Ijumaa, 14 Agosti 2015

JWTZ YAWAPA ONYO KALI WANASIASA






 



 



JESHI la Wananchi Tanzania (JWTZ), limekanusha kuwanyang'anya kadi za kupigia kura maofisa na askari wake kama ilivyodaiwa na mmoja wa viongozi wa chama kimoja cha siasa na kutolewa katika vyombo vya habari na mitandao ya kijamii



 



Amezungumza hayo jana Jijini Dar es Salaam wakati alipokutana na  waandishi  habari Mkurugenzi wa Habari na Uhusiano wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ), Kanali Ngemela Lubinga alisema madai hayo siyo ya kweli na kuwa jeshi hilo halijafanya hivyo na wala haliwezi kufanya hivyo.



 



“Wanajeshi hawaruhusiwi kuwa wanachama wa chama chochote cha kisiasa na kuwa mwanajeshi haruhusiwi kuwa shabiki wa chama chochote cha kisiasa”alisema Lubinga.



 



Lubinga alisema Jeshi la Wananchi Tanzania linafanya kazi zake kama 'professional state organ duniani na kuwa mwanajeshi anayekiuka huchukuliwa hatua za kinidhamu za kijeshi wala si za kiraia.



Alisema Jeshi la Wananchi Tanzania limesikitishwa na kauli hiyo iliyotolewa na kiongozi



huyo na amewatakaWananchi na viongozi wa kisiasa wafanye kazi zao za kisiasa na zisianzishwe hoja nje ya maeneo hayo ya kisiasa kwani lugha hizo za upotoshaji zinaweza kuleta hofu, ukakasi na wasiwasi kwa Wananchi.



 



Aliongeza kuwa jeshi hilo linaendelea na shughuli zake kama kawaida halipendi litolewe kauli za upotoshaji, kusikoeleweka ufuatwe utaratibu wa kuuliza kupata majibu ya uhakika kwani Wananchi wanaimani na jeshi lao.

 



Mkurugenzi wa Habari na Uhusiano wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ),


NAPE:WANAOIKIMBIA CCM NI OIL CHAFU

Na Tinah Reuben

KATIBU mwenezi na itikadi wa CCM Nape Nnauye amekanusha habari zilizozagaa katika mitandao ya kijamii kuwa mgombea wao wa uraisi John Pombe Magufuli amehaidi kuwapatia kompyuta mpakato  kila mwalimu pamoja na kila kijiji kupatiwa milioni 50.

Nape amezungumza hayo leo Jijini Dar es salaam alipokuta na Waandishi wa Habari alipokuwa anatoa taarifa hiyo iliyokanusha na kusema kuwa waliotoa taarifa hiyo wanalengo lakuwachafua na kutaka waonekana wameanza kampeni mapema.

Alisema hakuna sehemu ambayo Magufuli aliwahi kuongea kauli hiyo na anawashangaa watu pamoja na mitandao ya kijamii inayoeneza ujumbe huo ambao sio wa kweli hata kidogo.

Aliongeza kuwa wapo watu wasioitakia mema CCM na kwamba wamebaini mbinu hizo chafu na wanazifanyia kazi.



"Watu walianda waraka ule walidai kuona umeandikwa katika ilani ya CCM kitu ambacho sio kweli kwani Ilani imetoka rasmi jana",alisema Nape.

Akitolea ufanunuzi kuhusu kuhama kwa Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Shinyanga Hamis Mgeja,Nape alisema kuwa Mgeja alijitoa baada ya mwanaye wa Kike kushindwa katika mchakato wa Viti maalum mkoa wa Shinyanga.

Alisema kuwa baada ya mwanae kushindwa Mgeja alitaka chama kimbebe mwanae kinyume cha misingi ya chama na alipokataliwa alikasirikia na kutangaza uamuzi wake wa kukihama cham.

"Watu walikimbia CCM wamekimbia kwa mabaya yao pia walionzisha vyama upinzani wote misingi yao ni CCM na kama wanaondoka atushangai.....kwanza walioaznisha hivyo vyama hawajafanikiwa na wanaokwenda hawata fanikiwa,"alisema Nape

Aliongeza kuwa kitendo cha wanachama hao kujiondoa CCM nisawa na fundi anayetoa Dizeli chafu ndani ya injini ya Gari na kuwepa safi.

Alisema kuwa anawashangaa wapinzani wanavyopokea dizeli chafu zinazopelekea injini zao kuwa mbovu na zosizofa kabisa.

Aidha alisema kwa kawadia chama kinautaratibu wa kupokea wanachama wapya hivyo ni kitendo cha kushangaza kuona wapinzani wanapokea wanachama walioshindwa katika vyama vyao.