Jumamosi, 29 Julai 2017

MBUNGE GULAMALI AFANYA ZIARA YA KUONA MAENDELEO YA UFUFUAJI WA KIWANDA CHA MANONGA GENERY

NA RAYMOND URIO

Mbunge wa Jimbo la Manonga kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM), Seif Khamis Gulamali leo ametembelea kiwanda cha Manonga Ginery kinachohusika na kutengeneza pamba, kilichokuwa kimesimama kwa takribani miaka ishirini (20) bila ya kufanya.




Mbunge wa Jimbo la Manonga, Seif Khamis Gulamali akisaliamiana kwa furaha na mmiliki wa kiwanda cha Manonga Genery, Urvesh Rajan leo alipotembelea kuona maendeleo ya ufufuaji wa kiwanda hicho kilichopo Wilayani Igunga kata Choma. ( Picha zote na Raymond Urio )


Mapema leo hii Mbunge Gulamali aliwasili katika eneo la kiwanda hicho, iliyopo Jimbo la Igunga Kata ya Choma akiwa pamoja na Mmiliki wa kiwanda hicho, ndugu Urvesh Rajan pamoja na viongozi wa Serikali za mitaa, wahandisi na mafundi wa viwanda.

Mbunge wa Jimbo la Manonga, Seif Khamis Gulamali (kushoto )akioneshwa moja kamba na mmiliki wa kiwanda cha Manonga Genery, Urvesh Rajan zinatokana na zao la pamba katika kuona maendeleo ya ufufuaji wa kiwanda hicho leo Wilayani Igunga kata ya Choma. Katikati ni katibu wa kiwanda cha Nyuzi Tabora. ( Picha zote na Raymond Urio )
Akizungumza na waandishi wa habari baada ya kutembelea na kuona maendeleo ya ufufuaji wa kiwanda hicho ili kianze kufanya kazi upya, baada ya kukaa kwa miaka kadhaa bila ya kufanya kazi, Mbunge Gulamali alisema, leo nimekuja kuoana maendeleo ya kufufuliwa wa kiwanda hichi ikiwa ni sehemu ya kutaka kutimiza tena ahadi yangu niliyo itoa kwa wanachi wa Igunga na Manonga kwamba lazima kiwanda cha Manonga Ginery, kianze kazi ili wananchi waweze kunufaika katika zao biashara ya pamba na wengine kupata ajira kwa kuendesha maisha na kukuza uchumi wa viwanda nchini.
     
Mmiliki wa kiwanda cha Manonga Genery, Urvesh Rajan akizugumza na Mbunge wa Jimbo la Manonga, Seif Khamis Gulamali (katikati), alipotembelea kuona maendeleo ya ufufuaji wa kiwanda hicho leo Wilayani Igunga kata ya Choma. Kushoto ni Mwenyekiti wa Igombensabo Lazaro Ngullo.      
" Leo nimekuja kuona maendeleo ya ufufuaji wa kiwanda hichi ikiwa ni sehemu yangu ya ahadi niliyo itoa kwa wananchi wangu wa jimbo la Manonga pamoja na Igunga kwamba lazima kiwanda hiki kifanye kazi tena, ili biashara ya zao la pamba lirudi tena na wananchi na waweze kupata ajira katika kiwanda hichi pia kukuza uchumi wa nchi ya Viwanda.

" Kufufuliwa kwa kiwanda hiki ni fursa kubwa ya maendeleo kwa jamii ya wana Igunga na Manonga na hasa wakulima wa zao la pamba hata kwa wananchi wanao lilia ajira, hivyo fursa kwa sasa iko wazi, alisema Gulamali.


Mbunge wa Jimbo la Manonga, Seif Khamis Gulamali akipewa moja ya maelezo ya mashine ya ya zao la pamba ndani ya kiwanda cha Manonga Genery, leo alipotembelea kuona maendeleo ya ufufuaji wa kiwanda hicho kilichopo Wilayani Igunga kata Choma.
Hata hivyo Mbunge Gulamali alisema kuwa bila kumpa ujumbe mmiliki wa kiwanda hiki na kutompa matakwa ya wananchi basi ingekuwa sicho kilichotokea leo, kwahiyo nimetumia uongozi wangu kwaajili ya wananchi wangu ili kuona maendeleo yakiendelea tena katika swala kiwanda na kuona zao la pamba likirudi tenaa kwa kasi katika Jimbo la Igunga na Manonga.
    

Mmiliki wa kiwanda cha Manonga Genery, Urvesh Rajan akimpa maelekezo Mbunge wa Manonga Seif Khamis Gulamali ndani ya kiwanda hicho (katikati), leo alipotembelea na kuona maendeleo ya ufufuaji wa kiwanda kilichopo Wilaya ya Igunga kata ya Choma.

Lakini pia Mbunge Gulamali amewataka wakulima wa zao la pamba kuanza kulima kwa kasi kilimo cha hicho kwa kuwa sasa kiwanda hiki kitaanza kufanya kazi, hivyo juhudi na jitihada zenu ndio itakayoweza kufanya kiwanda hiki kiendelee kwa kuwa nao wanategemea pamba toka kwenu na wao waweze kuuza kwa wafanya biashara wakubwa wa nje ya mipaka na ndani ya nchi.

      
Mbunge wa Jimbo la Manonga, Seif Khamis Gulamali (kushoto) akizungumza na Mwenyekiti wa Igombensabo, Ndug, Emmanuel Ngullu.
Hata hivyo Mmiliki wa kiwanda hicho, ndug, Urvesh Rajan amemshukuru Mbunge Gulamali sambamba na uongozi wa serikali wa kata ya Choma kwa kuweza kuvumilia kwa kipindi chote tangia kiwanda kilivyo simama na hata pale alitoa ombi lake la kukufua tena kiwanda waliweza kumsikilliza na hivyo ni jambo la kushukuru.

Lakini pia mmiliki wa kiwanda hicho ndug, Rajan ametoa ombi kwa wakulima wa zao la pamba kuweza kujitaidi kulima zao hili kwa kasi, kwa kuwa kiwanda kinategmea sana zao hili na si zao jingine, hivyo pesa watakayo ilipa toka kwawakulima wana imani nao itarudi pale watakapo wauzia wafanya biashara na ndio kiwanda kitazidi kuendelea.


Mbunge wa Jimbo la Manonga, Seif Khamis Gulamali akiongozana na viongozi wa serikali pamoja na wahandisi alipotembelea kiwanda hicho leo kilichopo Wilayani Igunga kata ya Choma.

" Ninafurahi Mbunge Gulamali ameitikia wito wangu kwa kuja na kuona maendeleo ya kutaka kufufua kiwanda hichi hivyo, ni jambo zuri kuona kiongozi akiwa sambamba na wewe na mwenye kutaka maendeleo,

" haitochukua muda tutaaenda kuanza kazi hivyo nina waomba wakulima wa zao hili kuchangamkia fursa kwenye ulimaji kwa kuwa fedha watapata za kuendesha maisha hata ajira pamoja na kukuza uchumi wa nchi yetu, alisema. Rajan.

Hata hivyo Mwenyekiti wa kijiji cha Choma, Ndug, Emmanuel Methew alisema kuwa kitendo kilichofanyika leo cha mbunge kuja kuona maendeleo ya ufufuaji wa kiwanda hiki ni kitu kizuri kutokana ni mikaa mingi kutofanya kazi hivyo wakulima walikuwa wanapata tabu katika zao hili, hata mwishowe kukata tamaa katika kulima zao hili kutokana na kufa kwa kiwanda hiki.



Mbunge wa Jimbo la Manonga, Seif Khamis Gulamali (katikati) akisikiliza kwa makini maelekezo kutoka kwa mmiliki wa kiwanda cha Manonga Genery, Urvesh Rajan leo alipotembelea kuona maendeleo ya ufufuaji wa kiwanda hicho kilichopo Wilayani Igunga kata Choma.

"Kiwanda kufufuliwa tena ni jambo zuri hivyo nina imani kuwa wakulima watarudisha nguvu zao kwa kasi kwenye zao hili la pamba kwakuwa ndio moja ya zao kubwa katika mkoa wa Tabora, alisema Methew.

Jumatano, 26 Julai 2017

NA RAYMOND URIO

MBUNGE wa Jimbo la Manonga kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM), Seif Khamis Gulumali amefanya ziara katika kata ya Ntobo Kaskazini, Ngulu, Mwashiku na Choma kwenye Wilaya ya Manonga jana ikiwa ni sehemu ya kutekeleza ilani ya Chama hicho.
   

     Mbunge wa Jimbo la Manonga, Seif Khamis Gulamali akizungumza na wananchi wa kata ya Ntobe kaskazini iliyoko katika Wilaya ya Igunga Mkoa wa Tabora katika moja ya ziara yake leo. wa pili kulia ni Diwani wa kata hiyo, Emmanuel Samson. (Picha zote na Raymond Urio)

Awali Mbunge Gulamali aliwasili katika kata ya Ntobo Kaskazini na kujionea maendeleo yanayoendelea kwenye kata hiyo na kuhaidi kuendelea kutoa huduma kadiri inavyowezekana. Hata hivyo Mbunge Gulumali alitoa shukrani kwa wanachi wote walio weza kumchagua ili kuwa mbunge wao na kuweza kuwatumikia.

'Na washukuru wananchi wote wa Kata ya Ntobo kwa kuweza kunichagua na kuwa kiongozi wenu hivyo wajibu wangu ni kuendelea kuwahudumia kama niliweza kuhaidi. alisema Gulumali.
Hata hivyo Gulamali amechangia mabati 20 pamoja na mbao 50 za ujenzi wa ofisi za Chama hicho katika Kata hiyo. Lakini pia Diwani wa kata hiyo Emmanuel Samson alitoa shukrani kama sehemu ya kuwawakilisha waanachi wa kata hiyo kwa msaada huo pamoja na kuhaidi kumuunga mkono Mbunge huyo.

        Mbunge wa Jimbo la Manonga, Seif Khamis Gulamali akisikiliza maoni ya wananchi wa kata ya Ntobe kaskazini iliyoko katika Wilaya ya Igunga Mkoa wa Tabora katika moja ya ziara yake leo. kulia kwake ni Diwani wa kata hiyo, Emmanuel Samson.

Hata hivyo Mbunge Gulamali aliweza pia kuwatembelea wanachi wa kata ya Ngulu, kwa kuangalia maendeeo yanayoendelea baada ya awali kuchangia fedha kwaajili ya ukarabati wa barabara ya barabara kwenye kata hiyo.

Lakini pia Gulamali amehaidi kuchangia mifuko ya seruji kwa ajili ya kutengeneza choo cha Hospitali na nyumba ya Mganga Mkuu katika Hosptali ya kata.

     Mbunge wa Jimbo la Manonga, Seif Khamis Gulamali akisikiliza maoni ya wananchi wa kata ya Mwashiku iliyoko katika Wilaya ya Igunga Mkoa wa Tabora katika moja ya ziara yake leo.


Hata hivyo Gulamali aliweza pia kutembelea wananchi wa kata ya Choma pamoja na Mwashiku na kuwaeleza juu ya ufufuaji wa kiwanda cha ... kilichokuwa kimetelekezwa na Mmilimki .... wa kiwanda hicho kwamuda mrefu bila hata kufanya kazi.



     Mbunge wa Jimbo la Manonga, Seif Khamis Gulamali akizungumza na wananchi wa kata ya Choma iliyoko katika Wilaya ya Igunga Mkoa wa Tabora katika moja ya ziara yake leo

Lakini pia aliwahaidi pindi kiwanda hicho kitakapo fufuliwa itakuwa ni nafasi nzuri kwa wananchi wa Choma pamoja na wengine walio katika Wilaya ya Igunga ili waweze kupata kazi katika kiwanda hicho na kuweza kuendesha maisha yao na familia zao.


Jumamosi, 17 Desemba 2016

PROF. MBARAWA ATOA MAAGIZO KWA WAKUU WA WILAYA

prof
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa akizungumza na wakazi wa kijiji cha Kisorya Wilayani Bunda, mkoani Mara wakati alipotembelea na kukagua kivuko cha MV Ujenzi kinachotoa huduma kati ya Rugenzi Ukerewe na Kisorya wilayani hapo.
prof-1                                            
Mbunge wa Mwibara Mhe. Kange Rugora (wa pili kushoto), akiongea na Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa (wa pili kulia), katika ziara yake mkoani Mara wakati alipotembelea na kukagua kivuko cha MV Ujenzi kinachotoa huduma kati ya Rugenzi Ukerewe na Kisorya kilichopo Wilaya ya Bunda.
prof-2
Meneja wa Wakala wa Ufundi na Umeme Nchini (TEMESA), Eng. Fredinand Mishamo akitoa maelezo kwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa wakati alipotembelea na kukagua kivuko cha MV Ujenzi kinachotoa huduma kati ya Rugenzi Ukerewe na Kisorya wilayani hapo.
prof-3
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa, akishuka kutoka katika kivuko cha MV Ujenzi kinachotoa huduma kati ya Rugenzi Ukerewe na Kisorya wilayani Bunda, wakati alipotembelea na kukagua kivuko hicho.
prof-4
Muonekano wa kivuko cha MV Ujenzi kinachotoa huduma kati ya Kijiji cha Rugenzi Ukerewe na Kisorya wilayani Bunda.
prof-5
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa, akikagua kivuko cha MV Mara kinachotoa huduma kati ya Kijiji cha Mugara na Kuruge wilayani Bunda, wakati alipotembelea na kukagua kivuko hicho. Kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Bunda, Mwl. Lydia Bupilipili.

kero
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa, akisikiliza kero kutoka kwa mmoja wa wananchi wa Kijiji cha Iramba, Wilaya ya Bunda, mara baada ya kukagua kivuko cha MV Mara na kuongea na wananchi hao.
athari
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa, akiangalia athari za miundombinu ya barabara kwenye Daraja la Burendabufwe lilibomoka kutokana na mvua zilizonyesha hivi karibuni katika barabara ya Kibara-Iramba wilayani Bunda.
prof-6
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa, akicheza nyimbo za asili za kabila la wakerewe, wilaya ya Bunda kabla ya kuongea na wakazi wa kijiji cha Iramba, mkoani Mara.
prof-7

Mbunge wa jimbo la Mwibara, Mhe. Kange Lugora (kushoto) akiteta jambo na Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa (kulia), wakati wa mkutano wa hadhara uliofanyika katika kijiji cha Mwibara.
………………….

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa amewaagiza Wakuu wa Wilaya  na Wakurugenzi wa Halmashauri kote  nchini 
kuhakikisha wanafuatilia na kusimamia kwa ukaribu utekelezaji 
wa miradi mbalimbali  inayotekelezwa kwa kutumia Mfuko wa Barabara katika maeneo yao.
Akizungumza Wilayani Bunda, mkoani Mara baada ya kupokea taarifa ya hali ya miundombinu Wilayani hapo, Waziri Prof. Mbarawa amesema kuwa hatua hiyo pia itasaidia kudhibiti upotevu wa fedha za wananchi pamoja na kuongeza kasi ya utekelezaji wa miradi hiyo.
“Nawaagiza Wakuu wa Wilaya wote na Watendaji wa Halmashauri kuhakikisha wanasimamia ipasavyo miradi inayotekelezwa kwa kutumia fedha za Mfuko wa Barabara ambazo ni fedha za wananchi”, ameagiza Prof. Mbarawa.
Aidha, amemhakikishia Mkuu wa Wilaya ya Bunda kuwa Serikali itaendea kufanya kila linalowezekana kuimarisha miundombinu kwa maendeleo ya watanzania.
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya hiyo Mwl.Lydia Bupilipili, amesema kuwa wilaya hiyo imejiwekea utaratibu  wa kufuatilia miradi hiyo lakini pia inawaelimisha watendaji kata na vijiji kuhusiana na sheria ya barabara.
Katika hatua nyingine, Waziri Mbarawa ametembelea Kivuko cha Mv Mara na Mv Ujenzi na kuahidi kuboresha utoaji wa huduma katika vivuko hivyo ikiwemo ujenzi wa jengo la abiria katika kijiji cha Iramba na Kisorya.
Amewasisitiza kudhibiti mapato yatokanayo na vivuko hivyo ili kuweza kuongeza ufanisi na utendaji wa vivuko hivyo.
Naye, Meneja wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA), Mkoani Mara amemhakikishia Waziri huyo kufunga mifumo ya kielektroniki ili kudhibiti mianya ya upotevu wa mapato.
Aidha, Waziri Prof. Mbarawa ametembelea barabara ya Busambala – Kisorya (KM 120), na kutoridhishwa na hatua ya ujenzi wake, hivyo kutoa miezi sita kwa Mkandarasi wa Kampuni ya ujenzi ya Nyanza Roads Works anayejenga barabara hiyo kukamilisha ujenzi wake.
Prof. Mbarawa ameanza ziara yake ya siku mbili mkoani Mara ambapo anatarajia kukagua miradi mbalimbali inayotekelezwa na Wizara yake.
Imetolewa na Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, kitengo cha Mawasiliano Serikalini

ZIARA YA MAJALIWA HALMASHAURI YA ARUSHA

ngoma
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitazama ngoma ya wanawake wa kimasai baada ya kuzindua mradi wa maji wa kijiji cha Ondenderet wilayani Arusha Desemba 27, 2016. kushoto ni Mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
piga
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akipiga ngoma ya msanja iliyokuwa ikichezwa na wnanwake wa Arusha baada ya kuwasili kwenye kijiji cha Ondenderet wilayani Arusha Desemba 27, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
ziduka
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizundua mradi wa maji wa kijiji cha Ondenderet wilayani Arusha Desemba 27, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
twisha
 Waziri Mkuu, Kassim Majliwa akimtwisha ndoo ya maji bibi Agness Silima ikiwa ni ishara ya kuzindua mradi wa maji wa kijiji cha Onderet wilayani Arusha Desemba 17, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
pikaaaa
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na wananchi wa eneo la Kwamrombo wilayani Arusha ambao   walijipanga kwa wingi barabarani na kumshawishi kusimama  ili kuzungumza nao. Alikuwa katika ziara ya mkoa wa Arusha  Desemba 27, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
pikaaa-2222
Waziri Mkuu, Kassim Majliwa kizungumza na wananchi wa kijiji cha Ormapinu  wilayani Arusha ambao wlijipanga  kwa wingi barabarani na kumshawishi kusismama ili kuwasikiliza. Alikuwa katika ziara ya mkoa wa Arusha Desemba 27, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

RAIS DK. MAGUFULI AMPA KAZI PROFESA YUNUS MGAYA KUWA MKURUGENZI WA (NIMR), ALIAHIDI KUMPA KAZI NYINGINE BAADA YA KUTUMBULIWA (TCU)

nimr

NAPE AFUNGUA MASHINDANO YA MICHEZO MBALIMBALI WILAYANI KARATU.

ria1
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye akipiga baruti juu kuashiria ufunguzi rasmi wa mashindano ya michezo mbalimbali yanayofanyika Wilayani Karatu (Karatu Sports Festival).
ria2
Wanariadha wanaoshiriki mashindano ya michezo mbalimbali yanayofanyika Wilayani Karatu wakijandaa kuanza kukimbia wakati wa uzinduzi wa mashindano hayo uliofanywa na Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye Disemba 17/2016.
ria3
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye akisalimkia na baadhi ya washiriki wa mashindano ya michezo mbalimbali yanayofanyika Wilayani Karatu.
ria4
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye akisalimkia na baadhi ya washiriki wa mashindano ya michezo mbalimbali yanayofanyika Wilayani Karatu.
ria5

KAMPUNI YA NAMAINGO KUGAWA SUNGURA 600 KWA WAJASIRIAMALI DAR

sugu
 Mkurugenzi wa Kampuni ya Namaingo Business Agency, Biubwa Ibrahim (kulia0 na Meneja Mradi wa Sungura wa kampuni hiyo, Amos Misinde wakionesha kwa wanahabari, Dar es Salaam jana,  baadhi ya sungura 600 zitakazogawiwa leo kwa Wajasiriamali 2000. (PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA;KAMANDA WA MATUKIO BLOG)


Na Richard mwaikenda
KAMPUNI ya Namaingo, kugawa sungura 600 kwa Wajasiriamali 2000 Dar es Salaam leo, ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa mradi huo mkubwa nchini.


Mpango huo ulitangazwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Namaingo Business Agency, Biubwa Ibrahim katika mkutano na waandishi wa habari eneo la mradi huo wa Sungura eneo la Majohe, Dar es Salaam jana.


Alisema kuwa walengwa watakaonufaika na mradi huo, ni Wakulima  3000 waliojiunga katika vikundi vya ushirika 30 kutoka katika wilaya za Mkoa wa Dar es Salaam ambapo kila kikundi kina wakulima 50.


Biubwa alisema  kwa kuanzia ni vikundi 20 vya ushirika vyenye Wajasiriamali 2000 ndiyo watakaogawiwa sungura leo na wengine 1000 watafuata baada ya sungura hao kuzaliana. Kila kikundi kipatiwa sungura wazazi 27 na dume watatu.


“Hadi sasa tuna vikundi  30 vya ushirika, tutaanza mradi na vikundi 20 vitakavyopatiwa sungura kama mbegu ya kuzalisha kwa ajili ya kupatiwa vikundi vingine 10 vilivyobakia,” alisema Biubwa. 


Alisema kuwa ndani ya miezi mitano sungura wazazi 540 watakuwa wamezaa mara tatu, hivyo kuwa na watoto 9,720. Jumla hiyo inatokana na kila sungura mzazi mmoja kuzaa watoto 6.


Alisema mpango utakaofuata ni kila mwanachama kugawiwa sungura 8 kwa ajili ya kuendeleza ufugaji na kupata kipato kitakachosaidia katika maisha yao.


Akielezea faida ya ufugaji wa sungura, Meneja wa Mradi huo, Amos  Misinde alisema kuwa nyama ya sungura inahitajika sana na kwamba hadi sasa zinahitajika tani 5 za nyama hiyo kwa wiki. Sungura wakifugwa kwa uangalizi mzuri mmoja anaweza kufikisha uzito wa kilo 8 ambapo kilo moja ya nyama ni sh. 8,500.


Wanahabari walipata wasaa wa kutembezwa kwenye mabanda kuwaona sungura hao walioingizwa nchini wiki hii kutoka Kenya.
Sungura hao wapo chini ya uangalizi wa watalaamu kutoka Rabbit Republic ya Kenya, Suma JKT na Namaingo Business Agency pamona na watalaam wengine kutoka Chuo Kikuu cha Kilimo (SUA).




 Biubwa akimwingiza mmoja wa  sungura kwenye banda eneo la Majohe, Gongo la Mboto, Dar es Salaam
 Biubwa akifafanua jambo mbele ya wanahabari alipokuwa akielezea kuhusu mradi huo
 Wanahabari wakisikiliza kwa makini wakati Biubwa akizungumza nao
 Meneja Mradi wa Sungura wa Kampuni ya Namaingo, Amos Misinde akionesha sungura waliokwenye mabanda tayari kuwagawia wajasiriamali leo
 Mabanda yenye sungura
 Sungura wanaosubiri kuwekwa kwenye mabanda
 Sungura akila majani
 Meneja Masidizi wa Mradi wa Sungura, Denis Rugezia akiwa na sungura tayari kumpanga kwenye moja ya mabanda
 Mmoja wa wafanyakazi akiwapeleka sungura kwenye mabanda. Sungura hao wamewasili kutoka Kenya.

 Mtaalamu kutoka Chuo Kikuu cha Kilimo (SUA), akiwanesha wanahabari sungura dume
 Mmiliki wa Kamanda wa Matukio Blog, Richard Mwaikenda akiangalia mabanda yenye sungura
 Mmiliki wa Bongo weekend blog Khadija Kalili akikagua mabanda hayo
 Mmoja wa wanufaika wa mradi huo akiwa kwenye mabanda hayo
Makao Makuu ya Mradi wa Sungura eneo la Majohe, Dar es Salaam.