Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (Nemc), limesema halitasita kuvifungia viwanda vitakavyokwenda kinyume na sheria na utaratibu wa kutunza mazingira.
Kauli hiyo imekuja takriban sita tano tangu Nemc itangaze kukifungia kiwanda cha nguo cha 21 Century cha Morogoro kutokana na kushindwa kutakatisha maji ya kiwandani kabla ya kuruhusiwa kuingia mto Ruvu.
Ofisa Mwandamizi wa Mazingira wa Nemc, Glory Kombe alisema hayo juzi wakatia akuzungumzia hatua za kuchukuliwa dhidi ya uchafuzi wa mazingira unaosababishwa na shughuli za viwanda.
Kufungiwa kwa kiwanda hicho cha Morogoro kumekuja baada ya awali kufungiwa kiwanda cha kutengeneza sementi (Twiga cement) cha Dar es Salaam.
Kiwanda hicho ambacho sasa kimeruhusiwa kuendelea na kazi, kilifungwa kutokana na kushindwa kudhibiri vumbi lililokuwa likitokana na uzalishajiwa bidhaa hiyo, hivyo kuleta athari kwa wananchi.
Kombe alisema Nemc hatakuwa tayari kuona viwanda vikichafua mazingira kama vile hakuna sheria zinazowaelekeza namna bora ya kulinda mazingara ili kuepusha hatari.
Jumanne, 24 Februari 2015
Jumatatu, 23 Februari 2015
FURSA MILIONI 885 ZA CHINA,TANZANIA KUNUFAIKA NAZO
Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii
Gavana wa Benki Kuu nchini,Profesa Beno Ndulu amesema kazi milioni 885 za nchi ya jamhuri ya watu wa China wameshindwa kuziendesha,hivyo Tanzania inaweza kufaidika na kazi hizo katika kuongeza pato la taifa kwa sekta ya viwanda.
Profesa Ndulu ameyasema hayo leo katika warsha ya kujadili chamgamoto na jinsi ya kukabiliana nazo kwa ukuaji wa Uchumi kutokana na rasilimali zilizopo nchini.
Amesema pato la taifa katika sekta ya viwanda limezidi kukua kwa dola za Marekani milioni 1.3 hiyo ni tofauti na miaka 10 iliyopita,hivyo kutokana na hali hiyo sekta ya viwanda itazidi kuongeza pato la taifa kuliko ilivyo sasa.
Amesema sekta nyingine inayoongeza pato la taifa ni sekta ya usafirishaji ambayo imechangia pato la taifa dola za Kimarekani milioni 8.6.
Kwa upande wa Mbunge wa Kigoma Kaskazini na Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Mashirika ya Umma (PAC),Zitto Kabwe amesema uchumi umeshuka na uchumi uliopo unashikiliwa na watu wachache ambao ni wafanyabiashara
Amesema serikali iweke kipaumbele katika kilimo kutokana na kuwa na hali mbaya ya kiuchumi na wananchi wasifurahie kuwepo hali ya uchumi iliyopo sasa.
WALIODAI AJIRA JKT KWA KUANDAMANA HADI IKULU WAKAMATWA
Na Tinah Reuben
Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limesema kuwa kutekwa kwa kiongozi wa kupanga maandamano kwa waliochwa na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT),George Mgoba ni mchezo wa kuigiza ‘filamu’ na litaendelea kufanya uchunguzi wa kina wa tukio hilo.
Akizungumza leo na waandishi wa habari ofisini kwake.Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam,Suleiman Kova (pichani),amesema kuwa tukio la kutekwa kwa George limekaa kama mchezo wa kuigiza hivyo jeshi la polisi linafanya uchunguzi walihusika na tukio hilo.
Amesema wa umoja wa vijana hao walioandamana na kuongozwa na ,George haujasajiliwa sehemu yeyote kwa mamlaka zinahusika na usajili wa asasi nchini.
Kamanda Kova amesema vijana hao walidai kuwa wataajiriwa na jeshi hilo jambo ambalo halina ukweli wowote kutoka katika mamlaka ya jeshi hilo.
Aidha amesema vijana hao suala la ajira sio la serikali kutokana na ujuzi walioupata wanaweza kujiajiri sehemu yeyote kutokana ma mafunzo waliyapata katika Jeshi la Kujenga Taifa (JKT).
Kamanda Kova amesema kuna vijana wanne wamekamatwa ambao walikuwa katika mpango wa kuratibu maandamano ya kwenda Ikulu ili Rais Jakaya Kikwete awasikilize.
Amesema Makamu Mwenyekiti wa umoja huo ,Barali Kiwango amesalimisha mikoni mwa jeshi la Polisi ambapo wanaendelea kufanya naye mahojiano na kuwataka vijana hao wasikutane kwa ajili ya maandamano na wataobainika kufanya hivyo nguvu ya dola itachukua mkondo wake..
Ijumaa, 20 Februari 2015
Robert Mugabe atimiza miaka 91
Kiongozi wa nchi mzee kuliko wote duniani, Rais Robert Mugabe wa Zimbabwe, Jumamosi wiki hii anatimiza miaka 91 ya kuzaliwa, huku sherehe kubwa ikimsubiri.
Sherehe hiyo kubwa imezua gumzo hasa kutokana na kiasi kikubwa cha pesa kitakachotumika wakati wananchi wengi wa nchi hiyo wanaishi katika hali ya umaskini kupindukia.
Mugabe aliingia madarakani mwaka 1980 na tangu wakati huo ameendelea kubaki kwenye madaraka hadi sasa. Pia ana mpango wa kuwania kiti cha urais katika uchaguzi ujao wa nchi hiyo.
Utawala wa Mugabe umekuwa ukilalamikiwa na jumuiya za kimataifa kutokana na ukiukwaji wa haki za binadamu, kutumia vyombo vya dola kuwabana wapinzani.
Lakini sera yake ya kuwapokonya ardhi baadhi ya walowezi wa Uingereza, iliongeza mjadala wa namna anavyoendesha serikali yake.
Wafunga ndoa wakiwa wamelala kwenye majeneza
Ilikuwa
kama filamu au mchezo wa kuigiza, lakini kilichotokea kilikuwa kweli
mbele ya macho ya watu. Ndoa 10 zilifungwa mwishoni mwa wiki iliyopita
na kilichoshangaza zaidi ni wanandoa hao kufunga ndoa wakiwa kwenye
majeneza katika mji wa Wat Takien, Jimbo la Nonthaburi nchini Bangkok.
Wandoa hao walifikia uamuzi huo kutokana na imani kuwa kwa kulala kwenye jeneza muda mfupi baada ya kufunga ndo, kungeondoa mikosi kwenye maisha na kuwafanya kuishi maisha ya furaha.
Wanandoa hao walipanga majeneza yao yakiwa na rangi ya pinki na wakiwa ndani yake walilala pamoja kama vile maiti inavyohifadhiwa tayari kwa kuzikwa.
Majeneza hayo yalitengenezwa maalumu kwa ajili ya kuweza kulala watu wawili bila shida.
Kadhalika, wakiwa ndani ya majeneza, kila mmoja alishika ua na kulikumbatia kifuani, kabla viongozi wa kimila kufunika jeneza hilo kwa kutumia kitambaa cheupe ikiwa ni ishara ya kuondoa mikosi.
Kwa mujibu wa gazeti la Bangkok Post, wanandoa hao baada ya kutoka kwenye majeneza hayo, huanza maisha mapya wakiwa hawana mikosi kwa vile tayari inakuwa imeondolewa kwenye baada ya kumalziika ibada.
Hata hivyo, tukio hilo siyo mara ya kwanza kutokea nchini humo, kwani mwaka jana wakati wa shehere za siku ya wapendanao zilifanyika na kisha kufuatia na sherehe za kimila kama ilivyokuwa mwaka huu.
Lilipofanyika tukio kama hilo mwaka jana, hakukuwa na mapngo wa kulifanya tena katika mji wa Makha Bucha, lakini kutokana na maombi mengi kutoka kwa watu, ililazimu ukufanyika tena.
Wandoa hao walifikia uamuzi huo kutokana na imani kuwa kwa kulala kwenye jeneza muda mfupi baada ya kufunga ndo, kungeondoa mikosi kwenye maisha na kuwafanya kuishi maisha ya furaha.
Wanandoa hao walipanga majeneza yao yakiwa na rangi ya pinki na wakiwa ndani yake walilala pamoja kama vile maiti inavyohifadhiwa tayari kwa kuzikwa.
Majeneza hayo yalitengenezwa maalumu kwa ajili ya kuweza kulala watu wawili bila shida.
Kadhalika, wakiwa ndani ya majeneza, kila mmoja alishika ua na kulikumbatia kifuani, kabla viongozi wa kimila kufunika jeneza hilo kwa kutumia kitambaa cheupe ikiwa ni ishara ya kuondoa mikosi.
Kwa mujibu wa gazeti la Bangkok Post, wanandoa hao baada ya kutoka kwenye majeneza hayo, huanza maisha mapya wakiwa hawana mikosi kwa vile tayari inakuwa imeondolewa kwenye baada ya kumalziika ibada.
Hata hivyo, tukio hilo siyo mara ya kwanza kutokea nchini humo, kwani mwaka jana wakati wa shehere za siku ya wapendanao zilifanyika na kisha kufuatia na sherehe za kimila kama ilivyokuwa mwaka huu.
Lilipofanyika tukio kama hilo mwaka jana, hakukuwa na mapngo wa kulifanya tena katika mji wa Makha Bucha, lakini kutokana na maombi mengi kutoka kwa watu, ililazimu ukufanyika tena.
Alhamisi, 5 Februari 2015
Vikosi vya Chad vyawaua wapiganaji 200.
Jeshi la Chad linasema kuwa limewaua
wapiganaji 200 wa kundi la boko Haram huku nao wakipoteza wanajeshi 9
katika vita vikali vya kuuteka mji muhimu kazkazni mashariki mwa
Nigeria.
Wapiganaji wa Boko Haram waliwauwa watu 30 baada ya kutoroka mapigano hayo na kuelekea nchini Cameroon,mkaazi mmoja amesema.Vilikuwa vita vikali vilivyowahusisha wapiganaji wa Chad tangu waingie Nigeria ili kukabiliana na wanamgambo hao.
Vikosi vya Chad na vile vya Cameroon pia vinaendelea kuangusha mabomu katika msitu mkubwa wa sambiza ambapo wapiganaji hao wana kambi.
Boko Haram wanadaiwa kutorokea katika katika msitu huo baada ya kuwateka zaidi ya wasichana 200 wa shule mnamo mwezi Aprili kutoka mji wa kazkazini mashariki mwa Nigeria wa Chibok.
Haijulikani iwapo bado washichana hao wapo katika msitu huo.
Katibu Mkuu wa Chama cha Kijamii (CCK), Renatus Muabhi (katikati), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam leo, kwa niaba ya vyama 10 visivyo na uwakilishi wa wabunge Bungeni wakati wakitoa tamko kuhusu viongozi wa dini kutojihusisha na masuala ya siasa wakati huu wa kuelekea uchaguzi mkuu 2015 . Kutoka kushoto ni Katibu Mkuu wa Chama cha Sauti ya Umma (Sau), Ali Kaniki na Katibu Mkuu wa Chama cha Wakulima Tanzania (AFP), Rashid Rai.
Katibu Mkuu wa Chama cha Wakulima Tanzania (AFP), Rashid Rai (katikati), akizungumza katika mkutano huo. Kulia ni Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha UMD, Moshi Kigundula na Katibu Mkuu wa Chama cha Kijamii (CCK), Renatus Muabhi.
Katibu Mkuu wa Chama cha Sauti ya Umma (Sau), Ali Kaniki (kulia), akizungumza katika mkutano huo kuhusu suala zima la Nishati ya umeme nchini na sakata la Escrow. Kushoto Kiongozi wa chama cha Jahazi Asilia Mbwana Kibande na Amina Mcheka kutoka chama cha Chausta.
Naibu Katibu Mkuu wa wa Chama cha UPDP, Felix Makuwa (kulia), akichangia jambo kwenye mkutano huo.
Mwakilishi kutoka chama cha Chausta, Amina Mcheka akitoa ufafanuzi wa masuala kadhaa katika mkutano huo.
Mwakilishi kutoka chama cha Jahazi Asilia, Mbwana Kibande (kushoto) naye akichangia jambo kwenye mkutano huo.
viongozi wa vyama hivyo wakiwa kwenye mkutano huo.
Wanahabari wakichukua taarifa hizo.
…………………………………………………………………………….
Dotto Mwaibale
VYAMA kumi visivyokuwa na uwakilishi bungeni vimewaonya viongozi wa dini nchini katika kipindi cha mwaka huu ambako kutafanyika uchaguzi mkuu kutojihusisha na masuala ya siasa kwa kuwa kufanya hivyo ni kinyume cha sheria na katiba ya nchi.
Aidha, vyama hivyo vimeitaka serikali kupitia upya mikataba ya makampuni yanayozalisha umeme nchini kwa kuwa baadhi yanauza nishati hiyo kwa gharama kubwa licha ya kwamba baadhi yanazalisha umeme kwa kutumia gesi na kusababisha wananchi kuingia gharama kubwa.
Tamko hilo limetolewa na makatibu wakuu wa vyama vya AFP, CCK, SAU, UMD, Chausta, UPDP, NRA, Jahazi, Chauma na DP ikiwa ni salamu za kukaribisha mwaka mpya wa 2015.
Katibu Mkuu wa AFP, Rashid Rai, akisoma tamko hilo jana jijini Dar es Salaam kwa niaba ya wenzake, alisema katika miaka ya hivi karibuni kumejitokeza tabia ya viongozi wa dini kujihusisha na masuala ya siasa hususani kipindi cha uchaguzi mkuu na hivyo kuwachanganya wananchi.
Rai alisema viongozi hao wamekuwa wakitoa matamko kwenye vyombo vya habari kupendekeza au kutoa sifa ya kiongozi anayefaa kuongoza nchi au asiyefaa kupewa nafasi ya uongozi wa umma katika Taifa.
Alisema viongozi wa dini lazima watambue kuwa sheria inazuia viongozi wa dini kujihusisha na masuala ya siasa kwani hali hiyo inawachanganya wananchi kushindwa kujua kama viongozi hao wamebadilisha majukumu yao.
“Unakuta kiongozi wa dini anasema Rais ajaye awe ni mwadilifu na mcha Mungu, au anasema kiongozi huyu ni chaguo la Mungu, maana yake ni nini,kila dini au dhehebu lina vigezo vyake vya uadilifu na ucha Mungu,”alisema.
Rai alisema kama viongozi wa dini wanaona watu waliopo kwenye siasa wanafaidi sana ni bora wakaachana na masuala ya kuhubiri dini badala yake waanzishe vyama vya siasa au wajiunge na vyama vya siasa ili waendelee kupata neema wanayohisi inapatikana huko.
Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Chama cha SAU, Ali Kaniki, alisema sakata la akaunti ya Tegeta Escrow limetoa fundisho kwa serikali kuona umuhimu wa kupitia upya mikata ya makapuni yote ya makampuni yanayozalisha umeme.
Alisema baadhi ya makampuni yanayozalisha umeme na kuliuzia Shirika la Umeme nchini (Tanesco) yanatoza tozo kubwa hali ambayo imekuwa ikisababisha gharama za umeme kuwa kubwa hapa nchini.
“Tunayo makampuni yanayozalisha umeme hapa nchini ambayo ni Songas, IPTL Aggreko na Symbion, ukiangalia yote IPTL ndiyo inayouza umeme kwa bei ndogo ukilinganisha na mengi, tunataka serikali ipitie mikataba ya makampuni haya,”alisema.
Naye Katibu Mkuu wa CCK, Renatus Muabhi, alisema katika hali ya kushangaza baadhi ya makampuni licha ya kwamba yanatumia nishati ya gesi kuzalisha umeme lakini yamekuwa yakiuza umeme kwa bei ya juu. (Imeandaliwa na mtandao wa www. habari za jamii.com)
Jisajili kwenye:
Machapisho (Atom)