Jumatatu, 28 Septemba 2015

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AONGOZA WANANCHI KUAGA MWILI WA MAREHEMU CELINA KOMBANI, DAR, KUZIKWA KESHO MOROGORO.


 

  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akitoa heshima za mwisho mbele ya Jeneza lenye mwili wa aliyekuwa Waziri Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma,  marehemu Celina Kombani, wakati wa shughuli za kuaga mwili huo zilizofanyika leo Septemba 28, 2015 kwenye Viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam. Marehemu Kombani alifariki Agosti 24 huko nchini India na anatarajia kuzikwa kesho mkoani Morogoro.

Ijumaa, 11 Septemba 2015

UZINDUZI WA MFULULIZO WA VIPINDI VYA MAMA MISITU KUHUSU UZALISHAJI WA MKAA ENDELEVU WAFANYIKA NEW AFRIKA HOTEL LEO JIJINI DAR ES SALAAM

  Viongozi mbalimbali wakiwa meza kuu, kutoka kushoto Mkurugenzi wa Taasisi ya Natural Resource Forum (TNRF), Joseph Olila, Mkurugenzi, Idara ya Misitu na Nyuki wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Gladness Makamba, ambaye alikuwa mgeni rasmi wa uzinduzi huo, Msaidizi wa Balozi, Ubalozi wa UFINI ambao ni wafadhili wa mama misitu, Simo-Pekka Parviainen na Ofisa Mradi Ubalozi wa Finland, William Nambiza.


Jumanne, 8 Septemba 2015

MAKAMO WA RAISI DKT.BILALI ATOA TUZO KWA WAGANGA WASTAAFU.

DKT.AFUNGUA WA MWAKA WA WAGANGA WAKUU DAR




Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akihutubia wakati akifungua rasmi Mkutano wa mwaka wa Waganga Wakuu wa Mikoa, Halmashauri na Wakurugenzi wa Hospitali za Rufaa, ulioanza leo Sept 8, 2015 na Maadhimisho ya Miaka 40 ya Mpango wa Taifa wa Chanjo uliofanyika kwenye Hoteli ya Blue Peal Ubungo Plaza jijini Dar es Salaam. 
 

TAKWIMU WATANGAZA MFUMUKO WA BEI MWEZI AGOSTI


 Mkurugenzi wa Sensa na Takwimu za Jamii Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS), Iphrahim Kwesigabo (kushoto), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam leo mchana kuhusu mfumuko wa bei wa Taifa kwa mwezi Agosti, 2015. Kulia ni Kaimu Meneja wa Idara ya Takwimu za Ajira na Bei, Ruth Minja.

Alhamisi, 3 Septemba 2015



mgombea wa ubunge jimbo la Ubungo kupitia tiketi ya chama cha Mapinduzi(CCM) Dkt Didas Masaburi amewataka Wapinzani wasiweweseke katika kutafuta mtu anayewaloga kwa kuwa mchawi anatoka ndani ya chama chao kwa tabia zao za kukumbatia makapi ambazo haziendani na matakwa ya wananchi.

Dkt Masaburi amemesema hayo leo jijini Dar es Salaam wakati akizungumza na Waandishi wa habari kwenye ofisi za jimbo hilo zilizopo kata ya Manzese akikanusha kuhusika kuchochea yaliyofanyika juzi na baadhi ya vijana na kudhibitiwa na polisi.

"Haipo kwenye akili yangu na wala haitakuwepo kuwachochea vijana waandamane ingawa maandamano ya amani sioni kosa lake na kama maandamano yanaashiria kuunga mkono jambo na kama maandamano yale hayaendani na kudhuru wananchi na kuharibu mali zao,"alisema Makaburi.

Amesema kuwa anaunga mkono hoja za Dkt Slaa na kama angekuwa Chadema angeandamana kwa kuwa hoja hizo zilikuwa ni za kweli na atamkaribisha Mbowe na kumpongeza pamoja na wote watakaokuwa  tayari kuhamia kwenye chama chao. 

Amesema kuwa aliwapokea vijana waliochoshwa na vitendo viovu vinavyofanywa na viongozi wanaounda Umoja wa UKAWA kwa kuwalazimisha kujiunga na umoja huo na kuwa wao wanataka kukiona chama chao(Chadema). 

Mgombea huyo anaendelea kufafanua kuwa vijana hao walipelekwa na mgombea Udiwani wa Ubungo kupitia Chadema na ndiye aliyewaongoza kufanya maandamano baada ya kukatwa katika kura za maoni na kuomba kujiunga na CCM.

"Huyu mgonbea mara tu baada ya kura za maoni za Chadema alikuja kwangu na kusema yupo tayari kujiunga na kuwa  walimfanyia njama hivyo nimpokee na ataleta wafuasi wengi wa Chadema ili chama kishinde na amejiandaa vyema ambapo baadaye alitoka na kuanza kusema maneno,"alisema Masaburi.

Wakati huohuo wanachama 13 kutoka CUF na Chadema wamehamia rasmi kwenye Chama cha Mapinduzi(CCM).

Naye Halima Said  ambaye ni mgombea wa  Ujumbe viti maalum(Chadema)alisema kuwa ameamua kuhamia (CCM)kutokana na wamekuwa wakipotoshwa na na kuwa kiongozi ambaye pia ni mlezi wa chama hicho hayupo.