira za Kiargentina kwa wachezaji wake, akisema wanakuwa wajeuri na wakatili. Lakini mwisho, akasema ni wagumu kushindika na kocha huyo ni kati ya makocha bora kabisa duniani. 


Kwenye kutengeneza jambo mengi yanatokea, lakini mwisho ni matokeo bora. Simeone amekuwa akiyapata lakini tatizo kubwa ni Ligi ya Mabingwa.

Kinachovutia kwa huyu jamaa ni maneno yake ya mwisho kuhusiana na kuonekana hana bahati ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.

“Sitaki kuonyesha machungu yangu kwenu, lakini najua naumia kiasi gani kufika hapa mara mbili lakini sijarudi nyumbani na kombe. Hakuna ambaye angeweza kufurahia.

“Utaona, wachezaji wamepambana hadi mwisho, wamecheza mechi nyingi sana ndiyo maana dakika 15 za dakika 30 za nyongeza, kila mmoja alionekana ameisha kabisa.

“Najua hatukufika hapa kwa bahati hata kama kweli tuna bahati mbaya. Hatuwezi kuishia hapa, niwaahidi ninabaki Atletico na kwa mara nyingine tunataka kufika fainali ili tuiondoe bahati mbaya,” anasema.

Wengi wanaamini Atletico au Simeone wana bahati mbaya na kombe hilo. Kutokana na wanavyojituma watu wanawaonea huruma, vyote viwili anavikataa.

Utagundua kuwa Simeone si mpiganaji wa muda mfupi, si muoga, si anayetaka kuonewa huruma na anachoamini ni kurejea na kupigana tena ili wafike fainali kumaliza makosa ya fainali mbili zilizopita.

Hakuna ubishi, siku wakifanikiwa kuingia fainali tena, kutwaa kombe hilo halitakuwa na mjadala. Lakini utaona namna kamanda anavyopaswa kuwa, hata kama kaumia anaonyesha bado mapambano yanaendelea.

Simeone anaficha maumivu yake ili kuinua mioyo ya wachezaji wake lakini pia anafuta hisia za wao hawana bahati na Kombe la Ligi ya Mabingwa Ulaya. 

Kama yeye akikubali, maana yake vijana wake wakati mwingine watakuwa hawana sababu ya kulipigania.

Hii ni falsafa ya kiongozi sahihi ambaye maisha yake yote hachoki kupambana na hakati tamaa kwa kuwa hataki kuonewa huruma. Kuhurumiwa ni falsafa ya kusaidiwa au kubebwa, Simeone hataki na tayari amerejea tena kwenye mapambano.


MAFANIKIO YA SIMEONE
AKIWA MCHEZAJI 
Atletico Madrid
La Liga (1): 1995–96
Copa del Rey (1): 1995–96

Inter Milan 
Uefa Cup (1): 1997–98

Lazio (4)
Serie A (1): 1999–2000
Coppa Italia (1): 1999–2000
Supercoppa Italiana (1): 2000
UEFA Super Cup (1): 1999

TIMU YA TAIFA
Argentina (4)
Kombe la Mabara Fifa (1): 1992
Copa America (2): 1991, 1993
Artemio Franchi (1): 1993
Medali ya Fedha Olimpiki (1): 1996

KAMA KOCHA
Estudiantes de La Plata (1)
Ubingwa Argentina (1): Torneo Apertura 2006

River Plate (1)
Ubingwa Argentina (1): Torneo Clausura 2008

Atletico Madrid (5)
La Liga (1): 2013–14
Copa del Rey (1): 2012–13
Supercopa de Espana (1): 2014
UEFA Europa League (1): 2011–12
UEFA Super Cup (1): 2012

BINAFSI 
Kocha Bora wa Mwaka La Liga (2): 2012–13, 2013–14
Tuzo ya Miguel Munoz (1): 2013–14
Kocha Bora wa Mwezi La Liga (2): Oktoba 2013, Novemba 2015